Kipimo cha utrasound: maelezo, matumizi na maandalizi

kipimo cha utrasound
kipimo cha utrasound

Kipimo cha utrasound ni kipimo cha kitabibu kinachotumia mawimbi ya sauti, kuchukua picha za ndani ya mwili wako. Kwa jina jila utrasound huitwa sonography.

Teknolojia inayotumia kwenye utrasound ni sawa na ile inayotumika kwenye radar kuongoza ndege, na majini kupima umbali wa kifaa ndani ya maji. Kipimo cha utrasound kinamuwezesha daktari kuchunguza viungo na tishu mbali mbali bila hata ya kufanya upasuaji.

Kipimo cha utrasound hakitumii mionzi kabisa ukilinganisha na vipimo vingine kama x ray na CT scan . Kwasababu hii, ndio maana kipimo kinfaa sana kwa mjamzito kujua maendeleo ya ukuaji wa mtoto tumboni.

Kwanini ufanyiwe kipimo cha utrasound?

Watu wengi hufikiria utrasound ni kwa ajili ya kucheki maendelo ya mimba tu kwa mjamzito. Japo kipimo hiki kina kazi zingine nyingi sana.

Daktari anaweza kupendekeza ufanyiwe utrasound endapo unapata maumivu eneo la mwili, uvimbe ama dalili zozote zingine mbaya zinazohitaji uchunguzi wa viungo vya ndani.

Utrasound inaweza kutoa picha kwa viungo hivi.

 • kibofu cha mkojo
 • ubongo kwa watoto
 • macho
 • mfuko wa nyongo (gallblader)
 • figo
 • ini

Viungo vingine ni pamoja na

 • mifumo wa mayai ya mwanamke
 • kongosho
 • bandama
 • tezi dume
 • kizazi korodani na
 • tezi ya thayroid

Utrasound pia hutumika kumsaidia daktari wakati wa upasuaji.

Jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya utrasound

Maandalizi kwa ajili ya kipimo yanategemea na aina ya utraound unayotakuwa kufanyiwa.

Daktari anaweza kukujulisha ufunge kula walau kwa masaa 12 kabla ya utrasound, hasa kama utapimwa eneo la tumbo. Chakula na uchafu wa tumbo unaweza kuzuia kupenya kwa mawimbi ya sauti na hivo kuingilia vipimo na ubora wa picha.

Kufunga kula kabla ya kipimo

Kwa vipimo vya mfumo wa nyongo, ini, kongosho au bandama, daktari anaweza kukwambia usile chakula cha mafuta usiku mmoja kabla ya kipimo. Japo utaruhusiwa kunywa maji na kuendelea kutumia dawa zingine ulizoelekezwa. Kwa vipimo vingine, unaweza kujulishwa kunywa maji mengi na kushikilia mkojo, ili kibofu kionekane vizuri.

Hakikisha unamwezeleza daktari endapo kuna dawa zozote unatumia kwa muda huo, dawa za famasi ama tiba asili kabla ya vipimo. Ni muhimu kufuatilia maelekezo ua daktari na kuuliza maswali ale ambapo hujaelewa kabla ya vipimo.

Namna kipimo cha utrasound kinavyofanyika

Kabla ya kipimo, utapewa nguo ya hospitali. Kisha utalazwa kwenye meza au kitanda tayari kwa kuanyiwa utrasound.

Mtaalamu wa utrasound (sonographer), atakupakaa jelly laini kwenye eneo la ngozi ambalo litapigwa amawimbi ya sauti. Jelly hii husaidia kupunguza msuguano kati ya kipimo na ngozi, jelly pia inasaidia kusafirisha mawimbi ya sauti.

Baada ya kupakwa mafuta, kifaa kidogo kitapitishwa eneo la juu la ngozi na mawimbi makubwa ya sauti yatasukubwa kuelekea ndani ya mwili. Kisha yale mawimbi yanapogonga mfupa yanarudisha mwangwi. Mwangwi huu unatumwa moja kwa moja kwenye computer na kuzalisha picha, ambapo daktari atazitafsiri picha hizo kujua tatizo lako.

Kulingana na tatizo lako, utahitaji kubadili mikao kama mpimaji atakavokwelekeza.

Baada ya vipimo

Baada ya vipimo, daktari atakufuta jelly yote kwenye ngozi. Upimaji unachukua angalau dakika 30, kwa kutegemea na eneo linalopimwa. Utaruusiwa kuondoka na kurudi nyumbani kuendelea na shughuli zako.

Utrasound ni kipimo nafuu na salama sana cha kuzalisha picha. Picha ambazo zitamuongoza daktari kugundua tatizo lako.

Unahitaji maoni ama ushauri? Tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254 utajibiwa, Usipige simu namba ni ya whatsapp tu.

Bofya hapa kusoma kuhusu kipimo cha X rays