Je unajisi kwamba una dalili za mimba changa na huna uhakika? Njia pekee ya uhakika ni kufanya kipimo ndipo utajua mbivu na mbichi. Kabla ya kupima kuna dalili za awali ambazo waweza kuzitumia kukupa mwanga kwamba tayari una ujauzito

Je Kila Mwanamke anaweza Kupata dalili za mimba mapema?
Kila mwanamke anatofautiana na mwingine kimaumbile. Kuna wengine hwapati dalili kabisa hata mimba ifike miezi mitano, lakini kuna wanawake wengine huona dalili mapema sana mimba ya miezi mwili tu.
Wanawake wengi hushindwa kugundua mapema kama wana mimba kwasababu dalili nyingi za mimba hufanana na zile za kwenye hedhi mfano kizunguzungu na uchovu.
Dalili zifuatazo zitakupa mwanga iwapo tayari mimba imeingia, japo watakiwa kufahamu kwamba dalili hizi pia zaweza kuwa matokeo ya swala lingine la kiafya. Vipimo ni muhimu kufanyika ili kuwa na uhakika zaidi.
Dalili za Mimba Changa ni hizi
Kupata matone ya Damu nyepesi na Maumivu kwa mbali ya Nyonga
Baada ya mimba kutungwa yai lililorutubishwa hujishikiza kwenye ukuta wa kizazi. Kitendo hichi kinaweza kupelekea kutokwa na matone mepesi ya damu ukeni na maumivu kwa mbali ya nyonga. Damu hii huitwa implantation bleeding, inatokea siku 6 mpaka 12 baada ya mimba kutungwa.
Maumivu ya nyonga kutokana na mimba changa yanaweza kufanana na yale hedhi, wanawake huchanganya hilo na kudhani ni hedhi inaanza. Pamoja na kupata bleed nyepesi mwanamke anaweza kuona uchafu mweupe kama maziwa ukeni. Hiki ni kiashiria cha kuanza kuongezeka kwa ukuta wa kizazi ili kushikilia vyema kiumbe kilichotungwa.
Kumbuka uchafu waweza kuendelea kutoka wakati wote wa ujauzito hilo lisikupe mashaka, lakini kama uchafu utakuwa na harufu mbaya, unaleta muwasho na kujikunhapo unahitaji kuonana na daktari mapema iwezekanavyo kwani waweza kuwa na fangasi au maambukizi ya bakteria ukeni.
Kubadilika Kwa Matiti
Mabadiliko ya matiti ni moja ya kiashiria kwamba tayari una ujauzito. Kutokanana mabadiliko ya homoni , matiti yanaweza kukua na kujaa week moja baada ya kushika mimba. Matiti pia yanaweza kuwa mazito kuiko kawaidana eneo la chuchu kuwa na weusi zaidi.
Ukiona dalili hizi usiwe na hofu, tambua tu kwamba matiti yataendelea kukua ili kujiandaa kunyonyesha.
Uchovu na Kuishiwa Nguvu
Moja ya dalili kubwa ya mimba changa ni kuhisi kuchoka na kusinzia ovyo. Mwanamke huanza kupata dalili hizi wiki moja baada ya kushika ujauzito. Kwanini hali hii itokee? ni kwa sababu ya kuongezeka kwa homoni ya progesterone.
Ukipata dalili hii hakikisha unapata muda mwingi wa kupumzika. Kula zaidi vyakula vya protini na madini chuma.
Kichefuchefu(morning sickness)
Kisababishi kikubwa cha kichefuchefu kwa mimba changa haijulikani lakini mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito inaweza kuchangia. Kichefuchefu yaweza kukupata muda wowote, na kuhisi kutapika, japo kwa wengi hutokea zaidi asubuhi.
Baadhi ya wanawake hushindwa kula baadhi ya vyakula baada ya kupata mimba. Hali hii huchangiwa zaidi na mabadiliko ya homoni. Inawezekana kabisa hali hizi za kuchagua chakula, kichefuchefu ikamuandama mwanamke katika siku zote za ujauzito mpaka pale atakapojifungua.
Hakikisha unakula lishe nzuri kila siku ili kumpa mtoto virutubisho vyote vinavyohitajika.
Kukosa hedhi ni Dalili ya Mimba Changa
Dalili kubwa iliyo wazi ya kwamba tayari una ujauzito ni kupitisha hedhi. Japo siyo kila ukikosa hedhi ni mimba changa hapana, unaweza kukosa hedhi kutokana na mabadiliko ya homoni, kuongezeka uzito ama kupungua kupita kiasi, mwili kuchoka sana, matumizi ya vidonge vya kuzuia mimba .
Ukikosa hedhi zaidi ya week mbili ulizozoea basi hakikisha unanunua kipimo na kupima mkojo kujua kama mimba ipo.
Dalili zingine ya Kwamba una Mimba Changa
Kukojoa mara kwa mara: Kwa wanawake wengi hali hii huanza baada ya week 6 mpaka 8 ukishika mimba. Lakini kumbuka dalili hii yaweza pia kusababishwa na UTI na kisukari, muhimu kupima.
Kukosa choo ama kupata choo kigumu: kutokana na mabadiliko ya homoni, chakula hupunguza kasi ya kupita kwenue utumbo mdogo. Kupunguza tatizo hakikisha unakunywa maji ya kutosha, fanya mazoezi na kula vyakula visivyokobolewa na vya kambakamba kwa wingi.
Kubadilika kwa mood yako; hasa katka miezi mitatu ya mwanzo
Maumivu ya kichwa na mgongo,inatokea zaidi kwa wanawake wengi wenye ujauzito
Fahamu kwamba mwanamke mjamzito anaweza kuwa na dalili zote hizi ama akawa na dalili baadhi. Kama moja ya dalili hizi itakuboa na kukufanya ujisikie vibaya, ongea na daktari wako atakupa ushauri vizuri.
23 replies on “Dalili za Mimba Changa”
je kupata maumivu chini ya kitovu ni dalili ya mimba changa?
tafadhali rudia kusoma hiyo makala ya dalili za mimba
Je kuvimba ndani ya uke na kuhisi maumivu makali wakati wakukojoa hiyo ni dalili ya ugonjwa gani?
inawezekana ni maambukizi ya bakteria ukeni, nashauri uende hospitali mapema kupata huduma
kuhalisha, maumivu ya tumbo na mwili kukosa nguvu ni dalili ya mimba
zinaweza kuwa dalili za mimba, ila ni muhimu kununua kipimo cha mkojo (UPT) ili upate uhakika
Sasa kwa mwanamke aliye lala na mwanaume kwa siku zakumaliza hedhi yake yani siku ya kwanza na kuendeleya mbaka siku ya kumi mwanamke anaweza kuchukuwa mimba??
Niko na siku tano nikitematema mate, kuchoka na matiti kuwa uchungu
uende hospitali ya karibu yako kupima
mimba yaweza kuingia siku yoyote
Mwanamke aliye shiriki tendo la ndoa katika kipindi cha hedhi anaweza kupata mimba?
chansi ni ndogo sana ya kushika mimba lakini bado inawezekana, hasa kama ana mzunguko mfupi
Je kujiskia kichefuchefu na kutapika alafu hajiskii vibaya ni nin?
Ugonjwa gan mbaya uki mkuta mwana mke mwenye mimba ni hatar kwa afya yake na mtoto
ugonjwa wowote kujumla siyo salama kwa mjamzito
Kupata vichomi ni dalili ya mimba?
je ukiona dam inatoka ukeni na uke kuwa mkavu hivi na ute kuwa kam yai na nyonga kuuma ni dalili ya mimba
je mwanamke akiwa na kichocho anaweza kupata mimba??
Nenda hospitali utibiwe kwanza kabla hujaamua kubeba mimba
Najisikia mate kujaa mdomoni na hezi yangu inatoka nyepesi na ni nyeusi maumivu ya kichwa inaweza ikawa ni nn
HEEE
Nina mwezi sasa sijaona hedhi natumekua tukitumia withdrawal baada ya kutoa family shida inaezakua gani
Unaweza kuwa na mimba,nunua kipimo ujipime