Kukojoa kitandani, maelezo, ushauri na Tiba

kujikojolea na kukojoa kitandani
kitanda

Utangulizi

Kukojoa kitandani ni pale mtu anaposhindwa kubana mkojo na kudhibiti kibofu cha mkojo hasa nyakati za usiku. Hali inayopelekea mkojo kujikojolea bila hiyari yake. Kukojoa kitandani inaweza kuwa kitu cha kukera na aibu sana, hasa kama unachangia kitanda au chumba na watu wengine.

Kukojoa kitandani wa watoto ni jambo la kawaida kabisa, ni hatua mojawapo katika ukuaji wa viungo vya mtoto. Japo kwa watu wazima inaweza kuashiria tatizo kubwa la kiafya. Karibu asilimia mbili ya watu wazima wana shida ya kukojoa kitandani, kutokana na tatizo la kiafya lenye kuhitaji tiba ya hospitali.

Nini kinapelekea kukojoa kitandani?

Changamoto za kimwili pamoja na za kisailojia zinaweza kupelekea ushindwe kujizuia kukojoa usiku. Vyanzo vikubwa kwa watoto na watu wazima ni pamoja na

Kuvurugika homoni na kujikojolea kitandani

Kuvurugika kwa homoni pia yanaweza kuchangia kukojoa kitandani. Kikawaida mwili wa kila binadamu huzalisha homoni ya antidiutretic hormone (ADH). Kazi ya ADH ni kupunguza uzalishaji wa mkojo nyakati za usiku. Mkojo unapokuwa kidogo, kibofu kinaweza kuhifadhi mpaka asubuhi unapoamka kukojoa.

Watu wenye kiwango kidogo cha ADH hupata mkojo mwingi usiku na kibofu kushindwa kushikilia mkojo mpka kuachia.

Kisukari ni moja ya ugonjwa unaochangia kukojoa kitandani. Kama una kisukari, mwili wako unashindwa kudhibiti kuongezeka kwa sukari kwenye damu na hivo kuzalisha mkojo mwingi. Mkojo mwingi hupelekea mtu ashindwe kushikilia na kukojoa kitandani.

Mazingira hatarishi yanayopelekea kukojoa kitandani

Jinsia ya mtu pamoja na kurithi vinasaba ni vitu vinavyochangia tatizo la kukojoa kitandani kwa watoto. Watoto wa kike kwa wa kiume hupata hali ya kujikojolea katika umri wao wa utoto. Hasa umri wa miaka 3 mpaka 5. Upo pia uwezekano wa mtoto wa kiume kuendelea kukojoa zaidi ya umri huu.

Historia ya familia pia inachangia. Mtoto yupo kwenye hatari ya kupata tatizo la kujikojolea endapo wazazi wake au ndugu zake wa damu waliwahi kuugua tatizo kama hilo. Uwezekano ni mkubwa zaidi ya asilimia 70 endapo wazazi wote wawili walikuwa na tatizo hilo.

Tiba ya kukojoa kitandani

Mabadiliko ya mtindo wa maisha kudhibiti tatizo la kujikojolea

Kwenye kutibu tatizo, ni muhimu kuanzia kwenye kurekebisha baadhi ya tabia kwenye mtindo wako wa maisha. Kwa watu wazima anza kwa kupunguza kiwango cha maji unayokunywa usiku. Jaribu kujizuia kunywa maji mengi masaa matatu kabla ya kwenda kulala. Hii itafanya kibofu cha mkojo kuwa tupu kuelekea mda wa kulala.

Kunywa maji yako katika siku kabla ya chakula cha usiku. Kumbuka usipunguze maji unayokunywa katika siku nzima ila punguza kunywa nyakati za jioni. Kwa watoto hii njia inaweza isisaidie.

Jaribu kuacha kunywa vinywaji vyenye caffeine kama chai ya rangi, soda, kahawa, energy drink na pombe nyakati za usiku. Kabla ya kulala hakikisha unaenda haja ndogo, itasaidia kupunguza mkojo kwenye kibofu.

Mazoezi ya Kegel kwa mtu mzima

Mazoezi ya kegel yanasaidia kuimarisha misuli ya nyonga. Hasa kama tatizo lako la kujikojolea linatokana na kulegea kwa misuli ya uke na kibofu.

Muda msuli wa kufanya zoezi hili ni pale unapoenda haja ndogo. Wakati wa kukojoa ndipo unaweza kutumia misuli inayotakiwa. Kama utafanikiwa kubana misuli sahihi wakati unakojoa na ukagundua mabadiliko kwenye speed ya mkojo basi hapo umepatia zoezi.

Wakati unakojoa bana misuli ya ndani ili kuzuia mkojo usitoke. Bana mkojo wa sekunde 10 kisha uachie kwa sekunde kadhaa bana tena kisha achia. Mwanzo utakuwa mgumu lakini usikate tamaa endelea kufanya mpaka upatie zoezi. Usifanye kila muda unapoenda kukojoa ila jitahidi ufanye mara 4 kwa siku. Kama ilivo kwa mazoezi mengine, unavofanya zaidi kila siku unapata uzoefu na ndivyo unazopatia zaidi.

Kujikojolea kwa watoto

Pilika za mtoto katika maisha ya ukuaji zinaweza kupelekea ajikojolee kitandani. Ugonvi wa shuleni na michezo mingi ya nyumbani vinaweza kupelekea mtoto ajikojolee bila hiyari usiku. Mambo mengine yanayoweza kumtatiza mtoto akili mpaka akashindwa kujizuia mni pamoja na

  • kuzaliwa mtoto mwingine na yeye kuhisi atakosa upendo wa wazazi,
  • kuhamia makazi mapya na
  • mabadiliko ya ratiba zozote za nyumbani kama kula, kulala na kusoma.

Mjali mtoto mwenye tatizo la kukojoa kitandani

Zungumza na mtoto wako kwa upole namna anavyijisikia. Kumuonyesha mtoto kujali na uelewa kutamsaidia mtoto ajisikie vizuri na asiwe na msongo wa mawazo kuhusu tatizo lake.

Kama mtoto ameanza tatizo hivi karibuni na halikwepo kwa zaidi ya miezi 6, inaweza kuashiria tatizo la kiafya. Mpeleke mtoto hospitali endapo tatizo litaendelea zaidi ya wiki moja.

Usimchukie mwenye tatizo, chukia tatizo lenyewe

Usimchape mtoto kwasababu amekojoa kitandani, jua kwamba hajapenda hiyo hali. Ni muhimu kuwa na mazungumzo ya wazo na mazuri kati ya mzazi na mtoto kujua chanzoo cha tatizo lake. Mhakikishie mtoto kwamba uko naye pamoja katika kutafuta suluhisho la changamoto yake.

Pia jenga mazoea ya kumpa majukumu zaidi mtoto kutokana na umri wake. Kukojoa kitandani yaweza isiwe hida kubwa katika umri mdogo. Lakini kama tatizo linaendelea zaidi ya umri wa miaka mi5, kuna haja ya kumwona daktari bingwa wa magonjwa ya watoto.

Matibabu ya hospitali kwa tatizo la kujikojolea

Endapo shida ya kukojoa kitandani imeletekezwa na changamoto a kiafya, itahitaji matibabu zaidi ya kurekebisha tu mtindo wa maisha. Matibabu yatategemea na aina ya tatizo mfano

  • antibiotics kwa UTI
  • dawa za kupunguza tezi dume na
  • tiba za kutuliza kibofu kilichovimba na kututumka (anticholiergic drugs.
  • dawa za kisukari

Hitimisho kwa Tatizo la Kujikojolea

Watoto wengi huacha kukojoa kitandani katika umri wa miaka 6. Katika umri huu misuli ya kibofu inakuwa imara zaidi na imekuwa vizuri. Mabadiliko ya mtindo wa maisha, sapoti ya ndugu na wazi pamoja natiba ya hospita vinamaliza tatizo.

Japo tatizo hili la kujikojolea kitandani linaweza kumalizwa kwa kubadilisha mtindo wa maisha. Bado kuna umuhimu wa kutembelea hospitali ili kujua chanzo cha tatizo. Pia muhimu umwone daktari endapo tatizo limeanza ghafla katika utu uzima.

Kupata ushauri, Wasiliana nasi kupitia whatsapp tu namba 0678626254.

Bofya kusoma kuhusu tatizo la kula udongo+ushauri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *