Nini maana ya picha za X?
Picha za X au video za X ni mkusanyiko wa picha ama video zinazoonesha utupu wa binadamu. Lengo la picha na video hizi ikiwa ni kuamsha hisia za kimapenzi za mtazamaji. Video hizi zinatengeneza uraibu kiasi kwamba mtu anakuwa kama teja, hawezi kupitisha siku bila kuingia mtandaoni kutizama video za ngono.
Katika makala hii nitatumia maneno picha za X, video za X, video za ngono au pono kumaanisha kitu kimoja hichohicho. Nitatumia pianneno uraibu kumaanisha addiction yaani kuwa teja wa picha za X.
Upatikanaji wa Video na Picha za X
Bishara hii ya picha za x imekuwa kubwa sana kiasi cha matajiri kuwekeza pesa nyingi kutengeneza tovuti zenye maudhui haya. Takwimu zinasema kwamba kufikia mwaka 1997 kulikuwa na tovuti/website 1000 tu zenye video za X. Lakini mpaka mwaka 2015 tayari kulikuwa na zaidi ya tovuti/websites milioni mbili za X.
Watu wanavutiwa zaidi kutizama video za X kwasababu ya urahisi wa kuona maungo ya wanawake ama wanaume wengi kuliko ambavyo ungeona maisha yako yote. Mfano kupitia bando lako tu unaweza kutazama zaidi ya maungo 100 ya wanawake tofauti ndani ya dakika tu. Katika maisha ya kawaida ni vigumu kuwaona wanake 100 wakiwa watupu.
Nini kinatokea mpaka unapata uraibu/Addiction ya picha za X?
Chanzo cha uraibu wa picha za ngono ni kama tu ilivyo kwa uraibu mwingine mfano ule wa dawa za kulevya. Unapoangalia picha na video za ngono, ubongo unatoa kiwango kikubwa cha hormone ya dopamine. Homoni ya dopamine ndio inayokufanya ujisijie raha unapofika kileleni.
Kumbuka ubongo wake hauwezi kutofautisha kitendo cha kupiga punyeto baada ya kutazama picha za X, na kufanya tendo kikawaida. Endapo utafika tu kileleni, ubongo unaamrisha kuhitaji zaidi na zaidi kitendo hicho.
Msisimko wa kimapenzi husababisha utoaji mkubwa wa homoni ya dopamine. Licha ya kukupa furaha na kuhisi utamu, hormone ya dopamine inatengeneza hali ya kutaka tena na tena. Na ndio maana umekuwa muhanga wa kutazama picha za X kila siku.
Tabia hatarishi zinazochochea upende X.
Addiction ama uraibu wa video za X unaanzia kwenye taibia fulani za nje ama za ndani. Mteja hutaka kutazama picha za X ili kutuliza hali yake. Baadhi ya hisia na vitu vinavyokusuka ni pamoja na
- kuboreka
- upweke
- hasira
- hofu na woga
- msongo wa mawazo
- aibu
- kuhisi hupendwi ama huhitajiki
- safari ndefu hasa ukiwa peke yako
- kuachika kwenye mahusiano
- mabadiliko ya ghafla kwenye maisha
- matokeo ya kushtukiza mazuri au mabaya kwenye maisha
- ugumu wa kiuchumi
- mabishano na
- matatizo ya kifamilia
Kama unavyoona kuna vitu vingi sana vinavyoweza kukuchochea ukatazame picha za X mtandaoni. Ni ngumu kuepuka vyote kila muda lakini inawezekana kuepuka uteja wa picha za ngono.
Viashiria vitano kwamba mpenzi ama rafiki yako ameathrika na picha na video za X
1.Mabadiliko ya kitabia na mienendo
Mtu aliyeathirika na picha za X hawezi kujihusisha na kufurahia ipasavyo shuguli za kawaida za kimaisha. Tayari mtu huyu anakuwa na mabadiliko ya mood, mtazamo na hata vitu vya kumsukuma afurahie maisha. Baadhi ya dalili kama kama kuacha baadhi ya mazoea, mfano alikuwa mtu wa mazoezi sasa amesitisha na hata kuacha kujihusisha na marafiki.
2.Wanaficha sana mambo yao na kuwa wasiri
Aibu ya mtu kuwa mraibu wa picha za X zinamsukuma kuwa msiri na mambo yake na kutotaka ndugu kujua. Hii inajumuisha
- usiri kwenye matumizi ya pesa
- kujifungia sana ndani muda mwingi
- kuficha mahali alipo na anachofanya
- kufuta taarifa zake kwenye browser baada ya kutazama X
Watu walioathirika na picha za X hawapendi kabisa simu zao zishikwe. Na wanakuwa wenye hasira sana endapo watagundua mtu kafungua simu za computer zao.
3.Wanajikingia kifua na hawakubali kukosea
Athari ingine ya kuathirika na picha za X ni hali ya kutoa majibu kwa ukali na ovyo pale mpendwa wako anapokuuliza kitu ama kukwambia uache kutazama X. Wengi wa wahanga hujibu kirahisi kwamba hawajaathirika, wanatazama tu kupata raha ya mda mfupi na siyo tatizo kubwa kwao.
4.Hawaachi kutazama picha za X, pamoja na madhara yake
Hichi ndio kiini cha uraibu wowote. Endapo unajaribu kujinasua lakini inakuwa ngumu kupitisha siku bila kuingia mtandaoni kucheki video za utupu hapo kuna shida. Inaonesha tayari umeshakuwa na uraibu/addiction.
Mfano hasa ni pale mahusiano yako yanapovunjika au umefukuzwa kazi kwa kupoteza mda mwingi kuangalia pono badala ya kazi. Endapo imetokea hivo na bado unaendelea kutazama picha za X, maana yake tayari una uraibu.
Wanahitaji muda mrefu au video zaidi za ngono ili kuamsha hisia
Kuangalia pono inaweza kupelekea uchelewe kuashwa kihisia pale unapokutana na mpenzi wako kwenye tendo. Wahanga huhitaji kutazama picha na video zaidi za ngono ili kuwamshwa kuhisia.
Madhara ya kutazama Picha za ngono
1.Athari kwenye afya ya akili
Hili halina walakini kabisa: Picha za pono zinabadili kabisa mwenendo wa ubongo wako. Kadiri unavotazama picha za ngono, ubongo unazoea mazingira mapya ya kusisimua mwili na kuufanya ubongo wako utake zaidi na zaidi.
Ubongo wako utataka zaidi kutazama mikao na style mpya za ngono ambazo hukuwahi kuziona hapo mwanzo. Mfano kama mwanzo ulizoea pono za watu wakiingiliana kwa njia ya kawaida ya uke, utaanza kutafiuta pono za kinyume na maumbile. Ama pono za watu wazima wakiwaingilia watoto wadogo. Ni kama vile ubongo wako unakuwa sugu sasa unataka kitu kipya cha kukata kiu.
Pia mtu aliyeathrika na video za X ana weza kubadilika tabia na kujitenga zaidi na kuchanganya hisia za wasiwasi na hofu kama vile ndio hisia za kuamshwa kingono.
2.Uume kulegea na kushindwa kufanya tendo vizuri
Tafiti zinasema kwamba ongezeko la wanaume wengu kushindwa kusimamisha vizuri na kukosa hamu ya tendo kutokana na picha za x ni kubwa. Athari ya pono kwenye kukwama kwenye tendo la ndoa inachukua mtiririko huu
- Kwanza umejaribu kupiga punyeto baada ya kutazama picha za X na kugundua inachukua muda mrefu kumwaga mbegu.
- Kisha kusimamisha uume vizuri katika uhalisia unapokuwa kwenye tendo na mwenzi wako inakuwa ngumu.
- Unazidi kuangalia pono na unajikuta uume unasimama vizuri zaidi.
- Mwishowe uume unagoma kabisa kusimama hata ukiangalia picha za X tena na tena
Vijana wengi walio katika rika la kubalehe wanakutana na changamoto hizi za kushindwa kufanya tendo kikamilifu baada ya kuathirika na picha za X.
Tafiti zinaonesha endapo utaacha kuangalia Video za X, ubongo wako utajitengeneza kwa namna tofauti na utaanza kusimamisha uume vizuri ukiwa na mwenzi wako.
3.Kuvurugika kwa mahusiano yako
Pono ni mbaya sana kwa mahusiano yako kama ulikuwa hujui. Kukuteka akili yako na kukufanya uendelee kuangalia zaidi na zaidi, wacheza picha za ngono hutumia dawa za kuwafanya wasichoke mapema na kuongeza maumbile.
Kadiri unavoangalia utatamani na mwenzi wako akufanyie hivyo hivo kitu ambacho hakiwezekani. Endapo mwenzi wako hatakufanyia ulivotarajia utatamani kutafuta mwanaume au mwanamke mwingine wa kufanya nae ngono. Hapo tayari utakuwa umemsaliti mwenzi wako na mtafikia kuachana.
Pia kwasababu video za X zinapunguza sana hamu ya kufanya tendo hasa kwa wanaume. Wanaume wengi wanakuwa wateja wa kutazama pono na kusahahu kama wanatakiwa kuwaridhisha wake zao kitandani. Video za ngono zinawafanya kuridhika na kutohitaji tena kufanya tendo.
4.Uraibu wa video za X hupelekea ubaguzi na unyanyasaji wa kingono katika jamii.
Kwa miaka mingi sana imekuwa wazi kwamba upatikanaji wa video za ngono kirahisi unachochea tabia mbaya za unyanyasaji kupitia ngono kama ubakaji. Picha za ngono zinakufanya ubadili mtazamo wako kuhusu tendo la ngono na kujiamini zaidi. Hapo utataka kujaribu kila kitu unachoona kwenye video hizo.
Kwa kuongezea hapo wacheza picha za X hufanya hivo kwa rafu sana bila ustaarabu pamoja nakutumia maneno machafu na matusi ya kutosha wakati wa kurekodi. Video za ngono pia zina matukio ya watoto kufanyishwa ngono kinguvu bila hiyari yao. Hii itakusukuma nawe kwenda kubaka mtoto na kumfanya bila hiyari yake.
Hatua tano za kutibu athari ya kuangalia picha na video za X
1.Amua kuacha kuangalia video za ngono
Kuchomoka kutoka kwenye uraibu wa kutazama picha za ngono inakuhitaji kufuta vyanzo vyote vya video hizi kwenye simu na laptop yako. Nakushauri kutojihusisha na matendo yote ya ngono kwa muda wa miezi walau miwili.
Siyo tu kuatazama picha za X na kupiga punyeto, bali uache kwanza hata kuktana kimwili na mtu ili kusafisha ubongo wako. Kusafisha ubongo wako kutoka kwenye hisia za kimapenzi siyo jambo rahisi lakini inawezekana.
2.Tafuta msaada kwa mtu mwingine wa karibu
Iahitaji ujasiri sana kwa mwanamke au mwanaume kuomba msaada ili kuchana na uraibu wake kuliko kukaa kimya na kuendelea kuteseka. Mweleze rafiki wa karibu au mpenzi wako kwamba unahitaji kuachana na tabia ya kuatazama video za ngono.
3.Onana na mwanasaikojia alieyebobea
Mshauri atakuuliza baadhi ya maswali kuhusu historia yako. Kisha atakupa hatua za kufuata ili kuondokana na uraibu/addiction ya kutazama picha za X.
4. Weka mpango kazi/plan
Mfano unaweza kuamua kununua simu mpya, kisha kujisimamia kwamba katika kifaa hichi kamwe utadownload picha na video za uchi. Kwenye simu au kifaa chako unaweza kuweka safe mode, itasaidia kuchua maudhui kila mara unapoingia mtandaoni ili picha za uchi zisionekane.
5.Kula vizuri, mlo kamili na ufanye mazoezi ya viungo
Kutokana na kwamba wengi huanza kutazama picha na video za ngono baada ya kuwa bored. Tafuta kitu cha kufanya, weka ratiba ya kufanya mazoezi ya viungo kila siku, yatakuweka bize. Kula mlo kamili unaojumuisha aina zote za vyakula kila siku.
Hitimisho
- Tatizo la athari na uraibu wa video za ngono ni kubwa sana na linaathiri ubongo wako
- Kama unaamini mwenzi wako ameathirika na kutazama picha za X, zungumza nae usiogope.
- Kama wewe ndio mwenye tatizo, usiogope kuulizia msaada kutoka kwa rafiki au mwenzi wako
- Kila unapotaka kutazama picha za X, jikumbushe jinsi tabia hii ilivoharibu maisha yako na uandike kwenye notebook yako.
- Futa kila kitu kinachohusiana na X kwenye simu la laptop yako.
- Msaada wa kisaikolojia ni muhimu sana katika kuachana na tabia hii ya kutazama picha na video za X.
9 replies on “Kuacha Kutazama Video na Picha za X”
GOOD
Asante kwa ushauli wako mzuri
karibu na endelea kufatilia makala zetu
Good work
You’re wellcome
Its is so more perfect!
Mapinduzi
Umefanya kazi nzur
Asante