Mashavu Ya Uke Kusinyaa-Vaginal Atrophy

mashavu ya uke kusinyaa
mwanamke

Nini maana ya mashavu ya uke kusinyaa?

Mashavu ya uke kusinyaa, kitaalamu vaginal atrophy au atropic vaginitis, ni kitendo cha kuta za nje za uke kupunguza unene wake na kukauka. Matokeo yake ni muwasho, kuungua na maumivu makali wakati wa tendo la ndoa. Kusinyaa kwa uke pia kunaongeza hatari ya kupata UTI mara kwa mara na kukojoa mara kwa mara.

Tatizo la uke kusinyaa kikawaida linatokea wakati wa kukoma hedhi yani menopause. Kipindi hichi kunakuwa na upungufu mkubwa wa homoni ya estrogen. Pia tatizo laweza kujitokeza katika umri mdogo, pale tu kiwango cha estrogen kinapopungua.

Nini Maana Ya Homoni?

Homoni mana na yake ni vichocheo ndani ya mwili, kazi yake ni kusaidia shuguli za mwili zifanyike. Wanawake wanahitaji kichocheo cha estrogen ili kuzalisha ute ukeni na kuchochea mayai kupevuka. Baada ya kukoma hedhi, mifuko ya mayai inapunguza kasi ya kuzalisha homoni na hivo kupelekea uke mkavu.

Je kuna Uhusiano gani kati ya uke mkavu na fungus ukeni?

Hivi vyote viwili vinaleta dalili ya ukavu ukeni, muwasho na maumivu kwenye tendo. Japo ukavu ukeni unasababishwa na kupungua kwa estrogen, fungus inatokana na kukua kupita kiasi kwa vimelea wa fungus ukeni. Ikiwa unashindwa kutofautisha dalili, tafadhali nenda hospital uonane na daktari akuchunguze.

Nani yupo kwenye hatari zaidi ya mashavu ya uke kusinyaa

Wanawake wenye umri zaidi ya 50 na waliokoma hedhi, wapo kwenye hatari zaidi ya kupata changamoto hii. Vitu vingine vinachochea tatizo ni Pamoja na

Athari zipi nitapata baada ya mashavu ya uke kusinyaa

Waweza kupata changamoto hizi

 • damu kutoka
 • kushindwa kufurahia tendo la ndoa
 • maumivu kwenye kukojoa
 • damu kwenye mkojo kutokana na majeraha pamoja na maambukizi
 • kuhisi uke kuwaka moto
 • maumivu makali kwenye tendo
 • kuugua mara kwa mara UTI
 • kuhisi mkojo mara kwa mara

Vipimo kwa tatizo la uke kusinyaa

Daktari atakusikiliza dalili unazopata na pia kukufanyia vipimo kwenye via vya uzazi. Vipimo pia vyaweza kuonesha kama umefikia kipindi cha kukoma hedhi yani menopause.

Kwenye vipimo vya kucheki kizazi, daktari ataangalia sifa hizi:-

 • uke kupungua ukubwa na kina
 • kuvimba na kukauka kwa mashavu ya uke
 • kupungua kwa mavuzi
 • kuvimba eneo la nyuma la uke
 • kibovu kilicholalia uke na
 • kuvimba kwa mirija ya mkojo

Aina za vipimo kwa tatizo la mashavu ya uke kusinyaa

Kama umekutana na daktari mzoefu yeye ni rahisi zaidi kugundua uwepo wa tatizo lako. Vipimo vya maabara vitafanyika tu ili kutofautisha na changamotto zingine kama fangas ukeni. Vipimo hivi ni pamoja na

 • pap test-kipimo cha shingo ya kizazi kuona uwepo wa saratani
 • kipimo cha mkojo
 • vaginal PH-kucheki kiwango cha tindikali ya uke
 • damu kucheki homoni na
 • hadubini-microscopy

Maswali atakayokuuliza daktari hospital

 • je umeshakoma hedhi?
 • dawa gani unatumia kwa sasa?
 • je umejifungua mtoto hivi karibuni?
 • je umeona damu ?
 • unapata uchafu wowote usio wa kawaida?
 • ulishajaribu kutumia vilainishi vya pharmacy?
 • je unapata maumivu kwenye tendo?
 • hizi dalili zimekusumbua kwa muda gani?

Tiba ya kusinyaa mashavu ya uke

Kulingana na chanzo cha tatizo, daktari atapendekeza kwako tiba sahihi. Tiba ya homoni ya estrogen ndio inaonekana kufanya kazi vizuri zaidi.

Baadhi ya tiba huwa zinalenga kutibu dalili za ukavu ukeni,. Na tiba zingine zinalenga kupungua kwa estrogen. Tiba hizi ni pamoja na

Vilainishi ili kuongeza unyevu kwenye uke. Vilainishi havitakutibu tatizo bali vinapunguza tu zile dalili mbaya, ili ufurahie tendo. Unaweza uvitapata pharmacy ya karibu yako.

Dilator-hivi ni vifaa vya kutanua uke ambao umeanza kusinyaa na njia yake kuwa ndogo. Lengo la kutanua ni kusaidia uume uweze kupita wakati wa tendo. na daktari atakubadilishia ukubwa wa dilator kulingana na maendeleo yako mpaka uume uweze kupita.

Hormone therapy-Hii ni tiba ya kurekebisha vichocheo ili kufanya uke wako kuwa mlaini tena na mashavu kunona. Huduma hii inapatikana pia ofsini kwetu.

Je naweza kujizuia nisipate tatizo la uke kusinyaa?

Mwili wa mwanamke unazalisha homoni ya estrogen kulingana na umri. Hiki hakiwezi kuzuilika, ni kama kujizuia kuzeeka.

Pamoja na hilo kuna njia kadhaa unaweza kufanya ili kupunguza makali ya tatizo. Jizuie kuvaa nguo za ndani kama chupi zilizobana sana, pant liner na vitu vyote vinayoleta muwasho ukeni kama

 • perfume
 • powders
 • deodorants
 • vilainishi na
 • dawa za kuua mbegu ili usishike mimba

Bofya usome makala inayofuata kuhusu: Nini cha kufanya ukishakoma hedhi, ushauri, mazoezi na tiba kwa uke mkavu