Nywele Kukatika Baada Ya Kujifungua.

nywele kukatika
nywele kukatika

Wanawake wengi pale wanapokuwa wajwazito nywele zinakuwa nzuri na za kuvutia. Lakini baada tu ya kuzaa, mambo yanabadilika na meza inapinduka. Nywele zinaanza kunyonyoka na kukatika, nini shida?

Hapa chini nitaeleza kwanini nywele zinakatika na hatua gani uchukue ili kutunza nywele zako baada ya kujifungua.

Namna mabadiliko ya homoni yanavyochangia nywele kukatika

Homoni ama vichocheo ni sababu kubwa inayopelekea mabadiliko kwenye nywele zako baada ya kujifungua.

Kipindi cha ujauzito, kiwango cha homoni ya estrogen kinakuwa juu na kufanya nywele zako kunawiri vizuri na kupendeza. Kuongezeka kwa mzunguko wa damu nyakati za mimba inachangia nywele kukua vizuri na kupunguza nywele kunyonyoka.

Baada ya kuzaa nywele zinaanza kukatika

Sasa baada ya kuzaa, homoni nyingi hushuka sana, nywele zinaanza tena kupukutika kwa mafungu. Nywele hizi zinaweza kuanza kukatika muda wowote baada ya kuzaa, na zoezi laweza kuendelea mpaka mwaka mzima.

Tiba ya nywele kukatika baada ya kujifungua

Kumbuka ni kawaida nywele zako kukatika baada ya kuzaa. Hili linawatokea wanawake wote, usiogope chochote maana haupo peke yako. Kuna baadhi ya mambo waweza kufanya ili kutunza nywele zako nyakati hizi.

Njia asili za kutunza nywele zako.

Habari njema ni kwamba kuna mambo kadhaa waweza kubadili kwenye maisha yako hasa kwenye lishe, na kusaidia nywele zako zikue vizuri, hasa baada ya ile miezi mi4 ya mwanzo ya kunyonyesha.

Vyakula muhimu vya kula mara kwa mara kutibu nywele kukatika

1.Vyakula asili: hii ni formula namba moja unapojaribu kukuza nywele zako na kuzina zisikatike. Pendelea kula vyakula asili ambavyo umeandaa mwenyewe nyumbani, visivyo na kemikali hatarishi.

2.Mbegu za maboga-mbegu hizi zina madini ya zinc ya kutosha, ambayo ni muhimu sana kwa nywele zako. Nunua mbegu zako sokoni, zioshe kisha zikaange kwa chunvi kidogo na moto mdogo anza kutafuna.

3.Samaki wa maji baridi: Hawa wana omega 3 kwa wingi ambayo inasapoti ukuaji wa nweyle zako. unaweza pia kujaibu kirutubisho chetu chenye omega 3 kwa wingi.

4.Green tea- green tea, inachochea mwili kutoa sumu na kuimarisha ukuaji wa nywele.

5.Kula zaidi mbegu: mbegu kama chia zina kambakamba kwa wingi na zinasaidia ukuaji wa nywele

6.Caffeine: tafiti zinaonesha vyakula vyenye caffeine vinachochea ukuaji wa nywele. Vyakula hivi ni pamoja na kahawa na chocolate. Lakini tumia kwa kiwango kidogo sana

Acha kutumia vyakula hivi

1.Vyakula vyenye mafuta mabaya: Mfano ni mafuta ya margarine, mafuta yote ya kupikia yaliyoganda mafuta ya soy na mafuta yaliyochemshwa sana.

2.Sukari: Sukari inakuja katika amna nyingi, inaweza kuwa ya mezani ama sukari iliyoongezwa kwenye vyakula viwandani. Sukari zote hizi ni za kuwa nazo makini kwani zinachangia upotevu wa nywele zako.

3.Pombe:Pombe zinaongeza sumu mwilini na kuathiri ini na hivo kupelekea nywele kukatika. KUvuta sigara pia inachangia tatizo.

4.Vyakula vilivyosindkwa: vyakula hivi vingi vimetengenezwa kwa mafuta mabaya ama vina sukari iliyoongezwa ambayo siyo salama

Mafuta: Essential oils za kuchochea nywele zako kurefuka

Rosemary oil ni mafuta mazuri sana kwenye kuimarisha nywele zako. Mafuta ya rosemary yanaaminika kuchochea ukuaji wa seli za nywele na hivo kufanya nywele zako kurudia urembo wa zamani.

Mafuta ya lavender na peppermint: ili upate faida vizuri ya mafuta haya fanya hivi: Chukua matone kidogo ya lavender, rosemary na peppermint changanya na mafuta mengine mengine ya nazi au ya mzeituni kisha paka kwenye nywele zako mara 2 mpaka 3 kwa siku.

Kupata faida vizuri ya mafuta haya, hakikisha unanunua yale original, kutoka kwenye chanzo cha kuaminika. Kama utayakosa mtaani kwako unaweza kupata kutoka kwetu. Tayari tulishafanya utafiti na kupata mzalishaji wa kuaminika.

Utapata aina zote tatu za mafuta haya yani rosemary, lavender na peppermint kwenye ofisi zetu hapa mwembechai kwa tsh 50,000/= Tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254.