Kushika Mimba Baada ya Uzazi wa Mpango

uzazi wa mpango
uzazi wa mpango

Baada ya kutumia uzazi wa mpango kwa muda mrefu sasa imefikia kipindi unataka kushika mimba ingine upate mtoto. Najua unaweza kuwa na wasiwasi sana pengine kutokana na maneno uliyosikia kwa wengine juu ya madhara ya uzazi wa mpango.

Ni kweli kwamba kwa baadhi ya wanawake inaweza kuchukua miezi/miaka mingi kushika tena mimba baada ya kuacha kutumia uzazi wa mpango. Hasa kama njia unayotumia imeathiri mpangilio wa homoni. Hapa chini ni mambo ya muhimu unayotakiwa kuyafahamu unapotaka kushika mimba baada ya uzazi wa mpango.

Lini Watakiwa Kuacha Kutumia Uzazi Wa Mpango?

Mpaka pale utakapokuwa tayari kushika mimba ingine ndipo uache kutumia uzazi wa mpango. Maana unaweza kushika mimba ndani ya mwezi mmoja ukishaacha kutumia uzazi wa mpango. Kama umechoka kutumia njia kama kitanzi, sindano au vidonge unaweza kutumia kondomu kwa kila tendo la ndoa mpaka pale ukiwa tayari kushika mimba.

Muda gani nitashika mimba baada ya kuacha uzazi wa mpango?

Kama unatumia njia za kuzuia mbegu kama kondomu, unaweza kushika mimba mapema zaidi endapo tu usipotumia. Wanawake wengi huweza kushika mimba ndani ya miezi michache baada ya kuacha kutumia uzazi wa mpango wa homoni kama kitanzi, njiti, sindano na vidonge.

Hapa chini ni maelezo kwa kila aina ya uzazi wa mpango, jiangalie upo kwenye kundi gani.

Njia za Kupanga Uzazi

Vidonge vya kupanga uzazi(birth control pills): Unaweza kushika mimba ndani ya miezi mitatu baada ya kuacha kumeza vidonge. lakini wanawake wengi hushika mimba ndani ya mwaka mmoja.

Kitanzi: Kuna uwezekano ukashika mimba mapema sana baada tu ya daktari kukutolea kitanzi. Wanawake wengi huanza kutoa mayai(ovulation) baada ya mwezi mmoja kitanzi kikiondolewa, baadhi huchukua miezi 6 mpaka mwaka mmoja.

Njiti: Kama ilivyo kwa kitanzi inawezekana kushika mimba mapema baada tu ya kutoa kitanzi. Wanawake wengi huanza kutoa mayai yaliyokomaa baada ya mwezi mmoja .

Sindano: Kwa kulinganisha na njia zingine za kupanga uzazi sindano yaweza kukufanya uchukue muda mrefu zaidi kushika mimba baada ya kuacha kuchoma. Wanawake wengi huchukua miezi mpaka 10 mayai kuanza kupevuka, wachache huchukua hata miaka miwili na zaidi.

Na ndio maana madaktari wanashauri kama unataka kushika mimba mapema zaidi ndani ya mwaka mmoja baada ya kuacha uzazi wa mpango basi usitumie sindano, maana zaweza kukuchelewesha zaidi.

Je ni salama kubeba mimba mapema tu baada ya kuacha uzazi wa mpango?

Jibu ni ndio. Tafiti za hivi karibuni zimethibitisha kwamba ni salama kushika mimba mapema tu baada ya kuacha kutumia uzazi wa mpango.

Je ni lazima upate hedhi kwanza ndipo ushike mimba?

Siyo lazima. Baadhi ya wanawake hawapati hedhi miezi kadhaa baada ya kuacha kutumia uzazi wa mpango. Ni kwasababu njia hizi za kupanga uzazi hubadili mpangilio wa homoni.

Lakini fahamu kwamba waweza kushika mimba hata kabla ya kupata hedhi. Kama yai limeanza kutolewa mapema kabla ya hedhi na ukakutana na mwanaume bila kinga unaweza kushika mimba.

Nawezaje Kujua Kama Yai Limepevuka?

Njia ya uhakika zaidi ni kwa kutumia ovolation kit. Hizi waweza kuzipata famasi. Zinatumika kufatilia lini yai linapevuka na kutolewa tayari kwa urutubishaji.

Lakini kuna viashairia vingine ambavyo mwili huonesha mfano kuongezeka kwa joto la mwili, hamu ya tendo kuongezeka na kupata ute ute unaovutika kama yai.

Na je Vipi kama usiposhika mimba hata baada ya kuacha uzazi wa mpango?

Endapo umeacha kutumia uzazi wa mpango na mimba imegoma kuingia kwa zaidi ya mwaka mmoja ni jambo la msingi ukienda kuonana na daktari akufanyie vipimo na tiba. Mtaalamu wa magonjwa wa wanawake atakufanyia upembuzi tatizo lako na anaweza kutoa ushauri na tiba ya kukusaidia ushike mimba mapema.

Tumia Evecare na UCP ushike mimba mapema

Faida na kazi za Evecare+UCP kwa mwanamke

  1. Kusafisha kizazi na mirija ya uzazi
  2. Kurekebisha homoni
  3. Kuchochea upevushaji wa mayai
  4. Kuimarisha uzalishaji wa uteute wa uzazi na hivo kuongeza chansi ya kushika mimba mapema ndani ya miezi miwili baada ya kumaliza dozi.

Gharama ni Tsh 125,000/= Tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254 uanze tiba.

Tahadhari

Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge fake vya evecare na ucp, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb

Bofya kusoma kuhusu: chanzo cha ukavu ukeni na kushindwa kufurahia sex