Categories
Uncategorized

Maumivu ya kichwa baada ya tendo

maumivu ya kichwa

Japo inatokea kwa watu wachache sana, unaweza kupata maumivu ya kichwa baada ya kufanya tendo hasa baada ya kufika kileleni. Maumivu haya yanaweza kuisha ndani ya dakika chache ama yakaendelea kwa zaidi ya masaa mawili.

Je maumivu ya kichwa baada ya tendo yakoje?

Maumivu haya (orgasim headache)yanaweza kuanza taratibu kwenye shingo na kichwa kadiri unapopandwa na hisia na kuongezeka kadiri msisimko watendo unavoongezeka. Au maumivu yanaweza kuja kwa haraka na makali sana kwenye eneo la mbele kuzunguka macho, pindi tu ukifika kileleni.

Karibu asilimia 75 ya watu wanaopata maumivu ya kichwa, wanasema yanatokea pande zote za kicha kulia na kushoto.

Je nini chanzo cha tatizo?

Madakatari wanafikiri kwamba maumivu ya kichwa ni kutokana na mishipa midogo ya damu kuvimba (vascular headache). Pale mtu akifika kileleni.

Pale mtu anapofika kileleni, presha ya damu hupanda juu kwa kasi. Kupanda huku kwa presha kunapelekea mishipa midogo ya damu ya kichwa kutanuka haraka na hivo kupelekea maumivu ya kichwa.

Vihatarishi vinavyopelekea maumivu ya kichwa kwenye tendo

Kila mtu anaweza kupata maumivu ya kichwa baada au wakati wa tendo. lakini tafiti zinasema kwamba chansi ya wanaume kupatwa na tatizo ni zaidi ya mara 4 kwa wanawake.

Pia watu walio kwenye umri wa kuanzia miaka 40 na kuendelea wapo kwenye hatari zaidi ya kukutwa na tatizo ukilinganisha na vijana wadogo.

Watu wenye historia ya kuumwa kichwa mara kwa mara kutokana na mwanga mkali au kikohozi pia wanaweza kuumwa kichwa kwenye tendo.

Je maumivu yanaisha kwa muda gani

Kwa kiasi kikubwa maumivu ya kichwa kwenye tendo huisha yenyewe ndani ya dakika chache. Baadhi ya watu hupatwa na maumivu haya mara moja na wengine hupatwa mfululizo katika week au mwezi.

Kama maumivu yatendelea zaidi ya lisaa na yanajirudia mara kwa mara, unatakiwa ummwone daktari. Matibabu ni pamoja na dawa za maumivu kama ibuprofen na dawa za kupunguza presha (beta blockers)

Maumivu ya kichwa baada ya tendo inaweza kuashiria uwepo wa changamoto kubwa ya kiafya. Kwa mazingira hayo unatakiwa kutibu chanzo cha tatizo kwanza.

Lini Unatakiwa Kumwona Daktari?

Siyo kila maumivu ya kichwa kwenye tendo ni ya kawaida. Daktari atakusaidia kujua kama tatizo ni la kawaida ama kuna chanzo kingine cha tatizo. Baadhi ya changamoto zinazoweza kupelelekea upate maumivu ya kichwa kwenye tendo ni pamoja na

 • Maambukizi ya bakteria, fungus au virusi
 • Magonjwa ya moyo
 • Kulegea kwa mshipa wa damu kwenye ubungo
 • Kupungua kwa njia ya mshipa wa damu safi kwenye ubongo
 • Kuvuja kwa damu ndani ya kichwa
 • Kiharusi
 • Matumizi ya baadhi ya dawa kama za kupanga uzazi

Maumivu yasiyo ya kawaida kwa kiasi kikubwa yanaambatana na dalili zingine kama

 • kichefuchefu
 • kutapika
 • shingo kukakamaa na
 • kupoteza fahamu

Watu wanaopata hizi dalili wanatakiwa kupelekwa hospitali haraka

One reply on “Maumivu ya kichwa baada ya tendo”

Sante sana wadau tafuta ushauri nasaha kwa daktar dambay wa magonjwa ya manawake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *