Saratani ya mapafu

saratani ya mapafu
saratani ya mapafu

Ni zipi dalili za awali za saratani ya mapafu?

Dalili za mwanzo kabisa za saratani ya mapafu ni pamoja na

  • kukohoa makohozi mazito au damu
  • maumivu ya kifua yanayoongezeka zaidi unapopumua, kucheka au kukohoa
  • pumzi kukata
  • kukoroma
  • mwili kuchoka sana na kukosa nguvu
  • kukosa hamu ya kula na uzito kupungua ghafla

Pia mgonjwa wa saratani ya mapafu atapata maambukizi ya mara kwa mara kwenye njia ya hewa kama nimonia.

Saratani ikisambaa

Endapo saratani itasambaa, baadhi ya dalili zinatongezeka kwa kulingana na kiungo kilichoathiriwa, nfano

  • kuvimba kwa mtoki, kwenye shingo
  • maumivu ya mifupa hasa kwenye mbavu, mgongo na hips
  • maumivu ya kichwa, mikojo na miguu kukosa nguvu na kukosa balance
  • ngozi na macho kuwa ya njano, endapo saratani imesambaa kwenye ini.

Vimbe za saratani zilizo juu ya mapafu zinaweza kuathiri seli za neva za macho, na kupelekea kushuka kwa kope za upande mmojawapo. Kupungua kwa mboni ya jicho, na upande mmoja wa uso kushindwa kutoa jasho.

Uvimbe pia unaweza kukandamiza mshipa mkubwa unaorudisha damu kutoka kwenye kichwa, mikono, kuipeleka kwenye moyo. Hii itasababisha kuvimba kwa uso, shingo na mikono pia.

Dalili za mabadiliko ya homoni

Saratani ya mapafu wakati mwingine huzalisha vichocheo sawa na homoni, na hivo kuletekeza dalili nyingi ikiwemo

  • misuli kulegea
  • kichefuchefu
  • kutapika
  • mwili kujaa maji
  • kupanda kwa shinikizo la damu
  • sukari kuongezeka kwenye damu
  • kupoteza fahamu mara kwa mara na
  • kushindwa kufanya maamuzi

Nini kinasababisha saratani ya mapafu?

Kila mtu anaweza kuugua saratani ya mapafu. ila wavutaji wa sigara wapo kwenye hatari zaidi ya kuugua.

Athari za moshi wa sigara

Pale tu unapovuta moshi wa sigara, mapafu yako yanaanza kuharibika. Kikawaida mapafu yanaweza kurekebisha athari ndogo iliyojitokeza, lakini kadiri unavyorudia tena na tena kuingiza moshi inafikia kipindi mapafu yanalemewa.

Kemikali hatarishi na mionzi

Kufanya kazi kwenye mazingira yenye gesi ya radon, ni chanzo kikuu cha pili kinachopeleka watu kuugua kansa ya mapafu.

Matibabu ya mionzi kwenye kifua: Tiba yoyote ya mionzi kwenye kifua mfano X-ray ama Ct sca ya kujirudia, inaweza kupelekea seli za mwili kubadilika kuwa seli za saratani.

Kuvuta moshi wa sigara kutokwa kwa mvutaji: Hata kama huvuti sigara, kitendo cha kuvuta moshi wa sigara inakuweka kwenye hatari ya kuugua saratani ya mapafu. Unaweza kuvuta moshi wa sigara bila kutegeea ukiwa nyumbani, kazini,bar au kwenye mgahawa..

Kemikali zingine zinazopelekea kukua kwa seli za saratani ni pamoja na

  • arsenic
  • cadmium
  • nickel
  • uranium

Tabia hatarishi zinazopekelea saratani ya mapafu

Kihatarishi kikubwa ni kuvuta vilevi vya moshi, ikijumuisha, sigara na cigar. Bidhaa za tumbaku zimejaa kemikali sumu nyingi sana.

Kwa mujibu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na magonjwa ya marekani, wavuta sigara wapo kwenye hatari mara 5 mpaka 30 zaidi kupata saratani ya mapafu kuliko wasovuta sigara. Unavovuta sigara kwa muda mrefu zaidi ndipo hatari inaongezeka zaidi

Kuvuta hewa yenye moshi wa sigara ni kihatarishi kingine.

Pia kufanya kazi kwenye mazingira yenye kemikali hatarishi kama tulivoorodhesha pale juu.

Vipimo kugundua saratani ya mapafu

Baada ya daktari kukuchunguza kwa macho na kuchukua taarifa za dalili unazopata, atakujulisha kujiandaa na vipimo kama

Vipimo vya picha ya ndani ya kifua: Vipimo hivi ni x-ray, MRI na CT scan. Vipimo vitaweza kugundua endapo kuna uvimbe wowote usio wa kaiwada kwenye mapafu yako.

Sputum cytology: kama unatoa makohozi unapokohoa, daktari atachukua sampuli ya makohozi na kupeleka maabara kwa vipimo zaidi.

Pia daktari atachukua sampuli ya nyama kwenye mapafu na kupeleka maabara. Vipimo vitatoa uhakika kama kweli uvimbe ni wa saratani.

Hatua za ukuaji wa saratani ya mapafu

Stage za saratani kwa madaraja, ni kuonesha kwa kiasi gani saratani imesambaa kwenye mwili. Uwezekano wa kupona saratani yako unategemea ni mapema kiasi gani umechunguzwa na kuanza tiba. Hii ni kwasababu saratani ya mapafu huanza kuleta dalili ikiwa tayari imesambaa.

Saratani ya mapafu ina hatua kuu nne ambazo ni

  1. Stage 1: Kansa/saratani imepatikana kwenye mapafu lakini bado hajisambaa nje ya mapafu
  2. Stage 2: Saratani ipo kwenye mapafu na imeanza kusambaa kwenye tezi za karibu za kutoa taka/ lymph nodes
  3. Stage 3: Saratani ipo kwenye mapafu, kwenye tezi za kutoa taka na kwenye mapafu na pia katikato ya mapafu
  4. Stage 3A: Saratani ipo kwenye mapafu na kwenye tezi lakini kwenye pafu moja pekee ambako ilianzia
  5. Stage 3B: Saratani imesambaa kwenye tezi za kutoa taka za kwenye pafu la pili naeneo la juu karibu na mfupa wa kola.
  6. Stage 4: Saratani imesambaa kwenye mapafu, na kwenye viungo vya karibu na mapafu.

Matibabu ya saratani ya mapafu

Ni muhimu sana kufanya vipimo sehemu tatu tofauti kabla ya kuanza tiba ya saratani yoyote ile. Jopo la wataalamu likijumuisha, mtaalamu wa mionzi, daktari bingwa wa saratani, daktari bingwa wa magonjwa ya mapafu na daktari wa upasuaji watakushauri juu ya tiba yako.

Tiba ya saratani itategemea na ukubwa wa tatizo lako, na tiba yaweza kutofautiana kwa kila mgonjwa. Tiba hizi zinajumuisha

  • Upasuaji kuondoa sehemu ya mapafu yenye seli za saratani ama pafu lote.
  • Tiba ya moinzi kuharibu na kuua seli za saratani
  • Tiba ya pamoja yani upasuaji , dawa chemotherapy na mionzi/ radiotherapy.

Soma zaidi kuhusu lishe ya mgonjwa wa saratani hapa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *