Categories
Magonjwa ya Kuambukiza

Tetekuwanga

tetekuwanga
tetekuwanga

Nini maana ya Tetekuwanga?

Tetekuwanga ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza. Ugonjwa unasababishwa na kirusi anayeitwa varicella-zoster. Watu wengi wanaugua tetekuwanga wakiwa wadogo, endapo hawakupata chanjo.

Mtoto anayeugua tetekuwanga anaweza kumwambukiza mtoto mwingine kwa urahisi sana. Kwa sasa tatizo siyo kubwa ukilinganisha na zamani kwani watoto sasa wanaweza kuachanjwa ili wasipate tetekuwanga.

Huwezi kuugua tetekuwanga mara mbili

Ukishaugua tetekuwanga huwezi tena kuugua maisha yako yote hata kama ukigusana na mgonjwa. Kama hujachanja unaweza kuugua tetekuwanga katika umri wowote ule.

Watu wazima wanaougua tetekuwanga wanakua wadhaifu sana na ugonjwa ukawapelekesha mno ukilinganisha na watoto. Ni bora kuugua tetekuwanga ukiwa mtoto kuliko kuugua ukubwani, au upate chanjo kabisa ili uisugue.

Tetekuwanga inaambukizwaje?

Unaweza kupata tetekuwanga kwa

 • kugusana na mgonwa mwenye tatizo
 • kuvuta hewa ya mgonjwa watetekuwanga au majimaji ya kooni na mafua
 • kugusa majimaji ya mgonjwa kwenye pua zako, mdomo na macho

Je kuna uhusiano gani kati ya tetekuwanga na mkanda wa jeshi?

Ukishaugua tetekuwanga, wale virusi wanabaki mwilini lakini hawasababishi tena tetekuwanga. Lakini siku virusi hawa wakiibuka wataleta ugonjwa mwingine unaoitwa mkanda wa jeshi ama shingles. Kwahivo mkanda wa jeshi hauambukizwi bali ni virusi wako wa tetekuwanga ulougua zamani ndo wanakuletea ugonjwa mpya.

Kumbuka watu wenye mkanda wa jeshi hawawezi kumuambukiza mtu mkdanda wa jeshi, basi wanaweza kumpa tetekuwanga, endapo huyo mtu hakuwahi kuugua tetekuwanga. Mkanda wa jeshi nao huisha wenyewe ndani ya week .

Dalili za tetekuwanga

Dalili za tetekuwanga hazijifichagi, ni rahisi sana kumtambua mgonjwa wa tetekuwanga. Dalili hizi ni kama

 • Homa
 • Kuhisi uchovu
 • kichwa kuuma
 • Maumivu ya tumbo
 • Malengelenge kwenye ngozi yanayowasha na kutoa maji
 • Makovu baada ya lengelenge kutoboka
 • Ngozi yenye madoadoa

Vipimo kugundua uwepo wa tetekuwanga

Kwa kutumia tu macho, muhudumu wa afya anaweza kugundua kwamba unaumwa tetekuwanga.

matibabu na huduma kwa mgonjwa wa tetekuwanga

Nawezaje kumsaidia mwanangu anayeumwa tetekuwanga?
Hakikisha mtoto anapata mda mwingi wa kupumzika na kunywa maji ya kutosha. tetekuwanga huwa inapona yenyewe ndani ya week 1 au mbili. Kumsaidia mtoto na muwasho unaweza kufanya haya

 • weka nguo yenye majimaji baridi kwenye lengelenge
 • hakikisha mwanao yupo eneo lenye ubaridi
 • ongea na mwanao asitoboea lengelenge kama mtoto mdogo sana mkate kucha ili ajijikune
 • unaweza kumpaka lotion maalumu au ukampa dawa zenye kiamabata cha antihistimine- nunua pharmacy
 • mwogeshe mwanao kwa maji baridi mara kwa mara. Mfute mtoto kwa taulo kama unakanda mwili, usifute kwa kusugua.

Usimpe mtoto dawa za asprin. Hizi zinaweza kumletea mtoto shida hasa mwenye homa. Kama huna uhakika dawa ipi ya kumpa mwanao, nenda pharmacy jieleze utapewa dawa sahihi.

Je kuna madhara zaidi yanaweza kutokea kwa mtoto mwenye tetekuwanga?

Changamoto kubwa zinazoweza kujitokeza kutokana na tetekuwanga ni pamoja na

 • bakteria kushambulia ngozi, damu na tishu laini
 • Nimonia- yani mapafu kujaa maji
 • mwili kupungukiwa maji kupita kiasi
 • ini kuathirika
 • damu kuganda

Nani anaweza kuugua zaidi na kulemewa na tetekuwanga?

Watu wenye afya njema, wanapougua tetekuwanga, huwa haiwapelekeshi sana. Japo wa watoto wadogo sana kuugua tetekuwanga inaweza kuwaletea shida zaidi, pia wenye mimba, wenye kinga dhaifu . Wagonjwa wa Ukimwi, saratani na wanapata tiba ya mionzi wanalemewa sana na tetekuwanga

Je tetekuwanga yaweza kuua mtu?

Ni mara chache sana tetekuwanga ikahatarisha maisha ya mtu. Watu wengi hupona mapema ndani ya wiki mbili baada ya kuugua. Japo wapo watu waliowahi kufa kwasababu ya tetekuwanga.

Je mwanangu anaweza kupata chanjo ya tetekuwanga?

Jibu ni ndio kuna chanjo ya tetekuwanga, ongea na mtoa huduma hospital atakupa maelekezo.

Je watu wazima wanaweza kuugua tetekuwanga?

Mtoto akishaugua tetekuwanga, mwili wake unapambana na virusi hao na kutengeneza kinga ya kudumu. Kinga hii inakaa mwilini miaka yote ya uhai wako, na itapambana na virusi wageni wataakaoingia siku zijazo.

Ni lini unatakiwa kumwona daktari?

Nenda hospital haraka endapo mtoto wako anapata dalili za

 • ana malengelenge kwe nye macho
 • kuumwa sana kichwa
  • ana malengelenge makubwa yanayotoa usaha
  • anashindwa kupumua vizuri

  Bofya kusoma kuhusu: kwanini unaugua kaswende sugu

  Leave a Reply

  Your email address will not be published. Required fields are marked *