Kwanini unatokwa na damu baada ya kutoa mimba?
Ni jambo la kawaida kutowa na damu baada ya kutoa mimba. Damu hii inaweza kufanana na ile ya hedhi lakini siyo hedhi. Damu ya abortion ni matokeo ya kubomoka kwa ukuta wa mfuko wa mimba ambao ulibeba kichanga.
Baadhi ya wanawake hawapati bleed kabisa baada ya kutoa mimba. Bleed yao hutoka pamoja na hedhi ya kwanza.
Kwa muda gani utatokwa na damu baada ya kutoa mimba?
Ni kawaida kutokwa damu kwa muda wa wiki moja mpaka mbili baada ya kutoa mimba. Baadhi ya wanawake wanaweza kutokwa damu ikastop kisha baada ya muda ikaendelea kutoka tena.
Damu yatakiwa kuacha kutoka baada ya wii mbili. Baada ya hapo unaweza kuendelea kupata vitone vichache vya damu kwa wiki kadhaa zinazofuata mpaka utakapopata hedhi yako ya kwanza.
Sifa ya damu inayotoka baada ya kutoa mimba
Bleed ya abortion hufanana sana na hedhi, tofauti hasa itakuwa kwenye rangi yake kwani bleed hii inakuwa brown zaidi wakati hedhi huwa imezidi wekundu.
Damu ya abortion huwa nzito zaidi kama ulitoa mimba kwa vidonge badala ya upasuaji.
Baadhi ya sababu zinaweza kuongeza au kupunguza kiwango cha damu ya abortion. Mfano unafanya mazoezi zaidi utapata bleed kubwa tofauti kama ukiwa mtu wa kupumzika zaidi.
Mabonge Ya Damu Iliyoganda
Unaweza kuona pia mabonge ya damu iliyoganda. Hii ni kawaida kabisa na siyo kitu cha kutisha. Mabonge ya damu yanakuwa madongo na mengine makubwa kama limau. Endapo unapata mabonge ya damu yanayotoka mfululizo kwa zaidi ya masaa mawili, unahitaji kwenda hospitali haraka kuonana na daktari.
Uchafu unaoambata na Damu
Utatokwa na uchafu unaoambatana na damu. Uchafu huu unaweza kuwa mlaini unaovutika kama kamasi. Chunguza kama uchafu huu ni wa njano au kijani na unatoa harufu kali. Kama hauna dalili hizi basi kuwa na amani lakini kama una dalili hizi ujue kuna maambukizi na unahitaji dawa.
Dalili zingine utakazopata baada ya kutoa mimba ni pamoja na
- maumivu ya nyonga na kiuno
- kichefuchefu
- kutapika
- homa
- maumivu ya kichwa na
- kuchoka sana
Je Naweza Kutumia Pedi na Tampon Baada ya kutoa Mimba?
Madakatari wanashauri kwamba uepuke kuingiza kitu chochote ndani ya uke baada ya abortion kwa muda wa week mbili. Unaweza kutuma pedi au kitambaa.
Lini Nitapata Hedhi Baada ya kutoa Mimba?
Hedhi yako yaweza kurudi hali ya kawaida ndani ya mwezi mmoja ujao. Kurejea kwa hedhi kunatofautiana kwa kila mwanamke na aina ya utoaji wa mimba uliofanya.
Baada ya kutoa mimba bado hormone za mimba zinaweza kuwepo na hivo kupelekea uchelewe zadi kupata hedhi.
Unaweza kufanya kipimo cha mkojo baada ya mwezi mmoja ukakuta bado inasoma positive. Ni kwamba mimba haipo ila tu hormone hazijashuka. Kama baada ya miezi mwili hujapata hedhi,fanya kipimo cha mkojo kuona kama mimba bado ipo na umuone daktari.
Hedhi ya kwanza baada ya kutoa mimba huchukua siku ngapi?
Hedhi yako ya kwanza inaweza kuchukua siku chache zaidi ulivozoea kama ulitoa mimba kwa upasuaji, na yaweza kutoka kwa siku nyingi kama ulitoa mimba kwa vidonge. Mabadiliko haya ni kutokana na mzunguko kurejea katika hali ya kawaida na pia mabadiliko ya homoni.
Hedhi ya kwanza baada ya Kutoa Mimba ina sifa zipi?
Hedhi yako itakuwa nzito sana kama ulitoa mimba kwa vidonge, kutokana na kubomoka kwa ukuta wa mimba ulioshikilia kiumbe. Utaweza kutokwa na damu iliyoganda pia.
Kama ulitoa mimba kwa upasuaji hedhi ya kwanza yaweza kuwa nyepesi sana, na kurejea hali ya kawaida kwa miezi inayofuata.
Dalili zingine unazoweza kupata kwenye hedhi yako ya kwanza baada ya abortion ni pamoja na
- tumbo kujaa gesi
- maumivu ya kichwa
- matiti kuwa laini sana
- maumivu ya misuli
- mood kubadilika na
- kuchoka sana
Je nikitumia uzazi wa Mpango utaathiri Mpangilio wa hedhi?
Baada ya kutoa mimba unaweza kuamua kutumia uzazi wa mpango ili usishike mimba ingine haraka kutokana na ushauri wa daktari. Njia hizi ni pamoja na sindano, vidonge, kitanzi, njiti na kondomu.
Uzazi kama vidonge vinaweza kufanya hedhi yako ikawa nyepesi sana na kupunguza siku za kutoka hedhi. Njia zingine kama sindano zinaweza kukufanya usipate kabisa hedhi mpaka pale utakapoacha kuchoma.
Je naweza Kushika Mimba tena Baada ya Abortion?
Baada ya kutoa mimba mayai yataanza kupevuka ndani ya week 4. Kwa maana hiyo ni kwamba unaweza kushika mimba mapema zaidi ndani ya mwezi mmoja ukishatoa mimba.
Kutoa mimba kwa kiasi kikubwa kunaathiri kushika mimba ingine. Baadhi ya wanawake kutoa mimba kunaweza kusababisha makovu kwenye kizazi na hivo kushika mimba ingine ikawa mtihani.
Lini Unatakiwa kumwona Daktari
Nenda hospitali haraka endapo
- unatumia pesi zaidi ya mbili kwa masaa mawili
- unapata maumivu makali ya mgongo
- unatokwa na mabonge ya damu makubwa zaidi ya limau
- umetumia dawa za maumivu lakini hujapata nafuu
- una homa kali
- unatokwa na uchafu weye harufu kali
- unatokwa na uchafu wa njano ama wa kijani
Kama umefanyiwa upasuaji kutoa mimba hospitali na hujapata bleed ndani ya masaa 48 muone daktari. Unahitaji pia kumwona daktari kama hedhi yako haitarejea baada ya miezi miwili kupita baada ya abortion.
Tunakushauri utumie vidonge vya UCP kusafisha kizazi
Baada ya kutoa mimba, kizazi kinakuwa kwenye hatari ya kupata maambukizi yaani PID. Maambukizi haya yanaweza kupelekea mirija kuziba na kukukwamisha usishike tena mimba kwa siku za baadae. Pamoja na dawa za hospitali, tunashauri utumie na vidonge hivi asili vya uterus cleansing pills (UCP) kusafisha kizazi. Vidonge havina madhara.
Uterus cleansing pill (UCP) ni vidonge 2 vilivyotengenezwa kitaalamu kwa kuzingatia uasili wa dawa kutatua changamoto za wanawake. Vidonge hivi vinatumika kwa wiki moja. Kidonge kimoja kinawekwa ukeni na kutolewa baada ya siku 3, kisha unapumzika masaa 24,unaweka tena kidonge kingine.
Angalizo
Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge vyenye mfanano na hivi vya UCP, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb
4 replies on “Hedhi baada ya Kutoa mimba”
nimekuelewa sana daktari
Thanks
karibu tena
Asante DAKTARI kwa maelezo yako. lakini bado ninamaswali mawili naomba unisaidie DOKTA. nimesomba baadhi za makala tofauti na hii, zipo makala zinasema baada ya utoaji mimba dalili za mimba kama kichefuchefu au maziwa kuuma zinapaswa kutoweka kwa siku 1, na makala zingine zilisema kwa siku 5. Lakini katika makala yako nimejifunza kuwa umefundisha baada ya utoaji mimba homoni za mimba zinaweza kuchelewa kushuka kwa muda wa mwezi 1. swali: kama homoni zinaweza kuchelewa kushuka kiasi cha mwezi 1 je hizi dalili za mimba kama kichefuchefu au maziwa kuuma haziwezi kuendelea kuwepo mpaka kwa muda huo?
2. nilisoma makala 1 imeeleza baada ya kutoa mimba upo uwezekano wa kusika mimba hata kwa siku 8-10 baada ya kutumia tembe ya kutoa mimba. swali: katika makala yako nimejifunza umeelezea kuwa mayai yataanza kupevushwa baada ya wiki 4 je hawa wataalamu waliolezea kuwa mwanamke anaweza kupata mimba tena hata kwa siku 8-10 baada ya kutumia tembe ya kutoa mimba je mayai upevuka kwa wiki ngapi baada ya kutoa mimba?