Kama mwanamke unaweza kuwa unanjiuliza kama ni salama kufanya tendo la ndoa wakati wa ujauzito ama siyo salama.
Pengine unafikiri yaweza kupekea mimba kuharibika? Au mtoto kupata majeraha? Pengine wajiuliza kuna staili fulani za tendo ambazo ni salama zaidi kwa mjamzito? Hapa chini ni taarifa muhimu ambazo watakiwa kuzifahamu.
Je Kufanya Tendo la Ndoa Wakati wa Ujamzito Ni Salama?
Jibu ni ndio, kufanya tendo wakati wa ujauzito ni salama kabisa. Uume kuingia ndani ya uke,zile pilika za kuingiza na kutoa haziwezi kuathiri mtoto, kwa sababu analindwa na tumbo na misuli ya ukuta wa kizazi pia.
Lakini pia mtoto analindwa na majimaji mazito(amniotic fluid).
Usijali kuhusu kusinyaa na kutanuka kwa uke pale unapofikia kilele, hakuwezi kufanya mimba ikatoka. Kutanuka huku ni tofauti na wakati wa kuzaa.
Mazingira gani inashauriwa usifanye tendo la ndoa wakati wa ujauzito?
Daktari anaweza kushauri usifanye tendo la ndoa kama
- una historia ya mimba kuharibika mara kwa mara
- uko kwenye hatari ya kupata uchungu mapema kabla ya week 37 za ujauzito
- unatokwa na damu na maumivu yasijulikana sababu yake
- chupa imepasuka na maji yanavuja
- mlango wa kizazi umefunguka mapema zaidi
- una tatizo kitaalamu placenta previa yani tishu za mirija unaomlisha mtoto chakula na hewa safi, umekuwa mpaka kuziba mlango wa kizazi
- kama unatarajia kujifungua watoto mapacha
Je naruhusiwa kupiga punyeto badala ya tendo?
Fahamu kwamba daktari akishauri usifanye tendo anamanisha pia usifanye kitu chochote ambacho kinakuamsha hisia na kukufikisha kileleni mfano kutumia dildo an vidole/ kupiga punyeto.
Hamu ya Tendo la Ndoa wakati wa Ujauzito
Kila mwanamke mwanamke mjamzito anatofautiana namna anavojisikia kuhusu tendo. Baadhi hamu ya tendo hupotea kabisa. Wengine hufurahia zaidi tendo na kupata msisimko zaidi wa mapenzi wakati huu.
Kipindi cha ujauzito ni kawaida kwa hamu ya tendo kubadilika. Muhimu zungumza na mpenzi wako namna unavojisikia. Mueleze unapenda staili ipi nzuri ya kufanya tendo isiyokuumiza.
Staili za Kufanya Tendo Kwa Mjamzito
Baada ya miezi minne ya mimba,usifanye tendo kwa njia ya kawaida ya baba na mama kwa kulala kitandani na mme wako akaja kwa juu. Itakusaidia kuepuka changamoto za mzunguko wa damu..
Staili nzuri ya kufanya tendo ni kwa wote kulala kwa ubavu. Kisha mwanaume akaingiza uume kwenye uke kupitia nyuma yako na pia dogie style,yani mwanamke kupiga magoti na mwanamume kuingiza uume kwa nyuma.
Kama huna uhakika na mwanaume unayekutana nae kipindi hiki cha ujauzito basi hakikisha anavaa kondomu. Kuwa na mimba haizuii kutoambukizwa magonjwa ya zinaa kama ukimwi, kisonono na chlamydia-maana maambukizi haya huathiri mtoto moja kwa moja.
Tendo la Ndoa Baada Ya Kujifungua
Kwa week 6 za mwanzo baada ya kujifungua inashauriwa usifanye tendo la ndoa. Sababu zikiwa unahitaji:-
- kupona kidonda wendapo njia ya uke ilikatwa kidogo kuongeza mlango wa mtoto kutoka
- kupona kidonda cha tumbo endapo kama ulijifungua kwa upasuaji
- uchovu kutokana na kujifungua
- mabadiliko ya homoni yatapelekea ukose hamu ya tendo kwa muda
- baaada ya kuzaa ni kawaida kuendelea kupata bleed kwa week 4 mpaka 6
- Stress kutokana na kuwaza sana kuhusu majukumu mapya kama mzazi
Kwa ujumla tendo la ndoa lifanyike baada ya mama kupona kabisa. Ongea na daktari wako akupe ushauri lini itakuwa sawa. Kwa kiasi kikubwa week 6 zinafaa kusubiri kabla ya kuanza tena tendo la ndoa. Muhimu hakikisha tu una utulivu kihisia na kimwili kabla ya kuanza .
6 replies on “Tendo la Ndoa wakati wa Ujauzito”
Safi sana
Mbona mtu hutoa vitu za white ambazo ziko ka maziwa wakati wa ujauzito?
Ni hali ya uke kujisafisha, kama inaambatana na muwasho yaweza kuashiria fungus, hapo chukua hatua ya kwenda hospitali mapema
thank you
kwanini mwanamke akisikiya hamu yatendo majiyanatokaga?
Thanks