Tiba asili ya upungufu wa damu+Kuongeza damu kwa Lishe

upungufu wa damu na lishe ya kuongeza damu
seli za damu

Anemia ama kwa lungha rahisi upungufu wa damu, ni pale mgonjwa anapokuwa na kiwango kidogo cha seli nyekundu za damu, ama akawa na upungu wa haemoglobin kwenye seli zake. Upungufu wa damu hupelekea dalili mbaya kwa mgonjwa kama kizunguzungu, mwili kukosa nguvu na changamoto ya kupumua.

Damu yetu imetengenezwa seli nyeupe na seli nyekundu za damu. Seli nyeupe hufanya kazi ya kulinda mwili dhidi ya magonjwa. Seli nyekundu za damu zinabeba kampaundi zinazoitwa haemoglobin ambazo hubeba na kusambaza hewa ya oksijeni kupitia damu kwenda maeneo mbali mbali ya damu.

Nini kinasababisha Upungufu wa damu?

Hedhi nzito, upungufu wa madini chuma, ujauzito, na majeraha makubwa ni sababu ya upungufu wa damu. Lakini pia tatizo la kurithi la sickle cell anemia ni chanzo cha upungufu wa damu, ambapo mtu anazaliwa na seli nyekundu zisizo na uwezo wa kusafirisha oksijeni.

Tiba asili za kuongeza damu ukiwa nyumbani kwako

1.Spinach

Spinach ni moja ya mboga nzuri sana wenye kuongeza damu mwilini. Japo kiwango cha madini chuma kilichopo kwenye spinach hakifonzwi vizuri na mwili mpaka pale ukichanganya na mboga zingine kama broccoli na viazi mviringo.

2.Beetroot

Beetroot ni moja ya chanzo kikubwa cha madini chuma . Wekundu wake uliokolea ni kiashiria na wingi wa madini chuma. Japo ile ladha yake kwa wengi kumeza juisi yake ni changamoto sana. Kufurahia ladha ya beetroot hakikisha unakamulia limau ndani yake, au blend pamoja na apple bichi.

3.Machungwa

Machungwa ni chanzo kizuri sana na Vitamin C na madini chuma. Glass moja ya juisi ya machungwa kwa siku itakutosha kukupa kiwango cha madini chuma kinachohitajika.

4.Apple

Rojo ya matunda ya apple inashauriwa kutumiwa sana na waoto wanaoanza kula baada ya ile miezi sita ya kunyonyesha bila kumpa chakula. Matunda haya yana kiwnago kikubwa cha madini chuma na pia kambakamba.

Ushauri mwingine kwa Mwenye upungufu wa damu

Usitumie vyakula vya namna hii siyo salama kama

  1. soda na vitu vinavyofanana na hivyo,
  2. vyakula na vinywaji vyenye sukari iliyongezwa hasa kutoka viwandani,
  3. wanga iliyosafishwa , na
  4. kahawa na chai nyeusi; vitu hivyo vinapunguza ufyonzaji ya madini ya chuma ambayo ni muhimu kuongeza damu mwilini.

Mgonjwa mwenye upunfu wa damu atumie kwa wingi vyakula vyenye madini ya chuma kama maini (kuku, mbuzi , ngome), nyama nyekundu, vitunguu maji, karoti, na tunda la parachichi

3 replies on “Tiba asili ya upungufu wa damu+Kuongeza damu kwa Lishe”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *