Jinsi Ya Kuvaa Kondomu

kondomu ya kiume
kondomu

Kondomu ni mpira laini mwembamba unaovalishwa kwenye uume kwa kondomu ya kiume ama kuingizwa ukeni kwa kondomu ya kike kabla ya tendo la ndoa.

Kondomu ikitumika kwa usahihi inazuia kupata mimba isiyotarajiwa na kukukinga na magonjwa ya zinaa. Mpira wa kondomu inakukinga kwa kuzuia majimaji yenye mbegu ama ya ukeni kugusa sehemu zako za siri.

Usitumie kondomu ya kike na ya kiume kwa pamoja, yani katika tendo la moja haitakiwi kwa mwanamke kuvaa kondomu ya kike na mwanaume kuvaa kondomu ya kiume, haitafanya kazi. Ni mtu mmoja tu atakiwa kuvaa kondomu.

Kondomu inaukinga vizuri dhidi ya magonjwa ya ngono kama ukimwi, homa ya ini na kisonono

Namna ya kutumia kondomu kwa usahihi

Kondomu ya kiume

  1. Kwa uangalifu fungua pakiti ya kondomu kwa kukata kidogo eneo la juu, hakikisha kucha zako ziwe fupi.
  2. Weka kwenye uume, kama bado hujatahiriwa kunja kwanza govi ndipo uvae kondomu
  3. Binya mwishoni kwa kondomu ili kutoa upepo
  4. Kunjua kondomu taratibu mpaka kwenye shina la uume
  5. Baada ya tendo kunja tena kondomu irudi kama ilivokuwa mwanzo na kuitoa kwenye uume.
  6. Tupa kondomu mahali ambapo watoto hawatafikia.

Matumizi ya kondomu ya kike

kondomu ya kike
kondomu ya kike
  1. Taratibu fungua pakiti yenye kondomu kisha itoe
  2. Jiweke vizuri ili kondomu iingie, unaweza kulala kitandani, ukaweka mguu mmoja kwenye kiti ama ukachuchumaa.
  3. Hakikisha ringi ndogo ya ndani ya kondo iko chini kabisa mwa kondomu
  4. Isokomeze kondomu taratibu ukeni kwa kidole, hakikisha inaingia ndani kabisa mpaka kwenye mlango wa kizazi.
  5. Kwa kutumia mkono wako shika uume wa mpenzi wako kisha uingize taratibu kupita kwenye mdomo wa kondomu
  6. Baada ya kumaliza tendo fanya kama unatwist kondomu kwa kushika ringi kubwa ya juu na uivute kisha itupe mbali na watoto.

Mambo muhimu ya kuzingatia unapotumia Kondomu ya Kiume

  • hakikisha usitoboe kondomu pale unapishika
  • angalia muda wa expiry kama tayari imepita muda wa matumizi itupe
  • tumia kondomu moja kwa kila mshindo, yani kila baada ya kumwaga vaa kondomu ingine
  • vaa kondomu muda wote mpaka utakapomaliza tendo
  • wakati wa tendo kama kondomu itapasuka, acha mara moja kufanya tendo, jisafishe kisha vaa kondomu ingine
  • unapovua kondomu fanya hivo taratibu, hakikisha mbegu hazimwagiki

Maswali Yanayoulizwa Mara Kwa Mara Kuhusu Kondomu

Je naweza kuhifadhi kondomu kwenye waleti yangu?
Jibu ni hapana. Kondomu yahitaji kuhifadhiwa mahali pakavu penye joto la wastani. Kuweka kwenye waleti inaweza kusababisha kondomu kuharibika.

Je kondomu inafaa kwa size zote za uume?
Jibu ni hapana, kila mwanaume ana urefu wake wa uume. Lakini watengenezaji wa bidhaa hii muhimu wamehakikisha wanatengeneza size ya kati inayofaa kwa kila mwanaume.

Isipokuwa kwa wanaume wachache wenye maumbile madogo zaidi au maumbile makubwa zaidi. Kama upo kundi hili usiogope kwenda famasi na kumweleza muuzaji kama maumbile yako madogo sana ama makubwa zaidi ili akupe kondomu itakayokufaa ufurahie tendo.

Makala inayofuata: Kondomu ya kike na jinsi ya kuvaa

13 replies on “Jinsi Ya Kuvaa Kondomu”

hiv jaman huu ugojw wa vvu tutauepukaje maana kam ni kondom kazi yake nikuzuia mimba isiingie na je endapo unahitaj mimb utafanyaje ili usipatwe na HIV duuh kazi ipo

Dah! Nyie watu siye tulio oa na mlio olewa ni kutulia na mwenzi wako tu ndani mnafanya mnavo taka bila mashariti kama mlisha chek afya mkaambiwa mko sawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *