Chanzo cha Mjamzito Kukosa Usingizi

mjamzito kukosa usingizi
mjamzito

Kwa mama mtarajiwa ama mjamzito kukosa usingizi ni kitu cha kawaida sana kutokea hasa katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito. Fahamu kwamba haupo peke yako. Wanawake wengi hupata shida ya usingizi wakati wa ujauzito.

Tatizo hili kitaalamu huitwa insomnia. Hapa chini ni visababishi vya kukosa kwako usingizi pamoja na mambo kadhaa ya kurekebisha ili ufurahie usingizi unapokuwa mjamzito.

Insomnia ni nini?

insomnia ni kitendo cha kukosa kupata usingizi na kushindwa kuendelea kulala wakati ukishapata usingizi. Wajawazito wanakutana sana na changamoto hii katika kipindi chote cha ujauzito wao. Hasa katika miezi mitatu ya mwanzo na miezi mitatu ya mwisho.

Katika kipindi cha mwisho cha ujauzito wanawake wengi hukosa usingizi kutokana na sababu mbalimbali kama ambavyo tunazieleza hapa chini.

Nini Kinasababisha Mjamzito Kukosa Usingizi?

Kuna sababu nyingi zinazokufanya muda mwingi uwe macho usiku mnene ikiwemo

Chanzo kingine cha kukosa usingizi inaweza kuwa msongo wa mawazo na wasiwasi. Pengine unawaza itakuwaje siku ya kujifungua, utawezaje kumlea mtoto atakayezaliwa, namna gani utanyonyesha. Pengine ndugu zako na ndugu wa mume utaishi nao vipi maana sasa unaongeza familia.

Jitahidi kumshirikisha mme wako kuhusu mawazo na fikra ulizonazo itakusaidia kupunguza mzigo wa stress.

Nini Cha Kufanya Ili Upate Usingizi Mtamu

1.Jiwekee ratiba ya kwenda kulala

Moja ya kitu kigumu kwetu ni kupanga ulale muda gani. Kwako mjamzito ili uanze kupata usingizi mzuri inabidi uweke mpangilio wa kwenda kulala muda ule ule kila siku. Yani ukisema saa 4 kamili usiku uwe kitandani basi fanya hivo kila siku bila kukosa.

Acha kutizama TV na kutumia simu na kompyuta lisaa kabla ya kwenda kitandani. Badala ya kuingia instagram au twitter mpaka usingizi ukukute, anza kwa kusoma kitabu kila siku kabla ya kwenda kulala.

Kama unaishi mazingira ya baridi basi haikisha kabla ya kulala unaoga maji ya uvuguvugu. Kama uko maeneo ya joto sana oga maji ya kawaida.

2.Lishe na mazoezi ni Tiba kwa Mjamzito kukosa usingizi

Mazoezi na chakula unachokula na kunywa vina matokeo ya moja kwa moja kwenye usingizi wako. Kunywa maji ya kutosha kila siku, na upunguze kunywa maji ikifika saa 1 jioni. Usitumie kahawa na chai ya rangi kuanzia saa 1 jioni.

Kula kidogo kidogo, yaani katika siku nzima gawanya milo yako hata mara sita. Usile mlo mzito kwa mara moja itakufanya upate kiungulia na kukosa choo.

Kula kidogo zaidi usiku na ujitahidi kabla ya saa 2 usiku uwe umeshakula. Fanya mazoezi kila siku wakati wa mchana, tembea , ogelea au ufanye yoga.

Pata muda wa kupumzika mchana. Lala kwa ubavu, weka mto katikati ya miguu, na tumia mto mwingine kuweka chini ya tumbo lako kadiri mimba inavozidi kuwa kubwa.

3.Fanya Shughuli ndogondogo

Usilale mda wote: Jishugulishe kazi zitakazokufanya uchoke uwe na uhitaji wa kupumzika. Osha vyombo, pika tembea, unaweza kufua pia ukiwa umesimama na kufanya usafi wa nyumba.

Bofya kusoma kuhusu: Kukosa choo kwa mjamzito+ushauri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *