Kitanzi Kusogea na Kutoka Kwenye Kizazi

kitanzi kusogea
kitanzi

Ni jambo linalotokea mara chache sana kwa kitanzi kusogea, na usipate hofu yoyote. Tambua tu kwamba ikitokea kitanzi kimesogea, inatakiwa kiwekwe sawa tena ama kitolewe kabisa.

Kitanzi ni kitu gani?

Kitanzi kwa lugha ya kitaalamu intrauterine device(IUD) ni njia ya kisasa kupanga uzazi kwa muda mrefu. Ni kifaa kidogo chenye umbo la herufi T, ambacho huchomekwa kwenye kizazi kupitia njia ya uke. Vitanzi hutengenezwa plastic ama madini ya copper.

Aina za Kitanzi

Kuna aina mbili za vitanzi. Kitanzi cha copper na kitanzi cha homoni (hormonal IUD). Kitanzi cha homoni kinaweza kukukinga usishike mimba kwa miaka mitatu mpaka mitano. Wakati kitanzi cha copper kinaweza kukukinga usishike mimba mpaka miaka kumi au zaidi.

Faida ni nyingi sana za kutumia kitanzi. Makala hii itaeleza kwanini kitanzi kinaweza kusogea, na utajuaje kama kimesogea pamoja na nini cha kufanya kitanzi kinaposogea.

Nini kinaweza kupelekea kitanzi kusogea?

Japo ni mara chache lakini inaweza kutokea kitanzi kusogea, na inatokea sana miezi michache baada ya kuwekewa kitanzi. Kitanzi kinaweza kusogea na kutoka endapo

  • kuta za kizazi zinameguka sana wakati wa hedhi
  • una ukuta mdogo wa kizazi
  • kizazi chako kimeinama
  • umewekewa kitanzi na muhudumu asiye na uzoefu

Kitanzi pia chaweza kutoka ama kusogea kutoka mahala pake endapo

  • una umri chini ya miaka 20
  • unanyonyesha
  • umeweka kitanzi haraka baada tu ya kujifungua

Unawezaje kugundua kama kitanzi kimesogea?

Kitanzi kinakuwa na nyuzi mbili zinazoningia kwenye mlango wa kizazi, kwahivo yatakiwa muda mwingi uwe unavihisi hivo vikamba.

Kuhakikisha kwamba kitanzi hakishasogea, wataalamu wanashauri uwe unacheki kitanzi chako kila mwezi baada ya hedhi. Ni kwasababu uwezekano ni mkubwa sana wa kitanzi kusogea nyakati za hedhi.

Hatu za kuchunguza kuhakikisha kitanzi chako kipo mahala pake

  1. Osha mikono yako vizuri kwa maji na sabuni
  2. Chutama kama unakunya ili kuweza kuupata vizuri uke
  3. Ingiza kidole kwenye njia ya uke mpaka uguse kitanzi
  4. Hakikisha unazishika kamba zinazoninginia kwenye mlango wa kizazi
  5. Na hakikisha usivute kabisa hizo kamba.

Kama unaweza kushika kamba basi kitanzi kipo mahala pake. Kama hautashika kamba, ama ukahisi ni ndefu kuliko mwanzo, na ukashika plastic ya kitanzi, basi kuna uwezekano kitanzi chako kimesogea.

Viashiria na dalili za kitanzi chako kusogea au kutoka

Kama kitanzi chako kimesogea kidogo tu waweza usihisi chochote. Lakini kama kitanzi kimesogea pakubwa utapata viashiria na dalili hizi

  • kushindwa kushika kamba za kitanzi
  • kushika plastic ya kitanzi
  • mme wako kugusa kitanzi wakati wa tendo
  • kupata hedhi katikati ya mzunguko
  • hedhi nzito sana ya mabonge
  • maumivu makali ya tumbo kuliko yale ya hedhi
  • kupata uchafu ukeni usio wa kawaida

Nini ufanye endapo kitanzi chako kimesogea

Kama unahisi kitanzi chaki kimesogea mahala pake, kamwe usijaribu kukirudisha nyumbani. Badala yake nenda hospital onana na muhudumu ama daktari akuchunguze.

Daktari atafanya uchunguzi ili kujiridhisha kama kitanzi kimesogea na kisha atakupa maelekezo ya kufanya.

Kama una mpango wa kufanya tendo kabla hujamwona daktari, hakikisha unatumia njia ingine mbadala ya kuzuia mimba mfano condom. Kwanini? kwasababu unaweza kushika mimba kitanzi kikisogea mahala pake.

Nini kinaweza kutokea endapo kitanzi kikisogea na kutoka mahala pake?

Kama daktari hataweza kuzipata kamba za kitanzi, atakufanyia kipimo cha mimba haraka. Unajua kwanini? kwasababu inawezekana ulishika mimba, na kitanzi siyo salama kwa mimba. Kama hakuna mimba, daktari atakupa njia zingine za kukukinga usishike mimba kama vidonge.

Baada ya hapo daktari atakufanyia utrasound kuona kitanzi ndani ya kizazi. Kama kitanzi bado kipo ndani, basi nini wewe uchague kiachwe huko ama kitolewe. Hii sasa itategemea na

Unaweza kuamua kitanzi kitolewe kabisa

Dalili unazopata pengine una maumivu makali nk
unahitaji kuzaa ama kubadili njia ya uzazi wa mpango ama
kitanzi kipo mahala pabaya inabidi kitolowe kwa maelekezo ya daktari.

Kumbuka kama kitanzi kiliwekwa hivi karibuni, kinaweza kurudi mahala pake ndani ya miezi michache.

Kama daktari hatakipata kitanzi kwa utrasound, nasi attakufanyia x ray ya tumbo na nyonga. Kisha mtashauriana sasa nini kfanyike.

Je kitanzi ni njia sahihi kwangu?

Kuna aina nyingi za uzazi wa mpango, sindano, vidonge, kondom , kalenda nk. Kitanzi kina faida na hasara pia

Tuanze na faida za kitanzi

  • ufanisi wake ni zaidi ya asilimia 99
  • kinakaa mda mrefu mpaka miaka 10
  • muda wowote unaweza kutoa na kushika mimba
  • kitanzi cha homoni kinafanya hedhi iwe nyepesi sana na kukupunguzia maumivu
  • usiri (unaweza kumficha mpenzi wako kama una kitanzi ama umwambie ukiamua ajue)

hasara za kitanzi

  • inahitaji kuhudhuria clinic mara kwa mara ili kucheki kama hakijasogea
  • kuweka na kutoa inaweza kuleta maumivu makali
  • inaongeza hatari ya mimba kutunga nje ya kizazi (ectopic pregnancy)
  • kitanzi cha copper kinaweza kuleta hedhi nzito sana ya mabonge inayoambatana na maumivu makali
  • hatari ya kupata PID na fungus kuongezeka
  • inaweza kutengeneza makovu kwenye kizazi, japo hii ni mara chache sana.

Maelezo ya Mwisho kuhusu Kitanzi

Kitanzi ni njia salama na yenye ufanisi kupanga uzazi. Japo inatokea mara chache sana lakini tambua kitanzi kinaweza kusogea na kuhama mahali pake.

Kitanzi kuhama kinatokea sana week chache za kwanza baada ya kuanza kutumia. Na pia endapo unapata damu nzito sana na ukuta wa kizazi kubomoka kupita kiasi, hii inaongeza chansi ya kitanzi kusogea.

Kama unahisi kitanzi kimesogea, nenda hospitali umwone daktari haraka. Usijaribu kabisa kukirudisha kitanzi kwa mikono yako.

Bofya usome kuhusu: Maumivu na Aina za Tumbo la Chango