Siku 30 Za Kushika Ujauzito Haraka

kushika ujauzito haraka
mjamzito

Umeshaamua sasa unataka ushike mimba. Hongera sana! Uamuzi wa kushika mimba na kuzaa ili uanze kulea ni mafanikio makubwa sana katika maisha yako. Lakini je mwili waka uko tayari kubeba mimba? Hizi ndizo hatua unazotakiwa kufanya kwa siku 30 zijazo ili kujiandaa kushika ujauzito haraka.

Wiki ya kwanza (siku 1-7)

Siku ya 1: Sitisha kutumia uzazi wa mpango ili kushika ujauzito haraka

Kama unahitaji kushika mimba, itakulazimu kusitisha matumizi ya uzazi wa mpango. Utashika mimba mapema tu baada ya kuacha kutumia njia baadhi za kuzuia mimba kama kondomu, kitanzi na vidonge. Wanawake wengi hushika mimba wiki mbili tu baada ya kuacha uzazi wa mpango.

Baadhi ya wanawake wanaotumia njia zingine za kupanga uzazi kama sindano na njiti, huchukua mpaka miezi mitatu au sita kuweza kushika mimba.

Siku ya 2:Anza kutumia vidonge vya Multivitamin

Ujauzito unahitaji virutubishi vingi sana kukua. Muhimu kujiongezea virutubishi hivi kwa kutumia vidonge vya multivitamin ili kuimarisha ukuaji wa mimba endapo itaingia na kuepusha mimba kuharibika mapema kutokana na kukosa virutubishi.

Siku ya 3:Ongeza na Folic acid

Pamoja na multivitamin, utahitaji kuanza kutumia folic acid kidonge kimoja kila siku. Nenda famasi ya karibu ununue folic acid au folate. Folic acid itasaidia kupunguza hatari ya changamoto za kimaumbile kwa mtoto. Baada ya kushika mimba daktari atakuongezea dozi zaidi ya folic acid.

Siku ya 4. Anza kula mlo kamili kushika ujauzito haraka

Unaweza kupata vitamin na madini mengi kutoka kwenye lishe yako. Anza sasa kula vizuri mpaka wakati wa kujifungua. Katika chakula chako weka makundi yote ya chakula yani protini, mafuta, mboga za majani, matunda na nafaka isiyokobolewa.

Siku ya 5: Weka ratiba ya kuanza mazoezi

Mazoezi ya viungo ni njia nzuri sana ya kujiandaa kushika mimba. tenga walau nusu saa kufanya mazoezi kila siku. Fanya mazoezi ya kukimbia, kuruka kamba, kupanda mlima au kufanya squats.

Siku ya 6:Muone daktari akufanyie vipimo vya kizazi na homoni zako.

Kufanya checkup ni muhimu sana katika kufatilia kama kuna changamoto yoyote ya uzazi, inayoweza kukukwamisha kushika mimba haraka. Mweleze daktari kwamba unajiandaa kushika mimba, atakupa ushauri wa kina.

Siku ya 7:Jiwekee tabia ya kulala masaa 8 kila siku.

Usingizi mzuri utakusaidia kurekebisha homoni zako na kupunguza athari ya msongo wa mawazo. Jiwekee walau masaa 8 ya kulala ukiwa umezima taaa. Jenga tabia ya kupunguza matumizi ya simu na kompyuta nusu saa kabla ya kwenda kulala.

Wiki ya pili(siku ya 8-15)

Siku ya 8: Weka appointment ya kuonana na mtaalamu wa magonjwa ya uzazi

Kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo umri wako, changamoto za uzazi ulizowahi kupata mwanzo nk. Utahitaji kumwona daktari ama specialist wa matatizo ya uzazi.

Baadhi ya maeneo ya kupima ni pamoja na mirija ya uzazi na kucheki mayai kama yanapevuka. Utahitaji pia kupima kama unacmagonjwa ya zinaa

Siku ya 9:Anza kufatilia mzunguko wako kujua siku za hatari

Sasa ni muda wa kuanza kufatilia mwenendo wa mzunguko wako kujua siku za hatari za kushika mimba haraka.

Anza kwa kurekodi lini hedhi yako ilianza na kuisha, kisha lingansha terehe kwa miezi walau mitatu.

Unajuaje siku za hatari kushika ujauzito haraka?

Njia zifuatazo zitakusaidia kujua siku ya ovulation/siku za hatari

  1. Kwa miezi 8 mpaka 12 rekodi siku ambayo unaanza hedhi na uhesabu siku zote za kila mzunguko. Siku ya kwanza ni ile unayoanza hedhi katika mwezi husika na hesabu mpaka siku unayoanza hedhi katika mwezi mwingine hapo mzunguko mmoja utakuwa umekamilika.
  2. Rekodi mzunguko mfupi na mzunguko mrefu zaidi katika ufuatiliaji wako.
  3. Kupata siku yako ya kwanza ya hatari, chukua namba ya mzunguko mfupi zaidi toa 18. Mfano mzunguko wako mfupi ni siku 27-18 inabaki 9.
  4. Kupata siku yako ya mwisho ya hatari kwenye mzunguko, chukua siku za mzunguko wako mrefu toa 11. Mfano mzunguko wako mrefu ilikuwa siku 30-11 inabaki 19.
  5. Katika mahesabu hapo juu ni kwamba siku za katikati ya mzunguko mfupi na mrefu ndizo siku zako za hatari. Kwamaaana ya kwamba siku kati ya 9 na 19 ndizo siku zako za hatari. Kama unataka ushike mimba basi fanya tendo siku ya 9 ya hedhi mpaka siku ya 19.

Siku ya 10:Punguza matumizi ya vitu vyenye kemikali hatarishi

Sumu nyingi zinazoingia mwilini pasipo kujua zinaweza kuwa hatari kwa mimba yako. Jaribu kupunguza sumu hizi kwa

  • Kupunguza matumizi ya marashi yenye kemikali
  • Kupunguza matumizi ya sabuni asii
  • Punguza baadhi ya vipodozi

Fanya haya ukiwa nyumbani

Tengeneza vifaa vyako vya usafi, kwa kutumia maji na apple vinegar badala ya kemikali zenye harufu kali kusafisha chooni na jikoni. Kula vyakula asili ulivyopika wewe nyumbani.
Pendekeza kula chakula fresh badala ya kile cha kwenyye makopo.

Siku ya 11:Jiwekee mazingira ya kupunguza msongo wa mawazo

Jaribu kwa kutumia dakika kadhaa kutembea hasa kwenye sehemu tulivu isiyo na kelele. Mfano kwenye shamba la miti au shamba la maua.

Siku ya 12:Jaribu kuanza kufanya mazoezi ya yoga

Mazoezi ya yoga yana faida nyingi sana kwenye afya ya uzazi. Yoga itakusaidia kuutuliza mwili na kukuondolea hofu na kutuliza hisa zako. Jaribu kutafuta mwalimu wa mazoezi aliye karibu nawe.

Siku ya 13.Muone daktari wa meno(Dentist)

Pamoja na vipimo vingine vya uzazi utakavyofanya, ni muhimu pia upitie kwa mtaalamu wa magonjwa ya meno kufanya checkup. Wakati wa ujauzito mabadiliko ya homoni yanaweza kuathiri afya ya meno yako. Kwahivo ni muhimu kubrashi meno yako mara mbili kwa siku na kuepuka vyakula vya sukari kulinda meno yako.

Siku ya 14. Acha kutuma pombe, tumbaku na dawa kiholela.

Tumbaku, pombe na madawa mbalimbali yanaweza kuathri mtoto tumboni. Vyote hivi vyaweza kusababisha mapungufu kwenye maumbile ya mtoto, mimba kuharibika na mtoto kuzaliwa njiti.

Siku ya 15: Furahia kufanya tendo la ndoa mara kwa mara.

Kama huna changamoto zozote kiafya basi huna haja ya kuvizia siku za hatari. Fanya tendo muda wowote na mara nyingi zaidi, utashika mimba.

Wiki ya tatu(siku ya 16-23)

Siku ya 16: Hakikisha unafatilia uzito wako kwa ukaribu

Uzito mkubwa kwa mjamzito utakuletea matatizo mengi ikiwemo kisukari, presha na kifafa cha mimba. Hakikisha unacheza kwenye uzito unaotakiwa kulingana na urefu wako. Daktari atakushauri wakati unaenda kwa vipimo.

Siku ya 17: Fatilia historia ya afya kifamilia

Mtoto wako atakayezaliwa atarithi baadhi ya sifa na mienendo kutoka kwa wanafamilia ikiwemo mama na baba yako. Hakikisha unafahamu kama kuna magonjwa yoyote ya kurithi kwenye familia yako na familia ya mwenza wako. Endapo utagundua kitu usiache kumshirikisha daktari.

Siku ya 18: Mshirikishe daktari kila dawa unayoamua kutumia

Hakikisha unamweleza daktari kwamba unajiandaa kushika mimba, ili akushauri vizuri matumizi ya dawa zozote au virutubishi unavyotumia kwa muda huo. Baadhi ya dawa siyo salama kwa ujauzito.

Siku ya 19: Ripoti ukatili wowote wa kijinsia unaofanyiwa

Endapo mme wako huwa anakupiga na kukujeruhi mara kwa mara, inaweza kutishia uhai wa mtoto. Hakikisha unaripoti kwenye mamlaka ya karibu nawe endapo unapata unyanyasaji wowote.

Siku ya 20:Fatilia siku za hatari kwa kutumia ovulation kit.

Endapo mzunguko wako haueleweki, yaani umevurugika, unaweza kuamua kutumia vifaa vya kufatilia siku za hatari. Vifaa hivi unaweza kuvipata famasi ya karibu.

Siku ya 21:Punguza matumizi ya caffeine

Caffeine inapatikana zaidi kwenye kahawa, energy drinks na chai ra rangi. Sitisha kutumia vitu hivi na badala yake kunywa maziwa, green tea na juisi ya matunda.

Siku ya 22:Anza kunywa maji ya kutosha

Jiwekee tabia ya kunywa maji mara kwa mara walau glass 8 kwa siku. Utakaposhika mimba utahitaji kuongeza zaidi kiwnago cha maji unachokunywa mpaka lita 3 au 4 kwa siku.

Siku ya 23: Anza kujjisomea makala mbalimbali jinis mimba inaingia

Jinsi Mimba Inavyofanyika iko hivi.

Yai linapokomaa hutolewa kwenye mfuko wa mayai(ovary)ili kurutubishwa,kitendo hiki huitwa ovulation. Kikawaida kila mwezi yai moja hukomaa na kutolewa kwenda wenye mirija ya uzazi lipate kurutubishwa.

Yai linakuwa salama masaa 12 mpaka 36 kusubiri mbegu ije irutubishe. Kama mbegu zinaweza kuishi mpaka siku 5 kwenye kizazi maana yake unaweza ukashika mimba ukifanya tendo la ndoa kwenye siku za mwisho za hedhi. Siku ambazo zinakaribiana na siku za yai kupevuka.

Wiki ya mwisho(siku ya 24-30)

Siku ya 24: Mshauri na mme wako kwenda kupima mbegu na magonjwa mengine.

Japo mimba kwa kiasi kikubwa inabebwa na mwanamke, lakini ni muhimu na mume wako kupimwa pia mbegu. Kwani asili 30 ya sababu zinazopelekea mwanamke kukosa mimba zinasababishwa na mwanaume.

Mshauri mme wkao pia kula vizuri, kufanya mazoezi, kuacha kutumia sigara na pombe. Unaweza kusoma zaidi kwa kubofya hapa kujua kiwango cha mbegu kinachohitajika kutungisha mimba.

Siku ya 25:Tumia virutubisho kuimarisha kinga

Wakati wa mimba kinga yako inaweza kutetereka sana, unaweza kupata mafua na homa za hapa na pale. Unahitaji kujiimarisha kwa kula lishe nzuri na kutumia vitamin C.

Siku ya 26:Jifunze vitu gani vya kufanya na vitu vya kuepuka

Haikisha unawekeza muda mwingi kusoma tafiti za kiafya kujua vitu gani vya kufanya na vya kuepuka wakati wa ujauzito.

Siku ya 27: Kuwa mwangalifu kwenye kazi zako

Baadhi ya shuguli kama unyanyua vitu vizito na kusimama kwa muda mrefu siyo salama kwa ujauzito. Unahitaji kujua hili mapema uanze kujijengea tabia wakati unajiandaa kushika mimba.

Siku ya 28: Fanya vitu unavyovipenda mapema

Wakati wa ujazito kuna michezo hutaweza kufanya mfano kupanda mlima, kuruka kamba na kukimbia mwendo mrefu . Fanya hivi vitu mapema kabla hujshaika mimba.

Siku ya 29: Fuatilia bima yako ya afya

Bima ya afya itakusaidia kupata matibabu hata kama huna pesa wakati unaumwa. Tazama bima yako kama itaweza kulipia matibabu yoyote ikiwemo kama itahitajika kuazaa kwa upasuaji. Hakikisha pia bima yako imelipimwa mapema.

Siku ya 30: Imarisha mawasiliano na mwenzi wako.

Wote mnatakiwa kuwa kitu kimoja wakati huu wa kutafuta mtoto. Inaweza kuchukua miezi mingi zaidi kushika mimba kuliko ulivyopangilia. Kuwa muwazi kwa mpenzi wako kutasaidia yeye kukupa ushirikiano muda wote hata kama itahitajika vipimo zaidi.

7 replies on “Siku 30 Za Kushika Ujauzito Haraka”

mimba huwezi kujua kama imeingia baada ya tendo, ni mpaka usubiri hehdi ijayo kama utavusha basi ukapime. na kujua umri wa mimba ni mpaka ukafanye utrasound hospitali

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *