Nini Chanzo Cha Matiti Kuvimba

matiti kuvimba,mwonekano
mwonekano wa matiti

Nini Kinasababisha matiti kuvimba na kuwa Mazito sana? Ni kawaida kwa matiti kubadilika katika mzunguko wako wa hedhi. Lakini ni muhimu kuwa mfatiliaji mzuri kwani urembo wako upo kwenye matiti.

Endapo titi moja likikatwa kwa sababu ya ugonjwa inaweza kukuharibia shape yako nzuri. Kama matiti yako unaona kabisa yamekuwa mazito kupita kiasi basi hakikisha unaenda hospitali mapema kwani waweza kuwa na changamoto mojawapo kati ya hapa chini

Uvimbe Usio Saratani Kwenye titi(Fibrocytic breast)

Nusu ya wanawake wote duniani wanaweza kupatwa na tatizo hili katika kipindi fulani kwenye maisha yao. Uvimbe huu usio saratani unaweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye matiti yako, kama kujaa maji kwa tishu za matiti na kisha kufanya matiti kuwa mazito kuliko kawaida.

Dalili zingine za kukuonesha kwamba una uvimbe kweye titi ni pamoja na

  • maumivu na matiti kuwa laini sana kuliko inavotokea wakati wa hedhi
  • maumivu ya matiti yanayosambaa mpaka kwenye kwapa na kwenye mikono
  • kutokea na kupotea kwa nundu kwenye titi, ambazo zinabadilika ukubwa kila mara
  • kutokwa na majimaji ya kijani au kijivu kwenye matiti.

Matiti Kuvimba na Kuwa Mazito kwa Sababu ya Hedhi

Kutokana na mabadiliko ya homoni kuu mbili estrogen na progesterone,tishu za kwenye matiti zinaweza kuongezeka ukubwa.

Mabadiliko pia ya homoni hizi yanaweza kupelekea maji mengi kuhifadhiwa kwenye matiti na kufanya matiti kuwa mazito. Dalili zingine kwenye matiti wakati wa hedhi ni pamoja na

  • chuchu kuwa laini na zenye msisimko mkubwa
  • kuvimba matiti na
  • maumivu yanayosambaa mpaka kwenye kwapa

Kuvimba Matiti Kutokana na Mimba

Matiti kuvimba na kujaa ni dalili moja wapo ya mimba, na matiti huanza kuvimba week moja au mbili baada ya kushika mimba. Kuvimba huku hutokana na mabadiliko ya homoni. Matiti huvimba, kusisimka zaidi na pia kuwa malaini sana kuliko kawaida.

Kama matiti yako yamevimba na unaona kabisa umeshapitiliza hedhi basi kuna haja ya kuchukua kipimo cha UPT na kupima mkjo wako, maana yaweza kuwa ni mimba.

Dalili zingine za mimba changa ni pamoja na

  • kupitisha hedhi
  • kupata matone ya damu
  • mwili kuchoka sana
  • kizunguzungu na kutapika.

Kama mimba ipo kweli basi matiti yako yataendelea kukua na kuwa mazito zaidi kukuandaa kwa ajili ya kunyonyesha mtoto atakayezaliwa

Matiti Kuvimba na Kuongezeka Ukubwa wakati wa Kunyonyesha

Kunyonyesha mtoto ni changamoto sana. Bilashaka wewe kama mama umeshakutana na changamoto ya maziwa kutoka kwa wingi kupita kiasi na chuchu kuuma sana. Maziwa yanapokuwa mengi sana matiti hujaa zaidi na kuwa mzito.

Dalili unazoweza uzipata endapo maziwa ni mengi sana ni pamoja na

  • matiti kuwa magumu sana
  • matiti kuwa ya moto
  • wekundu kwenye matiti
  • chuchu kuwa flati
  • homa kwa mbali

Matiti Kuvimba Kutokana na Matumizi ya Dawa

Baadhi ya dawa zinaweza kupelekea matiti yako kuongezeka na kuwa mazito sana. Dawa hizi ni pamoja na vidonge vya uzazi wa mpango, dawa za uzazi na tiba za kurekebisha homoni.

Baadhi ya dawa za kupunguza msongo wa mawazo pia zaweza kubadili uwiano wa homoni na hivo kufanya matiti kuvimba na kuwa mazito sana.

Maambukizi Kwenye Matiti

Kitaalamu mastitis, maambukizi haya yanatokea sana kwa wanawake wengi wanaonyonyesha. Maambukizi haya yaweza kusababisha matiti kuvimba na kuwa mazito zaidi.

Mastitis hutokea pale maziwa yanapoziba mrija wa kupitisha maziwa na kupelekea bakteria wabaya kukua. Baadhi ya dalili kwamba umepata maambukizi haya ni pamoja na

  • matiti kuwa laini sana
  • kuvimba kwa matiti
  • maumivu makali hasa wakati wa kunyonyesha
  • kupata nundu kwenye titi
  • kupata homa na matiti kuwa na wekundu

Saratani Ya Matiti

Pamoja na kwamba saratani ya matiti inatokea kwa wanawake wachache zaidi, watakiwa kuchukua tahadhari pale unapoona dalili za tofauti. Dalili hizi ni kama

  • titi kuwa jekundu kwa zaidi ya nusu
  • ngozi ya titi kuwa ya njao kama ganda la chungwa
  • chuchu kuzama ndani
  • titi kubonyea ndani ya kuchelewa kurudi juu(dimple)

Je Ni Muda Gani Natakiwa Kumwona Daktari?

Ni jambo la kawaida matiti yako kubadilika na kuwa mazito. Lakini kumbuka ni muhimu sana kuwa na tabia ya kufanya vipimo vya matiti mara kwa mara. Kama una hofu kwamba matiti yako hayapo kawaida basi yatakiwa kwenda hospitali haraka.
Fuatilia mabadiliko ya matiti yako kila mara ili kugundua kama kuvimba ni kwa kawaida ama ni dalili mbaya.

Bofya kusoma kuhusu: Matiti kutoa maji maji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *