Faida na Hasara za Kufunga Kizazi

Kufunga kizazi kwa mwanamke na mwanume ni mojawapo ya njia permanent za kupanga uzazi . Kuna njia nyingi za kupanga uzazi ili mwanamke asishike mimba mapema wakati ambao hajajiandaa kushika mimba. Baadhi ya njia kama kondomu zitakusaidia pia kuzuia usipate magonjwa ya zinaa.

Kufunga kizazi(sterilization) ni njia ya uzazi wa mpango ambao ukifanyiwa hutaweza tena kuzaa moja kwa moja. Kumbuka kwamba njia hii haikuzuii usipatwe na magonjwa ya zinaa.

Mwanaume na mwanamke wote wanaweza kufunga kizazi. Kwa mwanaume njia hii kitaalamu huitwa vasectomy na kwa mwanammke ni tubal ligation.

Kufunga Kizazi kwa Mwanamke

kufunga kizazi mwanamke
kizazi

Kwa mwanamke kufunga kizazi hufanyika kwa upasuaji wa kukatwa, kufungwa, au kuzibwa kwa mirija yote ya uzazi. Kitendo hichi kinalenga kuzuia yai lililopevuka kukutana na mbegu.

Taratibu za Kufunga Kizazi Hospitali

Unapofika hospitali manesi watakuandaa na utachomwa sindano ya nusu kaputi. Utakatwa matundu madogo mawili kwenye eneo la tumbo, kisha kifaa kidogo huitwa laparoscope kinaingizwa kupitia matobo haya.

Kwa kutumia kifaa vingine vidongo utakatwa mirija kufugwa ama kuzibwa na kushonwa eneo la tumbo lililokatwa.

Baada ya masaa machache utakuwa sawa na waweza kurudi nyumbani. Kitendo hichi cha kufunga kizazi unaweza kuamua kufanyiwa wakati wa kujifungua. Ongea na mme wako mkubaliane juu ya jambo hili kwasababu hutaweza kushika tena mimba.

Kufunga Kizazi Kwa Mwanaume

kufunga kizazi kwa mwanaume
vasectomy

Kwa mwanaume kitendo hiki huitwa vasectomy. Ni upasuaji rahisi na salama kabisa kukata mirija inayobeba mbegu kutoka kwenye kiwanda cha kuzalisha mbegu(mapumbu).

Upasuaji huu hautakuzia wewe mwanaume kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa. Bado kutakuwa na majimaji yatakayotoka wakati wa kumwaga, ila tu majimaji haya hayatakuwa na mbegu.

Namna Kitendo kinavyofanyika Hospitali

Kwa kiasi kikubwa upasuaji huu hufanyika hospitali huku muhusika akiwa yuko macho pasipo nusu kaputi. Tundu dogo hutobolewa katika eneo la juu la mapumbu, chini ya uume kisha mishipa inayobeba mbegu(vas deferens) inakatwa na kufungwa kwa kutumia vifaa tiba. Baada ya upasuaji utaruhusiwa kurudi nyumbani baada ya masaa machache.

Maisha Baada Ya kufunga kizazi Kwa Mwanaume

Baada ya upasuaji unaweza kuwa mchovu kwa siku chache ila baadae utakuwa vizuri kabisa na utaendelea na kazi zako. Unahitaji kupumzika walau siku moja ama mbili. Wanaume wengi huanza kufanya kazi ndani ya week moja wakishafanyiwa upasuaji.

Je Unaweza Kufanya Tendo na kufurahia Baada ya Kufunga Kizazi?

Jibu ni ndio, utaanza kufanya tendo la ndoa ndani ya week moja baada ya kupona upasuaji. Muhimu endelea kutumia kinga kuzuia mimba mpaka pale utakapofanyiwa kipimo kuhakiki kama mbegu hazipo tena kwenye shahawa.

Nini hasara za Kufunga Kizazi Kwa Mwanaume?

Ubaya pekee wa kitendo hichi ni kwamba huwezi kurudi kawaida baada ya upasuaji. Ni kitendo cha moja kwa moja hata ikitokea umebadili mawazo yako hutaweza tena kumpa mwanamke mimba.

Na ndio maana madaktari wanashauri kitendo hiki kifanyike tu kwa wanaume wenye uhakika kwamba hawatahitaji kupata tena mtoto kwa siku za baadae.

Soma makala inayofuata kuhusu: Kitanzi na njia zingine za kupanga uzazi