Categories
Afya ya mwanamke na uzazi Malezi ya Mtoto na Kunyonyesha

Chanzo cha Mama kukosa Maziwa baada ya Kujifungua na Tiba

mama kukosa maziwa baada ya kujifungua

Pale unapojifungua kuna vitu unatagemea na kutakiwa kuzingatia, kuanzia kwenye mikao ya kunyonyesha, kumlaza mtoto na usafi wa mtoto. Mama kukosa maziwa baada ya kujifungua ni mtihani mkubwa sana kwa mwanamke anapojifungua. Leo utasoma kwanini maziwa yanatoka kidogo na nini cha kufanya ili kuongeza maziwa.

Je utajuaje maziwa yanyotoka ni kidogo na hayatoshi kwa mtoto?

Kama unanyonyesha mtoto kwa chupa ni rahisi kujua kiwango gani anatumia kwa siku. Lakini kama unanyonyesha kikawaida ni ngumu kujua mtoto anameza kiwango gani cha maziwa, kwahivo unatakiwa kujua viashiria vingine vya mtoto kushiba.

Mama kukosa maziwa nyakati za usiku

Wamama wengi hawanyonyeshi usiku, hasa kwaavile wanakuwa wamechoka na wanahitaji kupumzisha miili yao. Kwahivo kiwango cha homoni ya prolatin kitashuka na kupelekea maziwa kuzalishwa kidogo hata nyakati zingine. Prolactin ni kichocheo ambacho kinachochea maziwa yazalishwe mengi ili mtoto anyonye vizuri. Pia maziwa ya usiku yanakuwa na kiwango kikubwa cha mafuta mazuri ambayo ni muhimu kwa ukuaji wa mtoto.

Mama kukosa maziwa baada ya kujifungua: Dalili za kuoenesha maziwa yapo ya kutosha

Tatizo hili la mama kukosa maziwa linawapata watu wachahe sana. Hapa chini ni dalili za kukuonesha maziwa ya mtoto yapo mengi na yanatosheleza

Uzito wa mtoto haupungui na kuongezeka. Ni kawaida kwa mtoto kupoteza asilimia 5 mpaka 7 ya uzito kwenye siku za mwanzoni. Lakini uzito unatakiwa kurudia hali ya kuzaliwa ndani ya siku 10 mpaka 14.

  1. Mashavu ya mtoto yanaonesha yametuna wakati ananyonya
  2. Mtoto kupata choo mara tatu kwa siku katika siku za mwanzo baada ya kujifungua
  3. Mtoto haoneshi dalili yoyote ya kuishiwa maji, dalili kama kulia sana, mkojo mwekundu, mdomo mkavu na macho kuingia ndani
  4. Endapo mtoto ni mtulivu wakati wa kunyonya na anaachia nyonyo yeye mwenyewe baada ya kushiba
  5. Matiti yanaonekana laini sana baada ya kunyonyesha. Kabla ya kunyonyesha maziwa yanakuwa yamejaa na yakipungua maziwa yanakuwa laini na kunywea
  6. Mtoto anaonekana kumeza wakati huo ananyonya

Nini kinapelekea mama kukosa maziwa baada ya kujifungua?

Kuna sababu nyingi kwanini umejifungua hivi karibuni na maziwa ni kidogo sana au hayatoki kabisa. Baadhi ya sababu ni hizi

  • Matumizi ya vidonge kupanga uzazi
  • Kushindwa kumuweka mtoto vizuri ili adake titi
  • Mabaki ya kondo la nyuma kwenye kizazi
  • Historia ya upasuaji kwenye matiti
  • Kuvusha damu nyingi wakati wa kujifungua
  • Matumizi ya baadhi ya dawa baada ya kujifungua mfano dawa za aleji
  • Kumwanzishia mtoto maziwa bandia mapema sana bila kukamua maziwa yako mwenyewe

Mama kukosa maziwa baaa ya kujiungua: Nini kifanyike ili kuongeza maziwa ya mama?

Kunyonyesha kuna faida nyingi sana kwa mtoto na kwa mama. Kwa bahati nzuri kuna njia nyingi za kusaidia kuongeza maziwa ya mama ili mtoto anyonye zaidi.

  1. Nyonyesha au kamua maziwa mara kwa mara kadiri uwezavyo. kunyonya mara kwa mara kunashtua homoni ya hivo kuchochea zaidi uzalishaji wa maziwa. Hakikisha unanyonyeha mara 8 mpaka 12 kwa siku. Na kama maziwa yatakuwa kengi zaidi basi yakamue na yatunze ili utumie baadae
  2. Usimpe mtoto formula wala maziwa ya ng’ombe katika miezi 6 ya mwanzo. Tafiti zinaonesha mama anapunguza uzalishaji maziwa pale akianza kulisha mtoto chakula
  3. Badili titi unalompa mtoto kila unapotaka kunyonyesha, usikomae na titi moja pekee, tumia yote ili kuhakikisha maziwa yanaisha kwenye titi na hivo kuhochea mengine kuzalishwa
  4. Hakikisha unakunywa maji mengi na usiwe na kiu, pia upate muda wa kupumzika. Mwili wako unahitaji sana majimaji na lishe nzuri ukiwa unanyonyesha. Kula vyakula mbalimbali na, juisi na maji ili mtoto apate maziwa ya kutosha.
  5. Mpe mtoto nyonyo mda wote akiwa na njaa. Muweke mtoto karibu na titi utajua anataka kunyonya au kashiba
  6. Usilalie tumbo na matiti. Kugandamiza matiti inapunguza uzalishaji maziwa

Kwa ushauri na Tiba asili Tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *