Categories
Afya ya mwanamke na uzazi

Chanzo cha Maumivu ya Tumbo kwa Mjamzito

maumivu ya tumbo kwa mjamzito
mjamzito

Maumivu ya tumbo kwa mjamzito siyo jambo la kawaida hata kidogo.maumivu yanaweza kuwa ya haraka na kuisha ama yanaweza kuwa ya muda mrefu.

Ni muhimu kwa wewe mjamzito kujua kipi ni kawaida na kipi siyo cha kawaida wakati huu una mimba ili ujue muda gani umwone daktari kabla hujachelewa.

Maumivu ya Tumbo kwa Mjamzito kutokana na gesi nyingi

Gesi kwenye tumbo la chakula inaweza kuwa sababu ya tatizo lako. Maumivu yanaweza kuwa eneo moja ama yakasambaa kwenye kifua mpaka mgongoni. Tafiti zinasema kwamba wanawake wanapata gesi nyingi kwasababu ya kuongezeka kwa homoni ya progesterone kipindi hiki cha ujauzito.

Homoni hii inafanya misuli kulegea na hivo kupunguza kasi ya kutembea kwa chakula kwenye utumbo. Chakula kinachukua muda mrefu kuchakatwa na hivo kuzalisha gesi. Pia kadiri mimba inavokuwa kubwa inatengeneza mgandamizo kwenye utumbo na viungo vya karibu na hivo kuruhusu gesi kujikusaya.

Tiba Ya gesi Tumboni Kwa Mjamzito

Kama chanzo cha maumivu yako ya tumbo ni gesi nyingi tumboni, yatakiwa ubadili mtindo wa maisha. Jaribu kula kidogo kidogo katika siku. Usile milo mitatu mizito kama ambavo ulizoea mwanzo. Gawanya hata milo sita lakini midogo midogo.

Fanya mazoezi mepesi kama kutembea na yoga. Mazoezi yanachochea chakula kusagwa haraka na hivo kuzuia gesi kujikusanya. Punguza kula vyakula vilivyokaushwa kwa mafuta kama chips na vyakula kama mharage na kabeji ni chanzo cha gesi. Acha pia kunywa soda, jusi za viwandani na bia

Maumivu ya Maungio ya Nyonga hupeleka Maumivu ya Tumbo kwa Mjamzito

Eneo la nyonga linaweza kuuma kutokana na kutanuka ili kusapoti mtoto. Maumivu haya yanaweza kuwa ya haraka na kupita au yanaweza kuwa ya muda mrefu na kusambaa mpaka kwenye tumbo. Hali hii hutokea sana miezi minne ya mwisho kuelekea kujifungua.

Tiba ya Maumivu Ya nyonga

Kupunguza maumivu eneo la nyonga, jizoeshe kuamka taratibu ikiwa umetoka kulala ama ulikaa kwenye sofa/ kiti. Kama unajiskia kukohoa au kupiga chafya jikunye kidogo kwa magoti itasaidia kupunguza mgandamizo kwenye eneo la nyonga.

Fanya mazoezi ya yoga kila siku yatasaidia kunyoonya maungo ya mwili na kupunguza maumivu

Kukosa Choo Na Kupata Choo Kigumu(Constipation)

Hii ni adha mojawapo kubwa inawapata sana wajawazito wengi. Mabadiliko ya homoni, lishe, vidonge vya madini chuma na kukosa mazoezi ni chanzo cha mjamzito kukosa choo na kupelekea maumivu ya tumbo.

Tiba ya Constipation wakati wa ujauzito

Ongeza ulaji wa vyakula vya kambakamba kwenye lishe yako. Kunywa maji ya kutosha. Kula milo kidogo kidogo, usile mlo mkubwa kwa mara moja. Na usimeze vidonge vya kulanisha choo mpaka umeongea na daktari. Maana kumeza dawa ovyo yaweza kupelekea mimba kuharibika.

Sababu Zingine Za Maumivu ya Tumbo Kwa mjamzito

Maumivu ya tumbo inaweza kuwa ni ishara ya changamoto fulani kubwa ya kiafya kama

  • Mimba kuharibika
  • Mimba kutunga nje ya kizazi
  • Kukatika kwa kondo la nyuma
  • Kupanda kwa shiniko la damu kupita kiasi
  • Matatizo haya yote yanahitaji upate usaidizi wa hospitali haraka sana.

Matatizo mengine ya kiafya yanayoweza kupelekea uumwe tumbo, ambayo hayahusiani moja kwa moja na mimba ni pamoja na

Onana na Daktari mapema endapo maumivu yako ya tumbo yanaambatana na

  • Homa
  • Kutokwa na damu
  • Tumbo kubana na kuachia kama vile wajifungua
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Maumivu wakati wa kukojoa

Bofya kusoma makala inayofuata kuhusu:Hamu ya tendo la ndoa kwa mjamzito

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *