Namna ya Kulala kwa Mjamzito

Ulale ubavu wa Kushoto Au Kulia?

Pengine wajiuliza namna gani sahihi ya kulala kwa mjamzito? Wakati wa ujauzito madaktari wanapendekeza zaidi ulae kwa ubavu hasa kama mimba yako imeshakuwa kubwa. Hii ni kwasababu ya kuepuka kubinya damu inayozunguka kuelekea kwenye kizazi.

Kulala Kwa Ubavu wa Kushoto

Kulala kwa ubavu wa kushoto inaonekana ni mkao sahihi zaidi kulinganisha na mingine. Kwasababu mkao huu unaruhusu mzunguko mzuri wa damu kutoka wenye moyo wa mama kuelekea kwa mtoto.
Kulala kwa ubavu wa kushoto pia knapunguza mgandamizo kwenye ini na figo. Hii itasaidia kupunguza kuvimba kwa vidole vya mikono , miguu na kwenye enka.

Je ni kweli Kulala Upande flani Ni kigezo cha Jinsia ya Mtoto?

Unaweza kuwa umesikia tetesi kwamba mwanamke akipenda kulalia upande flani basi ni jinsia fulani ya mtoto. Hii ni tetesi tu haina ukweli wowote. Hakuna utafiti wowote unaoonesha ukweli wa jambo hili.

Miezi Mitatu Ya Kwanza Ya Ujauzito(First Trimester)

Kipindi hiki unaruhusiwa kulala kwa namna yoyote, aidha kwa ubavu wa kushoto, kulia, kulalia tumbo au hata mgongo. Lakini kama unataka kujizoesha mapema kwa ajili ya baadae basi anza kulala kwa kuweka mto katikati ya miguu yako. Hii itakusaidia ufurahie usingizi na usipate kashkashi zozote.

Miezi Mitatu Ya katikati ya ujauzito(Second trimester)

Kadiri tumbo linavoongezeka utahitaji kupata godoro imara ambalo halibonyei sana kujizuia mgongo kujikunja sana unapolala. Endelea kutumia mto katikati ya miguu.

Miezi mitatu ya mwisho(Third trimester)

Endelea kutumia mto kukupa sapoti katika miezi hii ya mwisho kuelekea kujifungua. Katika kipindi hiki pendelea zaidi kulala kwa ubavu wa kushoto. Na mara chache lala kwa ubavu wa kulia, hakikisha pia unaweka mto mwingine eneo la kichwa liwe juu kidogo.

Kulala kwa Tumbo ni Salama?

Pengine umekuwa ukijiuliza vipi naweza kulala kwa tumbo nikiwa na mimba na isilete madhara yoyote? Jibu ni ndio unaweza kulala kwa tumbo kwa week 16 za kwanza za mimba. Kadiri mimba inavokuwa kubwa wewe mwenyewe itakushinda kulala na tumbo na itabidi ubadili mkao.

Usiwe na hofu kwamba mimba itaharibika pengine ikitokea kwa bahati mbaya umelala na tumbo. Mtoto analindwa na majimaji ya amniotic fluid kwenye chupa yake.

Kulala kwa Mgongo

Kulala kwa mgongo ni salama ukiwa kwenye miezi mitatu ya mwanzo. Baada ya hapo kulala kwa mgongo itakuwa siyo salama kwani itasababisha upate matatizo ya maumivu chini ya mgongo, bawasili, matatizo ya tumbo na pia damu kutozunguka vizuri inavotakiwa.

Ikitokea mara chache usiku ukajisahau na kulala kwa mgongo basi usiwe na hofu badilisha tu mkao na maisha yaendelee vizuri mpaka ukishajifungua.

Bofya Kusoma: Kuhusu maumivu ya mgongo kwa mjamzito