Hedhi Baada Ya Kujifungua

ufatiliaji wa mzunguko-kushika mimba
mzunguko wa hedhi

Lini hedhi yangu itarudi baada ya kujifungua?

Hedhi baada ya kujifungua kwa kiasi kikubwa itarejea baada ya week sita mpaka nane baada ya kujifungua, endapo umeamua kutonyonyesha mtoto ziwa la mama. Kama umeamua kunyonyesha hapo kuna mawili, inaweza kurudi mapema ama ikachelewa zaidi.

Kwa wale wanaonyonyesha mtoto bila kumpa chakula kingine, wanawaeza wasipate kabisa hedhi kipindi chote cha kunyonyesha.

Kama hedhi yako itarudi mapema baada ya kuzaa kwa njia ya uke, daktari ana weza kushauri usitumie tampon. Hii ni kwasababu njia ya uke bado inapona, na tampon zinaweza kupelekea ukapata maambukizi.

kwanini hedhi baada ya kujifungua inachelewa sana kwa mama anayenyonyesha?

Kikawaida wanawake wanaonyonyesha hawapati hedhi haraka kwasbabu ya mabadiliko ya homoni. Homoni ya maziwa yani prolactin inakuwa juu sana na hivo kupelekea homoni zingine za hedhi kuwa chini. Na matokeo yake mayai yanakuwa hayapevuki na hivo urutubishaji haufanyiki kabisa. Bila yao kupevuka hedhi yaweza isitoke.

Je hedhi yaweza kuathiri uzalishaji wa maziwa ya mama?

Hedhi inaporejea, unaweza kuona mabadilko fulani kwenye kiwango cha maziwa, ratiba ya kunyonyesha na hata hamu ya mtoto kunyonya. Mabadiliko ya homoni ndio yanapelekea hali hii kwenye maziwa.

Unaweza kuona kiwango cha maziwa kikipungua, pia hata wewe unavojisikia kunyonyesha mtoto yaweza kupungua. Na ladha ya maziwa kwa mtoto pia inaweza kubadilika. Mabadiliko haya kwa kiasi kikubwa siyo tatizo, ni kawaida, na hayatakiwi kukuzuia wewe kumnyonyesha mtoto wako.

Vipi Kuhusu Uzazi wa Mpango?

Baadhi ya wanawake wanatumia njia ya kunyonyesha kama njia asili ya kupanga uzazi. Kitaalamu njia hii huitwa lactation amenorhea method-LAM. Inafanya kazi vizuri zaidi kwenye miezi 6 ya mwanzo ambapo kiafya haitakiwi umpe mtoto chakula kingine zaidi ya maziwa ya mama tu.

Pamoja na kwamba kunyonyesha kunapunguza chansi yako kushika mimba, hutakiwi kuitegemea njia hii asilimia mia. Kuna wakati inaweza kukuangusha ukajikuta umeshika mimba na mtoto bado mdogo.

Masharti ikiwa unatumia njia ya kunyonyesha kujizuia mimba

Endapo unataka kutumia njia ya kunyonyesha kupanga uzazi basi hakikisha masharti haya unatimiza, yatakiwa

  • mwanamke awe hajaanza kupata hedhi tangu azae
  • uwe unanyonyesha mara kwa mara bila kupitisha masaa manne
  • mzazi yupo chini ya miezi sita baada ya kujifungua na
  • mtoto bado hajaanzishiwa chakula zaidi ya maziwa ya mama

Kumbuka: Kipengele kimoja tu kikikosekana hapo juu basi hi njia inakuwa haifai tena kupanga uzazi.

Kama hutaki kushika mimba ingine haraka, basi tumia njia zingine za uhakika kujizuia na mimba. Kama hedhi yako ikianza kutoka, hapo nakushauri usiendelee kutumia tena njia hii. Badala yake nenda hospital ama kituo cha afya, upate maelekezo ya njia zingine za uhakika kupanga uzazi kama kitanzi, njiti, sindano na vidonge.

Je hedhi baada ya kujifungua itabadilika?

Pale hedhi yako ya kwanza inaporudi, lazima utaona mabadiliko sana ya hedhi tofauti n kipindi kabla hujazaa. Kumbuka kipindi hichi mwili wako unajirudi kwenye hali yake ya zamani. Unaweza kuona mabadiliko haya kwenye hedhi:-

Hedhi ya kwanza baada ya kuzaa yaweza kuwa nzito sana kuliko ulivozoea, pia maumivu yaweza kuongezeka kutokana na kuongezeka kwa ukuta wa kizazi. Kadiri unavoendelea na hedhi ijayo mabadiliko yatapungua na dalili mbaya zitaisha.

Wanawake waliowahi kuugua endometriosis kabla ya kushika mimba wanaweza kupata hedhi nyepesi zaidi baada ya kuzaa.

Nini kinapelekea ongezeko la maumivu kwenye hedhi ya kwanza?

Maumivu kwenye hedhi yako ya kwanza baada ya kuzaa yanaweza kupelekewa na sababu nyingi kama

  • ongezeko la ukuta wa kizazi
  • kasi ya kubomoka kwa ukuta kuongezeka
  • mabadiliko ya homoni wakati wa kunyonyesha

Nitegemee nini kwenye hedhi yangu ya kwanza?

Aidha ukijifungua kawaida ama kwa upasuaji, lazima ulipata kutokwa damu baada ya kujifungua.

Kwenye wiki za kwanza baada ya kujifungua ukuta wa kizazi utaanza kubomoka na kutokwa na damu. Damu hii nimabaki ya kuta zilizojengwa wakati una mimba ili kusapoti mtoto. Katika kipindi hichi utapata damu nzito sana , sometime iliyoganda.

Ute wa kawaida baada ya kuzaa-Lochia

Kadiri mda unavosogea damu itapungua na utanza kupata ute mweupe au mwekundu wa cream. Ute huu kitaalamu huitwa lochia.

Ute huu unaweza kuendelea kutoka kwa zaidi ya week sita, na hapo hedhi itaanza endapo hunyonyeshi. Endapo ute huu wa lochia umestop kuitoka mapema, na kisha ukaona damu, nasi hiyo ndio hedhi yako ya kwanza imewahi tu kutoka.

Tofauti kati ya hedhi na Lochia

Kama huna uhakika kwamba kinachotoka ni hedhi au bado ni uchafu wa ukeni, tazama maelezo haya.

  • uchafu yani lochia ni mwepesi na unaweza kuwa wa majimaji au mweupe kimwonekano na unatoka mapema kabla ya week 6. Kama utaona damu nyepesi baada ya week sita basi hiyo ni hedhi
  • lochia inaongezeka kutoka pale unapofanya kazi zaidi. kwahiyo kama bled hiyo inapungua ukipumzika na inaongezeka ukifanya kazi hiyo bado ni lochia na siyo period.
  • pia lochia inakuwa na harufu yake ya tofauti. inaweza kuwa na harufu flani tamu kwavile imechanganyika na mabaki ya mimba.

Mzunguko wa hedhi unatengemaa lini?

Kumbuka yaweza kuchukua mda mrefu kabla ya mzunguko wako kutengemaa baada ya kuzaa. Unaweza kushangaa hedhi ya kwanza ikawa ndefu sana, ya pili ikaja mapema zaidi kuliko ya mwezi ulopita.

Tambua kwamba ni kawaida kwenye mwaka wa kwanza hedhi kuvurugika katika ya mzunguko na mzunguko. Pia kiwango cha hedhi na utokaji wake byaweza kupishana kwa kila mwezi. hi inatokea sana kama unanyonyesha mda mwingi.

Dalili gani mbaya baada ya kujifungua natakiwa kuwa nazo makini?

Ni muhimu sana kuwasiliana na daktari endapo utapata moja ya dalili hizi

  • damu nyingi kiasi ya kutumia pedi zaidi ya moja kwa lisaa
  • bleed inayoambatana na maumivu makali sana
  • homa
  • bleed ya zaidi ya siku saba
  • kutokwa na harufu mbaya ukeni
  • maumivu makali ya kichwa
  • kupata mabonge ya damu makubwa
  • kushindwa kupumua na
  • maumivu wakati wa kukojoa

Mpigie daktari au nenda hospital haraka endapo utapata dalili hizi au dalili yoyoyte unayoona siyo ya kwaida.

Soma makala zinazofuata Kuhusu: Sindano za kupanga uzazi na

Aina za kitanzi, faida na madhara yake