Njia salama za kuacha kunyonyesha

kuacha kunyonyesha
kunyonyesha

Kumwachisha mtoto ziwa inachukua muda hasa kama mtoto amshazoea kunyonya kwa kipindi kirefu. Hatua zitakusaidia kuacha kunyonyesha kwa urahisi na pia zitamsaidia mama na mtoto kubadili ratiba ya unyonyeshaji kuelekea kwenye kuacha kunyonyesha.

1.Tambua lini unataka kuacha kunyonyesha.

Wanawake hawatakiwi kuacha kunyosha kipindi ambacho hawapo tayari, na pia haitakiwi kuendelea kunyonyesha wakati hawataki.

Wizara ya afya inatependekeza mama kunyonyesha kwa miezi 6 mfululizo bila kumpa mtoto chakula kingine chochote. Mtoto aanzishiwe chakula baada ya kutimiza umri wa miezi 6. Baada ya hapo mama aendelee kunyonyesha kwa mwaka mmoja na zaidi kama wote mama na mtoto watapenda.

Wakati mwingine wanawake humwachisha mtoto ziwa kutokana na maumivu ya matiti, matiti kuvimba na hata maneno ya ndugu na marafiki, ama hofu kwamba mtoto hapati chakula cha kutosha. Endapo unapenda kuendelea kunyonyesha na una changamoto kwenye matiti, muone daktari mapema.

2.Hakikisha unapata lishe ya kutosha

Wanawake wanaoachisha mtoto kunyonya chini ya mwaka mmoja, wanahitaji kumpa mtoto formula yenye virutubisho vua kutosha kuimarisha ukuaji wake.

Watoto wa umri wa zaidi ya miezi 6 bado pia wanahitaji formula au maziwa ya mama mwingine, lakini pia wanaweza kuanzishiwa chakula kigumu. Mtoto chini ya umri wa mwaka mmoja hatatakiwi kupewa maziwa ya ngombe au soya milk.

Watoto wanaoanza kula , wanatakiwa kupata virutubishi vingi vya protini, madini chuma na vitamin.

3.Epuka vitu vinavyokuondolea utulivu

Baadhi ya watoto huacha kunyonya kirahisi, na wengine huwa wagumu sana kuacha titi la mama. Kwenda taratibu itasaidia kupunguza athari kwa mama na mtoto pia.

Jaribu kuchagua kipindi ambacho hauko bize ili kumwachisha mtoto ziwa. Kama inawezekana tenga muda wa kuwa na mtoto mara nyingi, kwani anaweza kuwa na wasiwasi kama vile utamuacha mbali.

4.Usinyonyeshe nyakati za usiku

Watoto wengi wa umri miezi 6 mpaka mwaka mmoja wananyonya kidogo sana nyakati za usiku. Kumpuzisha mtoto kunyonya usiku kutakusaidia wewe kama mama kupata muda wa kupumzika.

5.Punguza vipindi vya kumnyonyesha mtoto taratibu

Inaweza kuwa changamoto sana kumwachisha mtoto kwa mara moja, kufanya hivo kutapelekea matiti kuvimba na kuuma chuchu. Pia kuacha haraka inaweza kupelekea kuathirika kisaikolojia kwa mama na mtoto. Njia nzuri ni kuacha kunyonyesha taratibu kwa kupunguza vipindi vya kunyonyesha.

Anza kwa nyakati ambazo siyo za muhimu sana kumnyonyesha mtoto, hasa wakati wa usiku. Vusha siku moja kisha subiri siku zingine tatu na uvushe tena na tena mpaka mtoto azoeee.

Baada ya hapo nyakati zilizobaki za asubuhi na jioni huwa ngumu sana kwa mama kuacha kunyonyesha. Anza kuvusha vipindi vya asubuhi na kunyonyesha jioni tu. Kisha nyakati zinazofuata mtoto mwenyewe ataacha kunyonya.

6.Tumia pump ya kukamua maziwa

Kunyonyesha ni kitendo kinachotegemea upatikaji wa maziwa na uhitaji wa maziwa. Endapo mtoto anahitaji zaidi maziwa, maana yake yatakiwa yazalishwe mengi na itakubidi kupup maziwa mengi zaidi kumtosheleza mtoto.

Mtoto asipopata chakula cha kutosha, atahitaji maziwa mengi zaidi. Unapokamua maziwa mengi kwa wakati mmoja unachochea mwili uzalishe maziwa zaidi na zaidi. Njia salama ya kuepuka hilo ni kwa kukamua maziwa kidogo kidogo katika muda fulani.

Mtoto anaponyonya anasisimua chuchu na kufanya mwili uzalishe maziwa zaidi na zaidi. Kumpa mtoto maziwa kwa kukamua kunasaidia kupunguza uzalishaji wa maziwa na hivo kurahisisha kitendo cha kumwachisha mtoto.

7.Shugulika na kuvimba kwa matiti

Kunyonyesha kwa njia ya kawaida na hata kukamua maziwa yaweza kupelekea maziwa kuuma na kuvimba. Kurekebisha changamoto hizi wakati unataka kumwachisha mtoto ziwa, jaribu hatua hizi

  • weka jani la kabeji kwenye kila titi kabla ya kuvaa bra kwa muda wa masaa mawili
  • kanda ziwa kwa maji ya uvuguvugu kabla ya kumyonyesha mtoto
  • fanya masaji kwenye matiti mara kwa mara
  • zungumza na daktari akuanzishie vidonge vya kupanga uzazi, vinasaidia kwa baadhi ya wanawake

8.Fahamu nyakati za hatari

Kumwachisha mtoto kunyonya huambatana na changamoto nyingi. Hatari mojawapo ni kupata maambukizi kwenye matiti na afya ya mtoto kuzorota.

Baadhi ya wamama kupata msongo wa mawazo na wasiwasi, na baadhi ya watoto hupata shida ya kuzoea maisha bila nyonyo. Muone daktari endapo

  • mama atapata homa
  • maziwa yatavimba, kuwa na wekundu na kuwa ya moto
  • kutokwa na majimaji ya kijani ama yenye harufu kwenye matiti
  • mama ana dalili za sonona na wasiwasi
  • mtoto anapata changamoto ya usingizi

9.Mtulize mtoto

Kunyoyesha mtoto ni zaidi ya kumpa virutubishi. Ni kitendo kinachomuunganisha mama na mtoto, na mtoto kuhisi yuko salama na kulindwa. Watoto wengi hupata raha na kusinzia wakati wa kunyonya.
Chukua hatua hizi kumtuliza mtoto

  • mkumbatie mtoto na ngozi yako ikutane na ngozi yake
  • mfundishe kuimba au kucheza pale anapohitaji nyonyo
  • mzoeshe namna mpya ya kulala ili apate usingizi vizuri

Kumjali mtoto itasaidia sana kumtuliza asiwe mpweke. Unapojaribu kumwachisha mtoto nyonyo anaweza kutaka kwa nguvu kunyonya. Unaweza kutafuta msaidizi katika kumuhudumia mtoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *