Uchafu Mweupe Ukeni Kabla ya Hedhi

uchafu mweupe ukeni
discharge

Je ni kawaida kutokwa uchafu mweupe kabla ya hedhi?

Wanawake wengi wanapata uchafu wa aina mbalimbali katika mzunguko wao wa hedhi. Unaweza kupata uchafu mweupe wenye ujazo wa kijiko kila siku na uchafu waweza kubadilika pia rangi zake siku hadi siku.

Mabadiliko haya rangi na harufu za uchafu ni matokeo ya kinachoendelea mwilini kwa maana ya na mabadiliko ya homoni na mazingira ya uke pia. Hapa chini tumechambua kwa kina nini kiashiria cha uchafu mweupe, aina zingine za uchafu na muda gani sahihi wa kumwona daktari

Uchafu Mweupe kabla ya hedhi unamaanisha Kitu gani

Kitalamu uchafu mweupe huu unaotokea kuelekea hedhi unaitwa leukorrhea. Uchafu huu wakati mwingine huwa wa njano umeundwa kwa seli na majimaji yaliyosafishwa kutoka ukeni.

Stage hii kwenye mzunguko wa hedhi huitwa luteal phase. Ni wakati ambapo homoni ya progesterone huzalishwa kwa wingi na hivo kusababisha uchafu mwupe au rangi ya wingu. Baadhi ya wanawake wazoefu wanaweza kutumia utokaji wa uchafu ukeni kama njia asili ya uzazi wa mpango.

Uteute mweupe mwembamba unaovutika ni uteute wa mimba, unatoka kipindi ambapo yai limepevuka. Uteute mzito mweupe ni ute usio wa mimba.

Uke ni Kiwanda Kinachojisafisha

Fahamu tu kwamba haijalishi rangi na mwonekano wa uteute unaotoka ukeni, siku zote utokaji wa ute ni ishara ya uke kujisafisha ili kuwa salama.

Nini Kinasababisha Kutokwa na uchafu mweupe ukeni kabla ya hedhi?

Sababu kubwa za uchafu ama ute ute huu mwupe kuelekea hedhi ni pamoja na
Utendaji salama wa via vya uzazi: Kwamba usiwe na hofu ni stage katika mzunguko wako kutokana na mabadiliko ya homoni.
Matokeo ya uzazi wa mpango: Kama unatumia uzazi wa mpango unaoavuruga homoni kama sindano , vidonge na njiti inasababisha kuongezeka kwa uchafu unaotoka ukeni.
Mimba: Kutokwa uchafu wakati unakaribia hedhi inaweza kuashiria kwamba mimba imeshika. Uchafu huu unaoashiria umeshika mimba unakuwa mzito, wenye cream unaoambatana na damudamu kwa mbali.

Magonjwa ya zinaa: Magonjwa ya kuambukizwa kwa njia ya ngono kama gonorrhea,chlamydia na trichonomiasis yanaweza kusababisha utokwe na uchafu mwingi. Muone daktari kama uchafu unageuka kuwa wa njano na kijani. unaoambatana na muwasho na harufu mbaya.

Fangasi ukeni: Fangasi ukeni ni tatizo kubwa sana kwa wanawake hivi sasa. Uchafu wa fangasi unakuwa mzito, mweupe na unaokatika kama maziwa mgando. Fangasi pia husababisha muwasho na hali ya kuchomachoma ndani ya uke na kwenye mashavu ya uke.

Maambukizi ya bakteria( bacterial vaginosis)
Maambukizi haya hutokea pale kiwango cha bakteria wazuri wanapopungua ukeni. Vihataraishi vikubwa ikiwa ni uvutaji wa sigara, kuwa na wapenzi wengi na kuosha sana uke mpaka ndani. Uchafu huu unaambatana na harufu ya shombo la samaki.

Mabadiliko Ya Uteute na Uchafu ukeni Katika mzunguko wako wa hedhi

Baada ya hedhi kuisha tegemea uke kuwa mkavu kwa siku tatu mpaka nne. Baada ya hapo utaona uteute mweupe unaonata kwa siku tatu mpaka tano. Kipindi hiki huitwa follicular phase ambapo yai linaanza kukua taratbu kuelekea kukomaa.

Wakati wa ovulation(yai kupevuka) tegemea kupata uteute mwepesi unaovutika kama yai. Katika kipindi hiki uteute huwa mwingi mara 30 zaidi ya ute ulozoea. Ute huu unateleza sana ili kusaidia mbegu kuogelea vizuri kwenda kurutubisha yai.

Uchafu Mweupe Baada ya Ovulation

Baada ya ya ovulation uteute mweupe huanza tena kutoka kuotokana na kuongezeka kwa homoni ya progesterone. Uteute huu utaendelea kutoka na kubadilika kuwa mgumu kama gundi unavoanza tena kukaribia hedhi.

Siku chache kabla ya hedhi unaweza pia kupata uteute wa njano. Na baada ya period inawezekana pia kupata uteute wa rangi ya brown. Uchafu wa brown ni matokeo ya mabaki ya damu ya hedhi yanatolewa.

Kutokwa na uteute wenye matone ya damu siku chache kabla ya siku uliyozoea kuanz ahehdi inaweza kuashiria umeshika mimba. Kama hedhi yako ikichelewa zaidi fanya kipimo cha mimba upate uhakika zaidi.

Lini unatakiwa Kumwona Daktari

Endapo uteute wako unaambatana na dalili hizi ni muhimu umwone daktari, kwani yaweza kuwa una maambukizi ya bakteria, fangasi au magonjwa ya zinaa. Dalili hizi ni

  • maumivu na hali ya kuwaka moto ukeni
  • vidonda ukeni
  • harufu mbaya ukeni
  • wekundu ukeni
  • kuvimba sehemu za uke ikiwemo mashavu na kisimi

Bofya kusoma kuhusu: Chanzo cha harufu mbaya ukeni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *