Categories
Afya ya Meno na Kinywa

Ulimi Kuchubuka

ulimi kuchubuka
ulimi

Ulimi wako ni umetengenezwa kwa msuli wa tofauti sana na kipeke sana na umejishika kwenye mfupa eneo moja tu la mwishoni. Ngozi yake imejaa testa za ladha.Mwisho wa makala hii utakuwa umejua chanzo cha ulimi kuchubuka na hatua 7 za kutibu tatizo.

Kazi kubwa za ulimi ukiwa ni

 • kusaidia utafunaji wa chakula na kukizungusha chakula kwenye mdomo
 • kuonja chunvu, tamu na kitu kichungu
 • kutamka maneno vizuri na sauti

Ulimi kuchubuka yaweza kusababishwa na vitu vifuatavyo

1.Majeraha kwenye ulimi

Endapo ngozi ya ulimi ilipata majeraha, kinga ya mwili inaanza kupambana ili kutoa zile seli ziliokufa. Kitendo hichi kinaweza kupelekea ulimi wao kuchubuka.

Kuna njia nyingi zaweza kupelekea ukapata mejeraha kwenye ulimi wako, njia hizi ni pamoja na

 • kunywa kitu cha moto sana mfano chai
 • kunywa au kula kitu chenye tundikali kwa wingi mfano vinegar, malimau nk
 • kula au kunywa vyakula vichachu mfano pilipili
 • kujin’gata ulimi nyakati za kuongea au kula, ama umepata ajali ya kujigongesha

2.Fungus ya ulimi-oral thrush

Fungus ya ulimi inasababishwa na vimelea wa candida. Dalili kubwa ya ulimi wako kuwa na fungus ni utando mweupe na pia kuchubuka ngozi

3.Vidonda vya mdomo-canker sores

Vidonda vya mdomo vinaleta maumvu sana kwenye ulimi. Na vidonda hivi tunaweza kuvigawanya katika makundi matatu

Minor. Hivi ni vidonda vidongo vya ukubwa wa ml 2 mpaka 8, na huwa vinapona vyenyewe.

Major: hivi ni vikubwa na vinafikia cm 1, vikipona vinaacha alama

Herpetiform: hivi bi vidonda vingi vinajikusanya pamoja na kufanya kidonda kikubwa.

4.Mabaka kwenye ulimi -geographic tongue

Mabaka haya yanaweza kuwa na rangi tofauti na ngozi ya kawaida ya ulimi. Mabaka haya mengi hayaumi na ni ya kawaida hata siyo saratani. Yanaweza kubabuka na kuisha yenyewe.

Lini unatakiwa kumwona Daktari

Unatakiwa kumwona daktari endapo unapata dalili mbaya zaidi, na vidonda vinazidi kukua kila siku bila kuonesha nafuu. Pia watakiwa kwenda hospitali haraka endapo unapata

 • homa kali
 • unashindwa kunywa maji vizuri au kula
 • ulimi unapata vidonda mara kwa mara
 • maumivu ya ulimi yasiyoisha hata kwa dawa za kununua dukani
 • unanuka mdomo kupita kiasi
 • ulimi unavimba na unashindwa kupumua vizuri

Huduma ya kwanza kwa tatizo la ulimi kuchubuka

 1. Usitumie vyakula na vinywaj vya moto sana
 2. Uache kunywa pombe na kuvuta sigara
 3. Safisha meno yako mara kwa mara na hakikisha kinywa chako ni kisafi
 4. Epuka kula vyakula vilivyokaangwa kwenye mafuta, vichachu na vyenye tindikali kwa wingi
 5. Nunua supliment ya vitamin C na B-complex pharmacy utumie
 6. Weka maji ya vuguvugu na chunvi kiasi, kisha yazungushe mdomoni na uteme
 7. Weka kipande cha barafu kwenye kwenye kidonda kupunguza maumivu.

Bofya kusoma kuhusu: Fungus mdomoni

Categories
Afya ya mwanamke na uzazi

Kubeba Mimba Katika Umri Mkubwa

mimba katika umri mkubwa
mimba uzeeni

Ni umri gani tunasema umeshika mimba uzeeni?

Kuanzia miaka 35 tunasema ni umri mkubwa zaidi wa kushika mimba (advanced martenal age)

Kutokana na sababu mbalimbali, wanawake wanaweza kuamua kuchelewa sana kutafuta mtoto. Hii imekuwa tabia maarufu sana katika miaka ya hivi karibuni. Mabadiliko ya teknologia yamechangia sana. Mfano mtu anaweza kuamua kutunza mayai na mbegu kisha zikatumika hata baada ya miaka mi5 kushika mimba.

Pamoja na teknologia kukua, bado hatari ya kubeba mimba katika umri mkubwa ipo. Changamoto kama mimba kuharibika, kifafa cha mimba, kujifungua kwa upasuaji nk

Kwanini ni hatari kubeba mimba katika umri mkubwa?

Kadiri umri unavosogea, uwezekano wa kuugua magonjwa sugu unaongezeka. Magonjwa kama kisukari, presha ya kupanda na magonjwa ya tezi ya shingo. Hata kama afya yako iko njema kabla ya mimba, unapopata mimba italeta mabadliko ya kukuweka kwenye changamoto.

Wanawake wanaobeba mimba katika umri zaidi ya 35 wapo kwenye hatari ya

 • mimba kutunga nje ya kizazi
 • mimba kutoka mapema
 • kuchelewa kujifungua
 • matatizo ya kondo la nyuma
 • kisukari cha mimba
 • presha ya kupanda
 • kifafa cha mimba
 • kujifungua mapema kabla ya wakati
 • kupungukiwa damu
 • magonjwa ya moyo
 • kuziba mishipa ya damu
 • kuvuja damu nyingi baada ya kuzaa

Changamoto kwa mtoto

Kuna ongezekeno la hatari ya mamatizo ya hitilafu za vinasaba, pale mayai yanapozeeka. Mwanaume yeye anazalisha mbegu mpya kila siku, ila kwa mwanamke ni tofauti.

Mwanamke anazaliwa na mayai yote, hakuna mayai mapya yanayozalishwa tena, ila tu yanapevuka kila mwezi. Mayai haya yanavokaa miaka mingi yanazeeka na kuwa na hitilafu za kivinasaba.

Kwa mtu mzima, mzunguko wa damu kwenye via vya uzazi na kuelekea kwenye kondo la nyuma unapungua, na hivo kupelekea ukuaji hafifu wa mtoto tumboni.

Pia hatari ya kuumwa kwa mjamzito katika umri mkubwa inaongeeka, na kuathiri ukuaji wa mtoto, kupungua majimaji ya mtoto, na kujifungua njiti.

Maandalizi ya kubeba mimba katika umri mkubwa

Wataalamu wa uzazi wanashauri kuweka sawa uzito wako, kufanya mazoezi, kula vizuri na kupunguza stress ni muhimu pale unapotaka kubeba mimba katika miaka 35+

Muone daktari akufanyie vipimo hasa kwa magonjwa ya kisukari, tezi ya shingoni, na presha ya kupanda. Ni muhimu sana kupima magonjwa haya kabla hujashika mimba kwasababu yanaweza kuwepo bila dalili yoyote. Hakikisha unamweleza daktari anayekupima kwamba unajaribu kubeba mimba.

Je mama mtu mzima atapata changamoto gani kwenye kujifungua?

Mjamzito anapokaribia kujifungua, kondo la nyuma huanza kulegea. Hii inamaanisha mishipa ya damu inaanza kuzeeka, na usafirishaji wa chakula na hewa kuelekea kwenye mtoto unapungua. Lengo ni kumuandaa mtoto kuanza kujitegemea kula akitoka nje ya tumbo.

Kitendo hichi kinatokea mapema sana kwa wajawazito wa umri mkubwa. Yaani usafirishaji unapungua mapema kabla ya muda muafaka wa kujifungua. Ndiomaana katika umri huu, mimba ikifika tu wiki 39 na hujapata uchungu, unazalishwa kwa lazima ili kumuokoa mtoto.

Watu wazima wako kwenye uwezekano mkubwa wa kujifungua kwa upasuaji kwasababu wanakosa nguvu ya kusukuma mtoto. Na watoto wanaozaliwa na wazazi wazee, wanaweza kuwa mapigo ya moyo ya tofauti na hivo kujifungua kwa njia ya uke ikawa hatari kwao.

Bofya kusoma kuhusu: Kujifungua kwa upasuaji, ushauri na hatua za kuzingatia

Categories
Afya ya mwanamke na uzazi Hedhi salama

Hedhi Mara Mbili Katika Mwezi

hedhi mara mbili katika mwezi
kalenda ya hedhi

Mzunguko wa hedhi

Hedhi ya kawaida inachukua mzunguko wa siku siku 21 maka 35. Nikisema mzunguko namaanisha jumla ya siku kuanzia ulipopata hedhi mwezi mmoja, mpaka utakapopata hedhi tena katika mwezi unaofata. Makala hii itaongelea tatizo la kupata hedhi mara mbili katika mwezi na nini cha kufanya.

Japo siyo kawaida kupata mizunguko tofauti kila mwezi. Baadhi ya mizunguko yaweza kuwa mifupi au mirefu kuliko mingine, na hivo kupelekea upate hedhi mara mbili katika mwezi.

Tazama na dalili zingine

Katika nyakati nyingi kupata hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja yaweza isiwe tatizo. Lakini kama inatokea kwa kujirudia ni muhimu kutazama na dalili zingine zinazoambatana. Endelea kusoma zaidi ili kujifunza kuhusu changamoto ya hedhi mara mbili katika mwezi

Hedhi mara mbili katika mwezi kwa mara ya kwanza

Watu wenye mzunguko mfupi mara nyingi sana wanapata hedhi mwanzoni na mwishoni mwa mwezi. Kwa mtu mwenye mzunguko wa kawaida wa siku 28 au zaidi, akipata hedhi mara mbili lazima ashituke.

Kumbuka hedhi isipotoka kwa wakati inaashiria changamoto ya kiafya. Ni ni rahisi sana kuchanganya hedhi na bleed ingine. Waweza kudhani ni hedhi kumbe unatokwa na damu tu kutokana na changamoto fulani.

Changamoto zinazoweza kupelekea bleed isiyo ya hedhi ni pamoja na

Mimba- mimba inapojishikiza kwenye ukuta wa kizazi yaweza kupelekea bleed.Ugonjwa wa zinaa: magonjwa ya ngono yanaweza kupelekea upate bleed kidogo na kutokwa na uchafu usio wa kawaida ukeni.

Mimba kuharibika-Mimba inapoharbika inaambatana na maumivu makali na kutokwa na mabonge ya damu. Ni muhimu kwenda hospitali mapema ikiwa una mimba na umeanza kuona damu.

Mabadiliko ya uzito– Mazoezi kupita kiasi na mabadiliko makubwa ya uzito wa mwili yanaweza kupelekea hedhi mara mbili.

Uzazi wa mpango wa kisasa-Hedhi kuvurugika na kutoka mara mbili inatokea sana kwa wanaotumia njia za kisasa kuzuia mimba , mfano sindano, njiti na vidonge

Vimbe kwenye mlango wa kizazi na ukuta wa kizazi: Hizi ni vimbe ambazo siyo saratani kwenye kuta za mlango wa kizazi na kwenye ukuta wa kizazi, ambazo zaweza kupelekea upate hedhi zaidi ya mara moja.

Saratani ya mlango wa kizazi: kutokwa damu yaweza kuashiria uwepo wa saratani

Tofauti kati ya damu ya hedhi na bleed ya tatizo la via vya uzazi

Hizi dondoo zitakusaidia kujua kama damu unayopata ni hedhi ama siyo hedhi

Kama ni hedhi ya kawaida itakulazimu kubadili pedi au tampon kila baada ya masaa kadhaa. Na damu kawaida inakuwa nyekundu nzito au ya kungaa, brown au pink

Kama ni matone ya damu ambayo siyo hedhi, haitahitaji kubadili pedi au tamponi mara kwa mara, unaweza kutumia pedi moja tu kwa siku. Damu yake yaweza kuwa ya pick, brown na inakata mapema ndani ya siku moja au mbili

Chanzo kikubwa cha mzunguko mfupi na hedhi mara mbili katika mwezi

Nini kinapelekea hedhi mara mbili katika mwezi? inaweza kutokana na mzunguko mfupi ama changamoto ya kiafya inayopelekea bleed ukeni.

Baadhi ya mambo yanayopelekea hedhi mara mbili ni pamoja na

1.Kukaribia kukoma hedhi-Perimenopause

Perimenopause ni kipindi ambacho mwanamke anakarbia kukoma hedhi yake, wakati ambapo kunatokea mabadiliko makubwa ya homoni. Kipindi hichi waweza kupata hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja. Perimenopasue inatofautiana kwa kila mwanamke.

Kuna wengine inachukua hata miaka 10 ndipo hedhi inakoma. Wakati wa kipindi hiki kuelekea kukoma, waweza kupata hedhi nzito sana, kuvusha miezi kadhaa bila hedhi, mzunguko kuwa mrefu , hedhi nyepesi sana. Menopause ndio kukoma hedhi kwenyewe. Mwanamke anakoma hedhi endapo atakosa hedhi kwa miezi 12 mfululizo.

2.Fibroids

Hizi ni vimbe zinazotokea kwenye kizazi. Ni vimbe zisizo saratani, na zaweza kuleta hedhi nzito, au ukavusha kabisa hedhi. Dalili zingine za fibroids ni pamoja na

 • kupata mkojo mara kwa mara
 • kuhisi uzito eneo la nyonga
 • maumivu chini ya mgongo
 • maumivu wakati wa tendo

Daktari atagundua kama una fibroids kwa kukufanyia kipimo cha utrasound.

3.Magonjwa ya tezi ya shingoni

Tezi huu huitwa thyroid, inakaa shingoni na ina umbo kama la kipepeo. Kazi ya tezi hii ni kuzalisha homoni ambazo zinaratibu mpangilio wa hedhi yako. Dalili za kwamba kuna tatizo kwenye tezi ya shingo ni pamoja na

 • kuhisi baridi mda wote
 • kuongezeka uzito
 • tumbo kujaa
 • kupungua mapigo ya moyo
 • kutoka na damu nyingi ya hedhi

Kwa upande mwingine ikiwa tezi yako inafanya kazi kupita kiasi utaanza kupata dalili hizi

 • kuhisi joto mda wote
 • macho kuvimba
 • moyo kwenda mbio sana
 • kukosa usingizi
 • kuharisha na
 • macho kuvimba

Hakikisha unaenda hospital, endapo utaanza kupata dalili hizi za tezi ya shingo.

Madhara zaidi ya kupata hedhi mara mbili

Watu wanaotoka kwenye familia zenye historia ya kuugua vimbe kwenye kizazi na kukoma hedhi mapema , wapo kwenye hatari zaidi ya kupata hili tatizo la hedhi mara mbili katika mwezi. Moja ya changamoto utakayopata kutokana na kupata hedhi mara mbili ni kupungukiwa damu. Dalili hizi zinaonesha kwamba umepungukiwa na damu.

 • mwili kuchoka sana
 • kizunguzungu
 • mapigo ya moyo kubadilika
 • kukosa pumzi
 • kuumwa sana kichwa

Je kuna umuhimu wa dawa kutibu hedhi mara mbili?

Hedhi mara mbili siyo tatizo ikiwa mzunguko wako ni mfupi. Japo ni muhimu sana kumuona daktari endapo kama utapata dalili hizi hapa chini

 • hedhi mara mbili kwa miezi mi2 au mi3 mfululizo
 • maumivu wakati wa tendo
 • hedhi nzito ya mabonge
 • damu ya kuganda
 • maumivu chini ya kitovu hasa kama maumivu hayaishi
 • maumivu makali kwenye hedhi
 • kupata matone ya damu katikati ya mzunguko ambayo yanajirudia mwezi unaofata

Kwa binti mdogo hakuna tatizo

Matibabu ya tatizo hili ya kupata hedhi mara mbili katika mwezi mmoja, yanategemea na chanzo cha tatizo. Watu wenye mzunguko mfupi au wanaopata hili tatizo kwenye miaka ya mwanzo ya kubalehe, hawahitaji tiba tatizo laweza kuisha lenyewe.

Tiba inalenga Chanzo cha Tatizo

Daktari anaweza kupendekeza akupe dawa za kurekebisha homoni zile za kupanga uzazi. Kama tayari unatumia dawa za kisasa za uzazi wa mpango, na unahisi ndio chanzo cha tatizo, mjulishe daktari ili akubadilishie njia ingine.

Kwa tatizo la tezi ya shingo: daktari anaweza kupendekeza vipimo zaidi na kukupa dawa kwa tatizo hili

Kama unakarbia kukoma hedhi: kuna dawa za hormone utapewa kupunguza ukali wa tatizo

Kwa vimbe yani fibroids: daktari anaweza kukupa dawa, ama akapendekeza upasuaji, kulingana na ukubwa wa tatizo.

Kubadili mtindo wako wa maisha pia utasaidia kurekebisha homoni zako, mfano kama una uzito mkubwa na kitambi, anza kufanya mazoezi na kupunguza vyakula vya sukari.

Bofya kusoma: Njia salama za kupunguza maumivu kipindi cha hedhi

Categories
Magonjwa ya Kuambukiza

Tetekuwanga

tetekuwanga
tetekuwanga

Nini maana ya Tetekuwanga?

Tetekuwanga ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza. Ugonjwa unasababishwa na kirusi anayeitwa varicella-zoster. Watu wengi wanaugua tetekuwanga wakiwa wadogo, endapo hawakupata chanjo.

Mtoto anayeugua tetekuwanga anaweza kumwambukiza mtoto mwingine kwa urahisi sana. Kwa sasa tatizo siyo kubwa ukilinganisha na zamani kwani watoto sasa wanaweza kuachanjwa ili wasipate tetekuwanga.

Huwezi kuugua tetekuwanga mara mbili

Ukishaugua tetekuwanga huwezi tena kuugua maisha yako yote hata kama ukigusana na mgonjwa. Kama hujachanja unaweza kuugua tetekuwanga katika umri wowote ule.

Watu wazima wanaougua tetekuwanga wanakua wadhaifu sana na ugonjwa ukawapelekesha mno ukilinganisha na watoto. Ni bora kuugua tetekuwanga ukiwa mtoto kuliko kuugua ukubwani, au upate chanjo kabisa ili uisugue.

Tetekuwanga inaambukizwaje?

Unaweza kupata tetekuwanga kwa

 • kugusana na mgonwa mwenye tatizo
 • kuvuta hewa ya mgonjwa watetekuwanga au majimaji ya kooni na mafua
 • kugusa majimaji ya mgonjwa kwenye pua zako, mdomo na macho

Je kuna uhusiano gani kati ya tetekuwanga na mkanda wa jeshi?

Ukishaugua tetekuwanga, wale virusi wanabaki mwilini lakini hawasababishi tena tetekuwanga. Lakini siku virusi hawa wakiibuka wataleta ugonjwa mwingine unaoitwa mkanda wa jeshi ama shingles. Kwahivo mkanda wa jeshi hauambukizwi bali ni virusi wako wa tetekuwanga ulougua zamani ndo wanakuletea ugonjwa mpya.

Kumbuka watu wenye mkanda wa jeshi hawawezi kumuambukiza mtu mkdanda wa jeshi, basi wanaweza kumpa tetekuwanga, endapo huyo mtu hakuwahi kuugua tetekuwanga. Mkanda wa jeshi nao huisha wenyewe ndani ya week .

Dalili za tetekuwanga

Dalili za tetekuwanga hazijifichagi, ni rahisi sana kumtambua mgonjwa wa tetekuwanga. Dalili hizi ni kama

 • Homa
 • Kuhisi uchovu
 • kichwa kuuma
 • Maumivu ya tumbo
 • Malengelenge kwenye ngozi yanayowasha na kutoa maji
 • Makovu baada ya lengelenge kutoboka
 • Ngozi yenye madoadoa

Vipimo kugundua uwepo wa tetekuwanga

Kwa kutumia tu macho, muhudumu wa afya anaweza kugundua kwamba unaumwa tetekuwanga.

matibabu na huduma kwa mgonjwa wa tetekuwanga

Nawezaje kumsaidia mwanangu anayeumwa tetekuwanga?
Hakikisha mtoto anapata mda mwingi wa kupumzika na kunywa maji ya kutosha. tetekuwanga huwa inapona yenyewe ndani ya week 1 au mbili. Kumsaidia mtoto na muwasho unaweza kufanya haya

 • weka nguo yenye majimaji baridi kwenye lengelenge
 • hakikisha mwanao yupo eneo lenye ubaridi
 • ongea na mwanao asitoboea lengelenge kama mtoto mdogo sana mkate kucha ili ajijikune
 • unaweza kumpaka lotion maalumu au ukampa dawa zenye kiamabata cha antihistimine- nunua pharmacy
 • mwogeshe mwanao kwa maji baridi mara kwa mara. Mfute mtoto kwa taulo kama unakanda mwili, usifute kwa kusugua.

Usimpe mtoto dawa za asprin. Hizi zinaweza kumletea mtoto shida hasa mwenye homa. Kama huna uhakika dawa ipi ya kumpa mwanao, nenda pharmacy jieleze utapewa dawa sahihi.

Je kuna madhara zaidi yanaweza kutokea kwa mtoto mwenye tetekuwanga?

Changamoto kubwa zinazoweza kujitokeza kutokana na tetekuwanga ni pamoja na

 • bakteria kushambulia ngozi, damu na tishu laini
 • Nimonia- yani mapafu kujaa maji
 • mwili kupungukiwa maji kupita kiasi
 • ini kuathirika
 • damu kuganda

Nani anaweza kuugua zaidi na kulemewa na tetekuwanga?

Watu wenye afya njema, wanapougua tetekuwanga, huwa haiwapelekeshi sana. Japo wa watoto wadogo sana kuugua tetekuwanga inaweza kuwaletea shida zaidi, pia wenye mimba, wenye kinga dhaifu . Wagonjwa wa Ukimwi, saratani na wanapata tiba ya mionzi wanalemewa sana na tetekuwanga

Je tetekuwanga yaweza kuua mtu?

Ni mara chache sana tetekuwanga ikahatarisha maisha ya mtu. Watu wengi hupona mapema ndani ya wiki mbili baada ya kuugua. Japo wapo watu waliowahi kufa kwasababu ya tetekuwanga.

Je mwanangu anaweza kupata chanjo ya tetekuwanga?

Jibu ni ndio kuna chanjo ya tetekuwanga, ongea na mtoa huduma hospital atakupa maelekezo.

Je watu wazima wanaweza kuugua tetekuwanga?

Mtoto akishaugua tetekuwanga, mwili wake unapambana na virusi hao na kutengeneza kinga ya kudumu. Kinga hii inakaa mwilini miaka yote ya uhai wako, na itapambana na virusi wageni wataakaoingia siku zijazo.

Ni lini unatakiwa kumwona daktari?

Nenda hospital haraka endapo mtoto wako anapata dalili za

 • ana malengelenge kwe nye macho
 • kuumwa sana kichwa
  • ana malengelenge makubwa yanayotoa usaha
  • anashindwa kupumua vizuri

  Bofya kusoma kuhusu: kwanini unaugua kaswende sugu

  Categories
  Afya ya mwanamke na uzazi

  Dalili Mbaya Kwa Mjamzito

  dalili mbaya kwa mjamzito
  mjamzito

  Kipindi cha ujauzito kinaambatana na mabadiliko mengi sana ya mwili, pamoja na mabadiliko ya kimaisha pia kwenye kujiandaa kumpokea mwanafamilia mpya. Ni kipindi pia ambacho waweza kuwa na hofu sana kuhusu mimba yako, na utakuwa mwangalifu sana. Hapa chini ni maelezo a kina juu ya dalili mbaya kwa mjamzito na hatua za kuchukua mapema.

  Mabadiliko mengi ambayo utayaona mwilini mwako, jua kwamba ni kawaida na ni lazima uyapitie. Dalili nyingi mfano kuumwa nyonga, tumbo kuunguruma, kukosa choo, kizunguzungu nk zinakuja na kupotea.

  Je dalili mbaya zinaisha mapema?

  Baadhi ya dalili waweza kukaa nazo mpaka siku unajifungua, na kuna zingine zinakuja na kupotea. Hapo ndipo yatakiwa kuwa makini kwa kila dalili unazopata. Kuna dalili zingine hatari ambazo haitakiwi upitishe hata siku 1 bila kwenda hospital, endapo utaziona.

  Dalili za Kawaida Ambazo siyo hatarishi

  Dalili nyingi kati ya hizi siyo hatari, na haitakiwi kupata hofu sana. Japo unaruhusiwa kumpigia daktari wako na kumuuliza ili upate uhakika zaidi. Dalili nyingi ya hizi zinajitokeza mimba ikiwa changa, na zingine baadae

  • kutapika
  • kutokwa na uchafu mwingi ukeni
  • kichwa kuuma
  • uchofu na kizunguzungu
  • maumivu yanayokuja kwa haraka na kupotea
  • kupungua uzito
  • kuhisi joto kali
  • kushindwa kuvuta hewa vizuri
  • mawazo, na kupata hofu ana kushindwa kufanya kazi zako vizuri

  Dalili mbaya kwa mjamzito.

  Dalili hizi zinatokea mda wowote wa ujauzito. Japo mimba inapokuwa changa zaidi ndipo hatari ya mimba kuharibika inakuwa kubwa, ila watakiwa kuwa makini kipindi chote.

  Dalili hatarishi ni pamoja na

  1.Kuvuja damu

  Kitendo cha kutokwa damu/bleed ukiwa na mimba siyo ishara nzuri hata kidogo, ni kiashiria kwamba kuna tatizo. ikiwa unatokwa damu nzito, na una maumivu makali ya tumbo upande wa kushoto au kulia na unajihisi kuishiwa nguvu, hii inaweza kuashiria mimba imetunga nje ya kizazi.

  Mimba ikitunga nje ya kiazi haiwezi kukua, inatakiwa kuondolewa ma[pema kwa upasuaji. Mimba hiozi huitwa ecopic, endapo haitaondolewa mapema, mgonjwa anaweza kupoteza maisha.

  Kama damu zinatoka nzito, tumbo linauma kuzunguka kitovu, hii inaashiria mimba imeharbika, na hii inatokea zaidi mimba ikiwa chini ya wiki 12. Sisemi kwamba mimba kubwa kubwa haziharbiki, hapana. Ni kwamba mimba nyingi zinaharbika zikiwa changa.

  2.Kutapika na kichefuchefu kupita kiasi

  Kwa mjamzito ni kawaida kupata kichefuchefu, lakini kama tatizo ni kubwa inaweza kuashiria shida kubwa ya kiafya. Kama unashindwa mpaka kula au kunywa chochote, hapo utaishiwa maji. Na kuishiwa maji inaweza kuhatarisha ujauzito wako.

  Kama unahisi kizunguzungu kinakutesa sana, ongea na daktari atakupa dawa ya kupunguza makali yake.

  3.Mtoto kuacha kucheza

  Mtoto kupunguza kucheza inaweza kuashiria kachoka, hii ni kawaida isikupe hofu. ila kama hachezi kabisa kwa siku nzima, hapo kuna shida kubwa.

  Sasa ili kugundua tatizo, inashauriwa ukiona mtoto hachezi mda mefu, jaribu unywe kitu cha baridi. Kisha lala kwa ubavu, na fatilia kama mtoto ataanza kucheza.

  Mpigie daktari, ama nenda hospital haraka endapo utagundua mtoto ameacha kucheza. Daktari atafanya vipimo kuona kama kuna hatari yoyote.

  4.Kupata uchungu mapema mimba ya miezi 7

  Kupata uchungu na mimba haijatimiza umri wa kujifungua, ni dalili mbaya. Kama tumbo linavuta na kuachia na hii hali itokee mara chache na kuisha hilo ni kawaida. Kwani hata ukifika kileleni baada ya tendo, lazima utahisi tumbo kuvuta.

  Lakini endapo tumbo linavuta na kuachia, kisha baada ya dakika 10 linaanza tena kuvuta na kuachia, hiyo ni ishara ya kuelekea kuzaa njiti. Mpigie daktari mapema endapo utaona hali hii.

  5.Chupa kupasuka mapema ni dalili mbaya kwa mjamzito

  Tunaposema chupa, tunamaanisha ule mfuko unaobeba mtoto. Mfuko huu unakuwa na maji yanayomlinda mtoto asiumie. Mfuko unapasuka pale mama akianza uchungu na yupo tayari kujifungua. Endapo mfuko utapasuka mapema na mtoto akaendelea kubaki tumboni, mtoto atakosa hewa na kupoteza uhai.

  Maji haya ni tofauti na mkojo, kwani hayaishi mapema yakianza kuvuja. Kwahivo tazama ukiona dalili ya kuvuja maji ukeni, tena maji mengi, nenda hospitali haraka.

  6.Maumivu makali yasiyoisha kwenye kichwa, tumbo na kushindwa kuona vizuri

  Hizi dalili zinaweza kuashiri kupanda kwa presha kitaalamu (preeclampsia) . Hili ni tatizo baya na linaweza kupelekea kifafa cha mimba. Tatizo linaambatana na dalili za presha kupanda na protini nyingi kwenye mkojo, hasa inatokea baada ya week 20 za ujauzito. Hakikisha unaenda hospital haraka endapo unahisi dalili hizo.

  Nawezaje kujizuia nisipate dalili mbaya kwa ujauzito wangu?

  Ukweli ni kwamba ni vigumu sana kujizuia asilimia zote kupata dalili mbaya kwenye ujauzito. Lakini kuna vitu vichache unaweza kufanya kupunguza hatari ya mimba kuharibika kabla ya muda wake.

  Hudhuria clinic zote na upate dawa za kuongeza damu mapema kabisa. Unapoenda clinic daktari atachukua historia yako na kukwambia endapo upo kwenye kundi hatarishi. Utapewa ushauri wa kina kuhusu lishe na afya ya akili pamoja na afya ya tendo la ndoa.

  Bofya kusoma kuhusu kifafa cha mimba