Weupe kwenye Ulimi

weupe kwenye ulimi
weupe kwenye ulimi

Nini Kinapelekea weupe kwenye ulimi, na jinsi ya kutibu

Nina hakika ukijitazama kwenye kioo na kuona weupe kwenye ulimi wako na utando mweupe utaogopa sana. Japo kwa kiasi kikubwa hii hali ni kawaida. Ulimi wote waweza kuwa mweupe ama pakawepo na vidoti vyeupe.

Ulimi mweupe mara nyingi siyo jambo ya kuogopa, ispokuwa katika mazingira na dalili flani ambazo tutachambua kwa kina. Ndiomaana ni muhimu sana kufatilia dalili za mwili wako, na kwenda hospital endapo unaona kuna weupe usio wa kawaida kwenye ulimi wako.

Endelea kusoma kujifunza kuhusu tatizo na nini cha kufanya ili upate kutibu tatizo lako.

Nini kinasababisha weupe kwenye ulimi?

Ulimi mweupe kwa kiasi kikubwa ni changamoto za usafi. Ulimi wako unaweza kuzibwa kwa utando mweupe unaoganda na kuvimba.

Bakteria, mabaki ya vyakula, fangas na seli zilizokufa zinaweza kuganda kwenye ulimi. Mkusanyiko wa uchafu huu unaweza kufanya ulimi wako uonekane mweupe.

Hapa chini ni mambo yanayochangia ulimi wako kuwa mweupe

  • kushindwa kusafisha vizuri ulimi wako
  • mdomo kuwa mkavu
  • mwili kuishiwa maji
  • kuvuta sigara na tumbaku
  • matumizi ya pombe
  • kula zaidi vyakula laini na
  • kupumua kwa njia ya mdomo

Magonjwa yanayoweza kupelekea ulimi kuwa mweupe

1.Fangasi mdomoni ni chanzo cha weupe kwenye ulimi

Fangasi mdomoni kwa kitaalamu oral thrush au oral candidiasis ni maambukizi ya fangasi aina ya candida kwenye kuta laini za mdomo.

Kwa watu wengi wenye fangasi ya mdomo haileti changamoto kubwa sana na wanaweza kuishi na wagonjwa na maisha yakaendelea. Japo kwa watu wenye kinga dhaifu fangasi wa mdomoni huleta athari sana na dalili mbaya zaidi.

Habari njema ni kwamba wagonjwa wengi wanapona vizuri kabisa wakipatiwa tiba kwa fangasi za mdomoni. Japo wagonjwa wengi huugua tena katika kipindi cha muda mfupi baada ya kupona hasa kama chanzo cha fangasi kwa upande ni uvutaji wa sigara.

2.Kaswende inapelekea weupe kwenye ulimi

Kaswende ni ugonjwa wa zinaa. Unaambukiwa kwa njia ya tendo, na pia kunyonya uke au uume. Kama haitatibika inaweza kupelekea utando mweupe kwenye ulimi.

Dalili zingine za kaswende ni pamoja na

  • mwilili kukosa nguvu
  • homa kali
  • maumivu ya kichwa
  • maumivu ya joints
  • kupungua uzito ghafla na
  • nywele kunyonyoka

Kama kaswende isipotibiwa mapema inaweza kupelekea

  • kupofuka macho
  • kupoteza kumbukumbu
  • magonjwa ya moyo
  • kupoteza uwezo wa kusikia na
  • maambukizi kwenye ubongo

Kwa bahati nzuri ni kwamba kaswende ikigundulika mapema inatibika kupitia antibiotics. Japo kwa wanawake wenye ujauzito kaswende ni hatari zaidi, ndiomaana ni muhimu sana mjamzito kupimwa kama ana kaswende.

Lini unatakiwa kumwona daktari?

Kama tatizo ni utando tu mweupe yani hakuna dalili zingine, hapo hakuna haja ya kumwona daktari. Lakini kama dalili za weupe haziishi, na kuna dalili zingine hapa chini, mwone daktari mapema. Dalili hizi ni kama

  • ulimi wako unauma na unahisi kama unachoma
  • una malengelenge kwenye mdomo
  • unashindwa kutafuna, kumeza na kuongea
  • una homa, kupungua uzito na vipele mwilini

Nini cha kufanya ili ulimi uwe msafi wenye afya?

Japo ni ngumu kuzuia weupe kwenye ulimi mara zote. Kuna baadhi ya vitu unaweza kufanya kupunguza ukubwa wa tatizo

  • jijengee tabia ya kufanya usafi kwenye meno kama
  • kutumia mswaki laini
  • brush meno yako mara mbili kwa siku
  • punguza kutumia vyakula vya sukari

Mambo mengine muhimu ya kufanya

Punguza matumizi ya mouthwash: Watu wanaotumia mouthwash kwa muda mrefu ili kutibu harufu mbaya mdomoni wako kwenye hatari zaidi ya kupata fangasi mdomoni, kwasababu mouthwash zinaua na bakteria wazuri.

Jenga mazingira ya kumwona daktari wa meno kila baada ya miezi sita. Epuka kula au kuvuta vitu vya tumbaku kama sigara

Punguza matumizi ya vyakula vya kusindikwa viwandani
Kula lishe mchanganyiko yani aina mbali mbali za vyakula-gusa makundi mengi

Bofya kusoma makala inayofuata kuhusu Haufu mbaya mdomoni, chanzo, ushauri na tiba ya nyumbani