Mafuta ya Mwarobaini

Mwarobaini (Azadirachta indica) ni mti unaopatikana hasa nchini India, Asia na pia bara la Africa. Mwarobaini umekuwa ukipewa sifa nyingi kwa zaidi ya miaka 1000 kutokana na uwezo wake wa kutibu changamoto nyingi za kiafya. Leo fahamu kwamba kuna mafuta ya mwarobaini pia, tutakweleza faida zake hapa.

Karibu kila eneo la mmea wa mwarobaini ni tiba, kuanzia majani, magome yake mpaka maua yake yanatumika viwandani kutengeneza dawa.
Ladha ya mwarobaini ni chungu, na rangi ya mafuta yake inaweza kuwa ya njano ama ya brown kulingana na namna mafuta haya yalivoandaliwa.

Pamoja na kwamba ladha yake ni chungu na harufu yake inaweza isiwe ya kuvutia kulinganisha na mafuta mengine lakini thamani yake katika kukutibu changamoto za kiafya ni kubwa sana.

Faida za mafuta ya Mwarobaoini Kiafya.

  • Kutibu changamoto za ngozi: mafuta ya Mwarobaini yanuwezo wa kupambana na bakteria, virusi, na vimelea wengine wabaya, kwahivo yaweza kutumika kutibu changamoto mbalimbali za ngozi kama chunusi, pumu ya ngozi nk
  • Kuimarisha afya ya nywele na kutibu fangasi kwenye nywele
  • Kupunguza hatari ya kuugua saratani; tafiti zinasema kwamba mafuta ya mwarobaini yanadhibiti ukuaji wa saratani ya mlango wa kizazi (cervical cancer), saratani ya utumbo mpana na saratani ya tezi dume.
  • Kuharakisha uponaji wa vidonda; kwa vidna unaweza kupakaa mafuta ya mwarobaini ili kuzuia kukua kwa bakteria na kupona mapema.

Je Mafuta ya mwarobaini ni salama kwa kila mtu?

Mafuta ya mwarobaini ni salama, lakini yanatakiwa kutumika kwa uangalifu hasa wa makundi ya watu hawa

  • Wagonjwa wa kisukari: mafuta haya yanweza kupunguza sukari kupita kiasi, ni vizuri mgonjwa akafatilia sukari yake mara kwa mara kuona kama kuna mabadiliko makubwa.
  • Wajawazito: matumizi ya mafuta ya mwarobaini kwa mjamazito yanaweza kusabisha mimba kuharibika.
  • Wagonjwa kwenye kundi la autoimmune disease( magonjwa yanayosababishwa na kinga ya mwili kushambulia tishu za mwili)- mafuta ya mwarobaini yanaweza kusababisha kinga yako kushambulia zaidi mwili.

Tuandikie kwa whatsapp no 0746672914 kupata mafuta ya Mwarobaini kwa Tsh 20,000/=

Bofya kusoma kuhusu mafuta ya karafuu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *