Mafuta ya Habbatus Sauda au black seed

Black seed kwa jina la kisayansi ‘Nigella sativa’ ni mmea ulioanza kutumika kwa zaidi ya miaka 2000 iliyopita kutibu changamoto mbalimbali.

Kwa waislamu, mbegu za habbatus sauda au black seed oil yanafahamika kama ‘Habbatul barakah’ ama mbegu ya baraka. Inaaminika kwamba hapo zamani mtume Muhammad aliuchukulia mmea huu kama tiba kwa magonjwa na matatizo yote ukiacha kifo tu.

Faida za Mafuta ya Habbatus sauda ama Black seed

1.Kupambana na fangasi: tafiti za kisayansi zinaonesha kwamba mafuta ya habbatus sauda yanaweza kutibu maambukizi ya fangasi mwilini

2.Kurekebisha kisukari: Tafiti zinasema kwamba mafuta ya habbatus sauda yana uwezo wa kuimarisha uzalishaji wa seli za beta( seli za kwenye kongosho zinazohusika na uzalishaji wa insulini) rejea topic ya kisukari kwa kubofya hapa, na pia mafuta haya yanasaidia kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu (serum glucose level).
Hii inawezekana kutokana na kwamba kiambata cha Nigella sativa ni mojawapo ya viambata vichache duniani vinavyosaidia kuzuia aina ya kwanza ya kisukari na ya pili pia- tafadhali bofya hapa kusoma zaidi kuhusu aina za kisukari
Tafiti pia zinaonesha kwamba black seed inauwezo wa kushusha kisukari kama ilivyo dawa ya metformin ambayo hutolewa hospitali kwa wagonjwa wa kisukari cha ukubwani, wakati huo habbatus sauda/black seed haileti madhara kama ilivyo kwa dawa ya metformin.

Metformin yaweza kuleta madhara kama

  • Tumbo kujaa gesi
  • Kuharisha na kukosa choo ama kupata choo kigumu
  • Maumivu ya kichwa
  • Ladha ya mdomo kuwa mbaya
  • Maumivu ya misuli na
  • Maumivu ya tumbo

    Faida zingine za mafauta ya black seed

    1. Kupunguza hatari ya kuugua saratani, hasa saratani ya utumbo mpana, ini, mapafu, matiti, kizazi, damu na saratani ya kongosho
    2. Kuimarisha mzunguko wa damu: kwa miaka mingi mafuta ya habbatus sauda yametumika kwa ajili ya kurekebisha shinikizo kubwa la damu.
    3. Kuleta nafuu kwa magonjwa mbalimbali ya ngozi: Mafuta ya habbatus sauda ni mazuri kwa afya ya ngozi na hayana kemikali mbaya kama ilivyo kwa mafuta na cream zingine, kama huna aleji na mafuta haya basi ni muhimu ukafikiria kuanza kuyatumia ili ufurahie faida zake.
    4. Kutibu magonjwa ya mfumo wa chakula kama kukosa choo kwa muda mrefu ama kupata choo kigumu na pia kutibu bawasili
    5. Kurekebisha mafuta mwili(cholesterol)

    Je ni Salama kwa kila Mtu Kutumia Mafuta ya Habbatus sauda?

    Mafuta ya habbatus sauda yanaweza kuleta aleji na kusababisha vipele vidogo pale ambapo itatumiwa mdomoni au kwenye ngozi ya nje. Ni jambo zuri kama ukiona dalili mbaya pale unapotumia mafuta haya usitishe kutumia.

    Yanapotumika kwa kumeza tumboni mafuta yanaweza kuleta hali ya kutapika, kichefuchefu na kuvurugika kwa tumbo kwa muda mfupi.
    Kwa mjamzito, mwanamke anayenyonyesha, mgonjwa wa kisukari, presha ama kama upo kwenye dozi muhimu kupata ushauri wa mtaalamu wa tiba asili au daktari kabla ya kutumia mafuta ya black seed.

    Namna ya Kutumia Mafuta haya ya Black Seed

    Matumizi ya mafuta yanatofautiana kulingana na changamoto na mwenendo wa afya yako kiujumla, dozi zifuatazo zimehakikiwa kisayansi na zinafaa kutumika

    Kwa mgonjwa kisukari: tumia kijiko kimoja cha mafuta, unaweza kuchanganya na apple cider vinegar kijiko kimoja kwa ajili ya ladha. tumia kabla ya kula mara mbili kwa siku, kwa miezi 12.

    Kutibu shinikizo kubwa la damu na cholesterol nyingi: tumia nusu kijiko cha mafuta ya habbatus sauda mara mbili kwa siku.

    Kuimarisha uzalishaji wa mbegu za kiume. tumia kijiko kimoja cha mafuta mara mbili kwa siku kwa miezi miwili.

    Kwa mgonjwa wa pumu: Tumia pamba kwa kuchovya kiasi kidogo cha mafuta ya black seed kisha vuta hewa yake puani na upakae kiasi kingine kwenye kifua na koo.

    Kwa mgonjwa wa bawasili na tumbo kiujumla: changanya kijiko kimoja cha mafuta na apple vinegar kizibo kimoja kwenye maji ya uvuguvugu nusu kikombe kisha kunywa nusu saa kabla ya kula

    Tuandikie kwa whatsapp no 0746672914 kupata mafuta original ya hebbatus Sauda kwa Tsh 40,000/=

    Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *