Uke Mdogo na Kupungua Kina Cha uke

kina cha uke+Uke mdogo
kina cha uke


Mitaani kuna mijadala mingi saa kuhusu urefu sahihi wa uume,lakini wachache zaidi huongeleza kina cha uke na uke mdogo.

Kina cha kawaida cha uke ni inch 3 mpaka inch 6, sawa na urefu wa kiganja chako. Japo urefu wa uke unabadilika katika nyakati tofauti. Mfano unapokuwa kwenye hisia za mapenzi, kina cha uke wako kinaongezeka ili kuruhusu uume kuingia vizuri.

Kila mwanamke ana kina chake cha uke, kwahivo usijilinganishe na mwanamke mwenzako. Soma zaidi makala yetu kujua kiachosababisha uke mdogo

Madhara ya Kupungua Kina Cha Uke

Uke kuwa mfupi na hupelekea uume kukwama kupenya kwenye uke.
Kama unapata dalili za ugumu wa uume kupenya kwenye uke, maumivu au hali ya kuugua wakati uume unaingia ukeni, na kujihisi maumivu makali yanayobakia ukeni baada ya uuume kutolewa, tatizo lina weza kuwa moja kati ya sababu hizi

Nini Cha kufanya endapo uume umegoma kupenya kwenye uke mdogo

Kama uume haupiti ukeni kutokana na changamoto za kawaida unaweza kujaribu mambo haya

  1. Kufanya tendo taratibu: ongea na mwenzi wako kwenda taratibu wakato wa tendo ili kupunguza msuguano.
  2. Jipe muda zaidi wa kutomasana kuongeza hamasa ya tendo na pia kuruhusu uke ulowane majimaji vizuri.
  3. Tumia vilainishi: Vilainishi vya majimaji zitasaidia kupunguza msuguano na kuruhusu uume kupenya kwenye uke. Ongea na daktari kupata ushauri kuhusu vilainishi gani ni ni salama ukeni.
  4. Pumzika kidogo: Kama umepata maumivu, jipe muda wa dakika kadhaa kupumzika kwanza ili misuli yako ilegee.
  5. Jaribu staili ingine ya kufanya mapenzi: Fanya majaribio ya mikao tofauti ya kufanya ngono, kisha chagua mkao mmoja ambao ni sahihi na usioleta maumivu zaidi kwa upande wako.

Changamoto Zinazopelekea Uke Mdogo ni Pamoja na

Vaginismus

Vaginismus ni kitendo cha misuli ya uke kujifunga pale unapojaribu kuingiza kitu iwe kidonge au tampon. Changamoto hii hutibiwa hasa kwa mazoezi ya nyonga.
Daktari anaweza kupendekeza kutumia kifaa maalumu cha kupanua uke wako yaani vaigani dilator.

Kuinama Kizazi huepelekea uke mdogo

Kizazi ni kiungo kidogo sana kilichopo nyuma ya uke wako. Kizazi hukaa kwa kuangalia mbele ya tumbo la chakula. Kwa baadhi ya wanawake kizazi huinama na kutazamana na uti wa mgongo.

Kizazi kilichoinama ama kugeuka hupunguza kina cha uke, na kufanya kuingiza kitu chochote ukeni kuwa changamoto. Kwa changamoto hii daktari anaweza kupendekeza aina fulani ya staili wakati wa tendo ili uume uingie vizuri pasipo maumivu.

Bofya hapa kusoma mazoezi ya kunyoosha kizazi kilichoinama

Makovu kwenye uke

Makovu kwneye uke kutokana na changamoto na tiba mbalimbali yanaweza kupelekea kupungua kwa kina cha uke. Tiba ya mionzi kwenye njia ya uke na upasuaji vinasababisha maovu ukeni.

Tiba kwa changamoto hii ni kwa daktari kupendekeza mazoezi(pelvic exercise) pamoja na kutanua uke(vaginal dilator). Pia unaweza kupunguza maumivu kwa kutumia kilainishi .

Lini Umuone Daktari

Endapo maumivu haya ya uke wakati wakuingiza kitu ndani aidha uume au tampon, yamekuwa makubwa mpaka kukukwamisha shughuli zako, inabidi kumwona daktari.

Daktari atakufanyia vipimo na upembuzi kujua chanzo cha tatizo lako. baada ya kugundua chanzo ndipo daktari atapendekeza tiba sahihi ya kukupatia.

Kama umependezwa na huduma yetu na unahitaji kutuchangia chochote ili tuendelee kutoa zaidi elimu hii, Wasiliana nasi kupitia whatsapp namba 0678626254.

Bofya kusoma kuhusu: Chanzo cha ukavu ukeni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *