Mtoto wa Jicho, Ushauri na Tiba

Nini maana ya Mtoto wa jicho?

Mtoto wa jicho ni hali ya kujitokeza kwa wingu kwenye lensi ya jicho. Mtoto wa jicho huanza pale pritoni ya kwenye jicho inapojikusanya na kuzuia lensi kutuma picha kwenye eneo a nyuma la jicho la retina. Kazi ya retina ni kubadili mwanga unaokuja kupitia lensi kuwa taarifa. Kisha taarifa hizi hutumwa kweye ubongo ili uweze kutafasiri ni kitu gani ulichokiona.

Mtoto wa jicho huanza taratibu mpaka kuathiri uwezo wako wa kuona. Unaweza kupata mtoto wa jicho katika macho yako yote mawili. Wazee na watu wazima wanaugua sana mtoto wa jicho.

Dalili za mtoto wa jicho

Dalili kubwa za mtoto wa jicho ni pamoja na

  • kuona kitu kama winguwingu ama picha iliyosambaa
  • kushindwa kuona vizuri nyakati za usiku
  • kuona rangi kama zimesambaa
  • kuona picha mbilimbili
  • uhitaji wa kubadili miwani mara kwa mara
  • kushindwa kuhimili mwangwa mkali

Nini kinapelekea upate mtoto wa jicho?

Kuna sababu nyingi zinapeleka mtoto wa jicho, Sababu hizi ni pamoja na

  • uzalishaji wa kemikali sumu kwa wingi(oxidants)
  • kuvuta sigara
  • miale mikali ya mwanga
  • matumizi ya muda mrefu ya dawa za steroids
  • kuugua kisukari na
  • tiba ya mionzi (radiotherapy)

Aina za mtoto wa jicho

Kuna aina tofauti za mtoto wa jicho. Aina hizi zinagawanywa kulingana na mahali na jinsi gani zimetokea.

  • Nuclear cataracts: inatokea katikati ya lensi ya jicho
  • Cortical cataracts: inatokea pembeni ya mboni ya jicho
  • Posterior cataracts: inatokea nyuma ya lensi ya jicho
  • Congenital cataracts: inatokea wakati wa kuzaliwa mtoto ama katika mwaka wa kwanza wa mtoto.
  • Secondary cataracts: inasababishwa na magonjwa ama matumizi ya dawa fulani. Magonjwa yanayopelekea ni pamoja na kisukari.
  • Traumatic cataracts: inatokea baada ya kupata ajali ya jicho
  • Radiation cataracts: mtoto wa jicho kutokana na tiba ya mionzi kutibu saratani.

Mazingira hatarishi yanayopelekea upate tatizo

  • umri mkubwa
  • matumizi makubwa ya pombe
  • kuvuta sigara
  • uzito mkubwa na kitambi
  • presha kubwa ya damu
  • majeraha kwenye macho
  • kukaa sana juani
  • familia yenye historia ya kuugua mtoto wa jicho kuugua kisukari na
  • mgonjwa alieye kwenye tiba ya mionzi

Vipimo

Daktari atakupima kucheki uwezo wako wa kuona kwa kutumia kipimo cha tonometry. Vipimo vingine utakavyofanyiwa ni pamoja na kucheki uwezo wako wa kuhimili mwanga mkali na rangi tofauti.

Tiba ya mtoto wa jicho

Kama hupendelei kufanyiwa upasuaji, daktari anaweza kukuweka kwenye tiba ya muda mrefu kusaidia kupunguza dalili mbaya. Utahitaji miwani yenye kioo kinene.

Upasuaji: Madaktari watapendekeza ufanyiwe upasuaji endapo tatizo linakuzuia kufanya kazi zako za kila siku kamakusoma na kuendesha chombo cha moto. Pia kama una tatizo lingine la macho, itahitaji upasuaji.

Upasuaji kuondoa mtoto wa jicho mara nyingi ni salama na uwezekano mkubwa wa kufanikiwa. Hatari kidogo zinazoweza kujitokeza ni pamoja na kupata maambukizi, kuvuja damu na athari kwenye retina.

Namna ya kujizuia usipatwe na mtoto wa jicho

Kupunguza hatari ya kuugua mtoto wa jicho

  • jikinge dhidi ya mionzi mikali kwa kuvaa miwani ya jua
  • fanya vipimo vya macho mara kwa mara
  • acha kuvuta sigara
  • kula zaidi matunda na mboga mboga kuondoa sumu mwilini
  • rekebisha uzito wako
  • punguza kula vyakula vya sukari na wanga ili kuondoa hatari ya kupata kisukari

Soma zaidi kuhusu: Presha ya macho

One reply on “Mtoto wa Jicho, Ushauri na Tiba”

MI BINAFSI NADHANI TUNA HAJA YA KUTAFTI TIBA MBADALA YA TATIZO HILI ILI KUWEZA KUPUNGUZA HATARI YA BAADAE KUWA NA WALEMAVU WA MACHO KWA KIWANGO CHA JUU.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *