Chanzo cha Kuvimba Mapumbu na kujaa maji

kuvimba mapumbu
kuvimba korodani

Kuvimba mapumbu yaweza kutokea baada ya ajali au changamoto kubwa ya kiafya. Inaweza kusababishwa ia na kujaa maji kwneye mfuko wa mapumbu au kukua kwa seli kupita kiasi.

Uvimbe huu kwa lugha rahisi huitwa busha, unaweza kuleta maumivu makali sana ama usiume. Endapo unapata maumivu makali, unahitaji kufika hospitali mapema upate tiba. Kwani waweza kupoteza korodani zako na usiweze tena kumpa mwanamke mimba.

Nini kinasababisha kuvimba mapumbu?

Kitendo cha kuvimba mapumbu kinaweza kujtokeza haraka sana au kikawa cha taratibu kwa muda. Moja ya chanzo kikubwa cha kuvimba kwa mapumbu ni kujinyonga kwa korodani.

Korodani zinajinyonga kutokana na ajali ama kitendo chochote kinasopelekea kupungua mzunguko wa damu kwenye korodani. Kujikunja na kujinyonga kwa mapumbu ni hatari sana na inaweza kupelekea kupoteza korodani.

Baadhi ya magonjwa yanaweza kupelekea kujinyonga kwa korodani. Magonjwa haya ni kama

  • saratani ya korodani
  • ngiri
  • kukua kupita kiasi kwa mishipa ya mapumbu
  • maji kwenye mapumbu
  • maambukizi kwenye mirija ya mapumbu
  • magonjwa ya moyo na
  • maambukizi kwenye ngozi ya mapumbu

Dalili za kuvimba mapumbu

Dalili kubwa unayoweza kuiona ni kuongezeka kwa mfuko unaobeba korodani kuliko kawaida. Viashiria vingine hutegemea na chanzo cha tatizo lako kama maumivu makali na uwepo wa nundu kwenye korodani. Muone daktari mapema endapo utaona dalili hizi

Kujua chanzo cha mapumbu kuvimba

Muhimu unapoenda kumuona daktari, hakikisha unamweleza daktari dalili zote unazozipata. Mjulishe daktari kama mapumbu yanauma na ya uvimbe kwa ndani. Baada ya daktari kukusanya taarifa zako, atapendekeza vipimo vya kukufanyia.

Vipimo hivi vitajumuisha kukutazama kwa macho na kushikashika pumbu zako. Pia kama daktari akiona inafaa, anaweza kupendekeza ufanyiwe utrasound kuona eneo la ndani la mapumbu.

Tiba ya hospitali kwa mapumbu yaliyovimba

Tiba ya tatizo hili la kuvimba kwa mapumbu, inategemea na chanzo cha tatizo. Kama chanzo ni maambukuzi ya bakteria, daktari atakupatia antibiotics kupambana na bakeria wabaya. Daktari pia anaweza kukupatia dawa zikusaidie kupunguza maumivu na uvimbe.

Upasuaji utahitajika endapo mshipa wa damu umevimba, hernia ama maji yamejaa kwenye mapumbu. Kama chanzo ni saratani ya mapumbu, tiba yake itategemea na hatua ya ugonjwa na aina ya saratani. Tiba za saratani hujumuisha upasuaji kuondoa korodani, tiba ya mionzi (radiotherapy) na dawa(chemotherapy).

Huduma ya kwanza ya nyumbani kupunguza maumivu

  1. Tumia kipande cha barafu kifunge kwenye kitambaa na ukiweke kwenye mapumbu|
  2. Tumia dawa za maumivu famasi
  3. Punguza mazoezi makali na shuguli nzito

Kumbuka hatuna dawa kwa changamoto hii: Muhimu nenda hospital ukapime na kupata dawa.

Bofya kusoma kuhusu: Chanzo cha uume kulegea na kushindwa kumudu tendo