Hatua za Kupunguza uzito Baada ya Kujifungua

kupunguza uzito baada ya kujifungua
kupunguza uzito

Kupunguza uzito baada ya kujifungua ni jambo gumu na linaloleta stress sana kwa wanawake wengi. Kila mmoja wetu anapenda kuwa na uzito wa kawaida ili kufurahia maisha na kutoogopa kuvaa nguo yoyote.

Uzito mkubwa na kitambi hasa baada ya kuzaa unakera sana na kukupunguzuia urembo wako. Najua unahitaji kupunguza uzito na kurudi kwenye shape yako ya zamani kabla hujashika mimba.

Usiwe na hofu haupo peke yako, tumefanya utafiti na kukuletea maelezo ya kuzingatia ili upunguze uzito na uanze kufurahia maisha kama zamani.

Wanawake Huongezeka unene wakati wa Ujauzito

Zaidi ya nusu wya wanawake wenye mimba huongezeka uzito zaidi kuliko kiwango kinachohitajika wakati wa ujauzito. Uzito mkubwa na kitambi unasababisha madhara zaidi kwa mjamzito ikiwemo

  • hatari ya kuugua kisukari na presha
  • kupata matatizo wakati wa kujifungua na
  • kifafa cha mimba

Hatua za kufuata ili upunguze Uzito baada ya kujifungua

1.Jiwekee malengo

Unataka kupungua kilo ngapi baada ya muda gani? lazima uandike kwenye daftari ama notebok yako, bila hivyo ni ngumu kufikia mafanikio. Mfano unataka kupungua kilo 20 ndani ya miezi mi4, maana yake ukivunja vunja malengo yako unatakiwa upungue kilo 5 kila mwezi.

Ukishajiwekea malengo, andika na mikakati ya kuchukua ili kufikia lengo la kila mwezi, kisha anza mara moja kutimiza.

2.Usijinyime kula baada ya kujifungua

Wakati huu ambao mtoto wako anahitaji zaidi maziwa ya mama, usinjinyime kula. Ukifanya hivo utamkosesha mtoto virutibishi vya muhimu. Badala yake chagua ule vitu gani na usile vitu gani. Punguza kula vyakula vya wanga na sukari, badala yake kula zaidi vyakula vyenye protini na mafuta mazuri.

3.Mnyonyeshe mtoto inavotakiwa

Shirika la afya duniani linapendekeza mtoto anyonye kwa miezi 6 bila kupewa chakula kingine chochote. Kunyonyesha mtoto kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu itakusaidia sana afya yako na ya mtoto pia kwa kumpa mtoto virutubishi vya kutosha.

Virutibishi hivi husaidia kuimarisha kinga ya mtoto dhidi ya maambukizi ya fangasi na bakteria, kupunguza hatari ya mtoto kuugua magonjwa ya utotoni kama pumu na kupunguza hatari ya mama kupata saratani ya matiti, kisukari, presha na uzito mkubwa

Miezi mitatu ya mwanzo ya kunyonyesha unaweza usione mabadiliko katika kupunguza uzito wako, usikate tamaa endelea kunyonyesha zaidi utaona matokeo.

4.Kula kwa wingi vyakula vyenye kambakamba(fiber)

Kwenye shopping yako ongeza vyakula vya nafaka ambavyo havijakobolewa na mboga za majani kwa wingi. Vyakula vyenye kambakamba kwa wingi vinapunguza kasi ya uchakataji chakula tumboni na hivo kukufanya usiwe mtu wa kula kula kila mara.

5.Ongeza na vyakula vya protini kwa wingi baada ya kujifungua

Vyakula vya protini vinaimarisha shughuli za mwili, kupunguza njaa na hivo kupunguza kiwango cha chakula unachotakiwa kula katika siku.

Tafiti zinasema kwamba mwili unatumia nguvu kubwa zaidi kuchakata protini kuliko aina zingine za chakula. Kwa mantiki hiyo mwili utachoma zaidi mafuta yaliyohifadhiwa mwili kupata nishati ya kuchakata chakula, na kupelekea upungue uzito bila kutumia nguvu nyingi.

Vyanzo vya protini ni pamoja na nyama ya ngombe au mbuzi, nyama ya kuku, mayai, samaki , karanga, mbegu na maziwa.

6.Epuka Sukari iliyoongezwa kwenye vinywaji na vyakula vya kusindikwa

Sukari iliyoongwezwa kwenye vyakula unavyovipenda zaidi kama baga, mandazi, mikate, sosage,pombe, icecream , keki na energy drinks,vinakufanya uendelee kunenepa zaidi. Epuka vyakula hivi na uanze kula chakula ulichopika wewe nyumbani.

Usitumie tena vyakula vya kwenye makopo au pakiti. Nenda mwenyewe sokoni fanya shopping, rudi nyumabani pika chakula chako upike ule.

Weka ratiba ya kufanya mazoezi

Kabla ya kuanza mazoezi ongea na daktari ni muda gani unafaa kuanza kufanya mazoezi hasa kama ulijifungua kwa upasuaji. Mazoezi yatakusaidia kuchoma mafuta mengi zaidi yaliyohifadhiwa mwilini.

8.Pata usingizi wa kutosha baada ya kujifungua

Kila siku pata muda mzuri wa kulala usiku masaa 8 au 9. Itakusaidia kuweka sawa homoni zako ili uweze kupungua kiurahisi. Baada ya kujifungua ongeza wafanyakazi wa nyumbani kukusaidia kubeba mtoto na kufua ili muda mwingi upate kupumzika.

Bofya kusoma makala inayofuata kuhusu: Faida za hasara za uzazi wa mpango

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *