Vidonge vya uzazi wa mpango, faida na madhara

vidonge vya uzazi wa mpango
vidonge vya kupanga uzazi

Maamuzi ya aina ya uzazi wa mpango unaotaka kutumia ni jambo binafsi. Japo muhudumu hospitalini atakupa elimu juu ya faida na hasara za kila njia, kazi yako ni kuchagua ipi itakufaa. Kama unafanya tendo la ndoa mara kwa mara, kuna umuhimu wa kutumia vidonge vya uzazi wa mpango ili usishike mimba isiyotarajiwa.

Jinsi vidonge vya uzazi wa mpango vinavyofanya kazi

Vidonge vinafanya kazi kwa namna mbili. Moja vinazuia mayai kupevuka. Hii ina maana mifuko ya mayai haitatoa yai kwenye siku ya hatari, kwahivo hakutakuwa na yai la kurutubishwa na mbegu. Mbili Vidonge vinafanya uteute wa kwenye uke kuwa mzito sana. Ute mzito unazuia mbegu kuogelea na kwenda kurutubisha yai.

Muda gani natakiwa kumeza vidonge

Ni muhimu kuendelea kumeza vidonge kila siku katika muda ule ule. Kupitisha hata masaa machache kunaweza kupelekea mayai yakapevuka na ukashika mimba.

Ufanisi wa vidonge vya uzazi wa mpango ukoje?

Kama vikitumika ipasavyo, vidonge vinafanya kazi vizuri kuzuia mimba. Taasisi ya kudhibiti magonjwa ya Marekeni (CDC) inasema kwamba ufanisi wa vidonge ni asilimia zaidi ya 91.

Baadhi ya matibabu yanaweza kupunguza ufanisi wa dawa za uzazi wa mpango. Matibabu haya ni kama

  • Baadhi ya antibiotics
  • Dawa za Ukimwi kama lopinavir na saquinavir
  • Baadhi ya dawa za kifafa kama carbamazepine na topiramate

Dawa za uzazi wa mpango zinaweza kupunguza ufanisi pia kwa mgonjwa anayetapika na kuharisha. Endapo utakuwa na maumivu ya tumbo, zungumza na daktari akupime kama uko kwenye hatari ya kushika mimba. Unaweza pia kutumia njia nyingine kama kondomu mpaka pale ukishapona.

Zipi ni faida za kutumia vidonge vya uzazi wa mpango.

Faida za vdonge ni pamoja na

  • Kukukinga dhidi ya mimba isiyotarajiwa muda wowote unapofanya tendo
  • Zinasaidia pia krekebisha mzunguko wa hedhi uliovurugika na hedhi nzito
  • Siyo kizuizi cha moja kwa moja kushika mimba. Ukiamua kushika mimba unaacha tu kumeza vidonge.

Pia aina ya vidonge vya uzazi wa mpango(combinationa pills) vinaweza kukukinga dhidi ya

Zipi ni hasara za vidonge vya uzazi wa mpango?

Vidonge vya kuapanga uzazi havitakukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa. Ili kujikinga na magonjwa haya, hakikisha unatumia kondomu.
Hasara ingine ni kwamba yatakiwa kumeza vidonge kila siku. Endapo utavusha hata siku moja tu, kuna hatari ukashika mimba. Hasara na madhara mengine ni pamoja na

  • Maumivu ya kichwa kutokana na kuongezeka kwa homoni ya estrogen
  • Kukosa hamu ya tendo la ndoa
  • matiti kuwa laini sana
  • Kichefuchefu hasa kama umemeza vidonge kabla ya kula
  • Kupata bleed katikati ya mzunguko

Endapo unapata dalili hizi, fahamu kwamba zinaweza kupotea baada ya miezi michache. Kama dalili hazitaisha muhimu uende hospitali na umweleze daktari akubadilishie aina ya vidonge.

Madhara Makubwa

Madhara makubwa ya vidonge vya uzazi wa mpango ni pamoja kuongezeka kwa hatari ya damu kuganda. Tatizo linaloweza kupelekea

  • Damu kutosafiri vizuri kwenye mishipa
  • Shambulizi la moyo
  • Kiharusi na
  • Damu kutosafiri kwenda kwenye mapafu

Usiwe na hofu sana kwasababu hatari ya damu kuganda kutokana na kutumia vidonge vya kupanga uazi ni mdogo sana. Kati ya wanawake 10,000 wanawake 10 ndio wanaweza kuwa kwenye hatari hiyo. Japo hatari ya damu kuganda inaongezeka zaidi kwa wanawake

  • wenye uzito mkubwa na kitambi
  • wanaougua presha ya kupanda na
  • wanaoumwa kulazwa kitandani kwa muda mrefu

Kama hizi taarifa zinakuhusu hakikisha unamweleza daktari mapema kabla ya kuanza kutumia uzazi wa mpango.

Zungumza na Daktari kuhusu Uzazi wa mpango

Kwa sasa kuna njia nyingi sana za kupanga uzazi, na vidonge ni njia moja nzuri sana. Lakini uchaguzi wa aina ya uzazi wa mpango itakayokufaa inategemea na sababu nyingi. Ili kujua njia salama kwa upande wako hakikisha unazungumza na daktari na kumuuliza maswali yote uliyonayo. Maswali haya ni pamoja na

  • Aina gani ya vidonge vya kupanga uzazi vitanifaa?
  • Je dawa zinazotumia zinaweza kuingiliana na vidonge vya kupanga uzazi
  • Je nipo kwenye hatari ya damu kuganda nikimeza vidonge?
  • Kuna njia gani zingine za uzazi wa mpango naweza kuzitumia?

Bofya kusoma zaidi kuhusu maandalizi ya kushika mimba baada ya kutumia uzazi wa mpango

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *