Kupiga Punyeto Kwa Mjamzito

kupiga punyeto kwa mjamzito
orgasm

Wakati huu moja ya jambo unaloweza kuwa unawaza sana ni kupiga punyeto kwa mjamzito kama ni salama. Wakati wa ujauzito ni kipindi cha furaha sana. Lakini kwa mimba ya kwanza inaweza kuwa kipindi cha ovyo kweli kutokana na mabailiko ya mwili.

Kwa ujauzito wa kwanza unakuwa unajifunza vitu vigeni kabisa kwako, unajifunza kipi ni salama na kipi usitumie. Pengine unajaribu kulinganisha ulichosoma mtandaoni na ulichoambiwa kliniki.

Kuna baadhi ya mambo kama kupiga punyeto na kujiridhisha mwenyewe vitakujia akilini. Pengine utaogopa kuuliza kwa watu kama ni salama kulingana na mila na desturi zetu. Makala hii itakupa majibu kwa mawali yako kuhusu kupiga punyeto wakati wa ujauzito.

Je ni Salama Kupiga Punyeto kwa Mjamzito?

Ukiwa mjamzito bado utahitaji kuridhika kingono (kufika kileleni)kama mwanamke mwingine. Wakati wa ujauzito hamu ya tendo la ndoa inaongezeka sana kwa wanawake wengi kutokana na mabadiliko ya homoni.

Wanawake wachache sana hujikuta hawana hamu ya tendo kabisa wala kupiga punyeto. Dalili mbaya kama kukosa nguvu, kichefuchefu na kutapika vinaweza kukutoa kabisa kwenye kuwaza mapenzi.

Baadhi ya wanawake hupata maumivu kwa mbali pale wanapofika kileleni wakati wa kufanya tendo au wakati wanapiga punyeto kujiridhisha wenyewe. Hali hii huletekezwa na kutanuka na kusinyaa kwa msiuli ya kizazi.

Mimba Kuharibika Na kufika kileleni

Kwa baadhi ya wanawake wachache sana walio kwenye hatari ya mimba kutoka, au wenye historia hiyo, kufika kileleni kunaweza kupelekea mimba kutoka pia. Mbegu za mwanaume zinapoingia zinafanya mlango wa kizazi kuwa laini na mimba kutishia kutoka. Hii ni kwa wanawake wachache mno, na utajulishwa jambo hili wakati unahudhuria kliniki.

Faida za Kupiga Punyeto Kwa Mjamzito

Wanawake wengi hupata furaha sana na kujihisi wepesi pale wanapopiga punyeto kipindi cha ujauzito. Kwa maana ni njia mojawapo ya kujitosheleza kihisia bila kuhitaji mwanaume wakati huu ambapo tumbo ni kubwa na unaona karaha kuingiliwa na mwanaume.

Kadiri mimba inavokuwa kubwa inakuwa changamoto sana kutafuta staili nzuri ya kutombana ili usiumie. Wanawake wengi wanahofu kwamba baadhi ya mikao itaumiza mtoto aliye tumboni. Kwenye jambo hili itahitaji kupiga punyeto ili kujiridhisha.

Kupiga punyeto wakati wa ujauzito haina tofauti sana na wakati mwingine ukiwa huna mimba. Kama unapendelea toy au vifaa fulani usitumie kama vitakuletea maumivu. Usitumie vifaa kupiga punyeto kama una historia ya mimba kuharibika, uliwahi kujifungua kabla ya wakati, unapata bleed ama mlango wa kizazi upo karibu.

Lini Hutakiwi Kupiga punyeto ukiwa mjamzito?

Katika mazingira fulani ya afya yako daktari anaweza kushauri usifanye ngono kabisa mpaka utakapojifungua. Katika mazingira yafuatayo haitakiwi kupiga punyeto wala kukutana kingono na mwanaume wako

  • una viashiria vya kujifungua mapema kabla ya muda wako
  • una historia ya kuzaa mapema
  • umepimwa na kugundulika una shida ya kondo la nyuma
  • umekuwa ukitokwa na damu katika ujauzito wako

Mwisho kabisa kama huna matatizo yoyote kwenye ujauzito wako, kupiga punyeto na kufika kileleni ni salama. Labda tu uwe umeshauriwa nadaktari kwamba usifanye hivo.

Bofya kusoma makala inayofuata kuhusu hamu ya tendo la ndoa kwa mjamzito

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *