Majipu ukeni, chanzo, ushauri na tiba

majipu ukeni
afya ya uke

Majipu ukeni mara nyingi husababishwa na bakteria wanaoshambulia eneo la unywele unapoota. Majipu mengi hutokea kutokana na athari ya bakteria wa Staphylococcus aureus. Sababu zingine ni pamoja na kuziba kwa tundu la jasho.

Kwa kiasi kikubwa jipu ukeni linaweza kuisha lenyewe ndani ya siku ama wiki kadhaa. Kuna njia mmbalimbali unaweza kufanya kupunguza maumivu na ukaharakisha mchakato wa kupona.

Kabla ya kubinya jipu, hakikisha umeosha mikono yako kwa maji na sabuni vizuri. Bila kuosha mikono kuna hatari ya kuleta maambukizi ya bakteria kwenye jipu na hivo tatizo kuwa baya zaidi. Baada ya kujitibia pia, osha mikono yako vizuri ili kupunguza hatari ya kusambaza bakteria maeneo mengine ya mwili.

Inachukua muda gani kupona majipu ukeni?

Jipu la ukeni mara nyingi huisha ndani ya wiki moja. Majipu mengi hunywea na kupotea na vingine hupasuka na kukauka. Kama jipu likipasuka, safisha eneo hilo vizuri na ueke bandage ndogo. Osha mikono yako vizuri na uwe unabadilisha bandage.

Kuota jipu moja siyo kwamba ni lazima utaota na majipu mengine mengi. Japo baadhi ya sababu hatarishi zinaweza kupelekea kuongezeka kwa majpu. Sababu hizi ni kama

 • msuguano wa eneo husika na nguo iliyobana
 • kuota vinyweleo baada ya kunyoa
 • maambukizi zaidi ya bakteria au virusi

Kama majipu yataongezeka zaidi, hakikisha unaenda hospitali kumwona daktari. Yawezekana unaugua ugonjwa unaopelekea upate jipu. Daktari atakuchunguza na kutibu chanzo cha tatizo ili kuzuia usiote majipu zaidi siku za baadae.

Matibabu ya hospitali

Kukata jipu na kulikausha. Endapo jipu lako ni kubwa na linauma, daktari anaweza kuamua kulikata na kukausha usaha wote na uchafu. Usijaribu kufanya jambo hili ukiwa nyumbani, hakikisha unaenda hospitali na kupewa huduma na daktari.

Dawa za antibiotics: Endapo maambukizi yanajitokeza mara kwa mara, hapo itahitaji upewe dawa za kuua bakteria maarufu ama antibiotics. Dawa hizi zinaangamiza bakteria wabaya wanaosababisha majipu na kuzuia maambukizi kwa siku za baadae.

Namna ya kujikinga na majipu ukeni kwa siku zijazo

 • badili wembe wa kunyolea kila mara
 • usichangie wembe wa kunyolea sehemu za siri na mtu mwingine
 • nyoa nywele baada ya kuzipaka lotion ya kunyolea au maji
 • nyoa mavuzi kwa uelekeo wa nywele
 • tumia antibiotics mpaka ziishe ili kupunguza hatari ya maambukizi kurudi tena.
 • kama una magonjwa ya zinaa hakikisha unapata tiba stahili kwa muda muafaka.

Tiba asili kuondoa majipu ukeni

1.Weka kitu cha moto kwenye eneo lililoathirika.

2.Tumia mafuta tiba ya tea tree kwa kupakaa eneo husika mara mbili kwa siku.

3.Unga wa manjano: manjano yana viambata vinavyoua bakteria wabaya na pia kupunguza ngozi iliyotutumka. Changanya manjano, maji na tangawizi na upakae mara mbili kwenye jipu.

4.Mafuta ya mnyonyo: Mfauta haya yana kiambata cha ricinoleic acid, kiambata ambacho kinapunguza kuvimba kwa ngozi. Tumia kiwango kidogo cha mafuta ya mnyonyo kwa kupakaa mara tatu kwa siku mpaka jiu liishe.

5.Mafuta ya mwarobaini; Mwarobaini ni antibiotics ya asili, inasaidia kutibu maambukizi ikiwemo ya kwenye jipu. Kutibu jpu lako, pakaa mafuta kidogo kwenye eneo lililoathirika mara tatu kwa siku. Hakikisha umeosha mikono vizuri kabla ya kuanza tiba.

Lini unatakiwa kumwona daktari

Baadhi ya dalili siyo nzuri na zinaashiria kwamba kuna tatizo la kiafya, linalohitaji tiba ya mapema. Dalili hizi ni kama

 • homa
 • kutokwa na jasho jingi
 • jipu kuuma zaidi
 • kutokewa na jipu kubwa zaidi ya inch mbili
 • jipu lisiloisha hata baada ya wiki mbili

Tiba kupitia vidonge asili vya UCP-Uterus cleansing pills

Kwa mwanamke mwenye changamoto ya kutokwa majipu ukeni mara kwa mara kutokana na maambukizi ua fangasi au bakteria, tunashauri atumie uterus cleansing pill kusafisha uke. Uterus cleansing pill (UCP) ni vidonge 2 vilivyotengenezwa kitaalamu kwa kuzingatia uasili wa dawa kutatua changamoto za wanawake kama majipu na vidonda ukeni, muwasho, fangasi ukeni, kutokwa uchafu na harufu mbaya ukeni.

Dozi moja yenye vidonge viwili vinatumika kwa wiki moja, na yatakiwa utumie dozi mbili. Kidonge kimoja kinawekwa ukeni na kutolewa baada ya siku 3, kisha unapumzika masaa 24 unaweka tena kidonge kingine.

Gharama ni Tsh 50,000/=

Angalizo pale unapotumia Uterus Cleansing Pill.

Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge vyenye mfanano na hivi vya UCP, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb.

Kumbuka dawa haitumiki kwa wanawake bikira na wajawazito. Usifanye tendo la ndoa wakati huo upo kwenye dozi, ukianza hedhi pumzika kutumia vidonge hivi mpaka pale utakapomaliza hedhi.

Tunapatikana Mwembechai Dar, Tuandikie kwa whatsapp no-0678626254 kuanza tiba.