Tiba ya Mionzi na Chemotherapy, Faida na Madhara

tiba ya mionzi kutibu saratani
tiba ya mionzi

Kuugua saratani ni jambo linaobadilisha sana mwenendo wa maisha yako. Japo kuna tiba aina nyingi kupambana na saratani ili kuzuia isiendelee kusambaa, aina mbili kubwa ni chemotherapy nan tiba ya mionzi yaani (radiotherapy)

Chemotherapy na tiba ya mionzi ni moja ya tiba kuu zinazotumika kwa mgonjwa saratani aina nyingi. Ijapokuwa tiba hizi mbili zina lengo moja la kupambana na seli za saratani, zina utofauti wake.

Kwenye makala hii kuna maelezo ya kina juu ya aina hizi za tiba, utofauti wake, namna zinafanya kazi na madhara kwa mgonjwa.

Tofauti kati ya chemotherapy na tiba ya mionzi (radiotherapy)

Tofauti kati ya tiba hizi za kansa ni namna zinavyofanyika.

Chemotherapy

Ni dawa zenye nguvu sana ambazo mgonjwa wa saratani anapatiwa kuua seli za saratani. Dawa hizi waweza kunywa ama kupitia sindano.

Kuna aina nyingi sana za chemotherapy. Daktari anayekuhudumia atapendekeza upate dawa sahihi kulingana na aina na stage ya saratani yako.

Chemotherapy yaweza kuwa na madhara mengi inategemea tu na aina ya dawa unayopatiwa.

Tiba ya mionzi(radiotherapy)

Tiba inajumuisha matumizi ya mionzi mikali kuelekea kwenye uvimbe wa saratani. Mionzi hii inabadili zinasaba vya seli za saratani na kuzifanya dhaifu mpaka zinakufa.

Aina hii ya tiba ina madhara madogo kwani inalenga tu kwenye uvimbe wa saratani.

Chemotherapy inavyofanya kazi

Chemotherapy ni dawa zinazolenga kuua seli za saratani kwenye mwili wako, seli ambazo zinaganyikwa kwa haraka na kuzalisha seli nyingine za saratani. Changamoto inakuja kwamba kuna seli zingine mwili ambazo siyo za saratani lakini zina kawaida ya kugawanyika haraka kuzalisha seli zingine nyingi. Maana yake seli hizi pia zitaathiriwa na chemotherapy.

Seli zingine zinazogawanyika kwa haraka ambazo siyo za saratani ni kama seli za

  • Nywele
  • Kucha
  • Mfumo wa chakula na
  • Mifupa(bone marrow)

Chemotherapy inaweza kuathiri seli za maeneo haya na kuleta madhara kwa mgonjwa. Daktari wako wa saratani (oncologist) atachagua dawa yenye madhara madogoi kulingana na afya yako.

Namna Tiba ya chemotherapy inavyotolewa

Tiba ya chemotherapy inaweza kutolewa aidha kwa kumeza mdomoni au kupitia sindano. Chemotherapy hutolewa kwa awamu, hasa kila baada ya wiki kadhaa.

Madhara ya chemotherapy

Unaweza kupata madhara kutokana na tiba hii ya chemotherapy. Madhara yanategemea na aina ya dawa ulizopatiwa. Baadhi ya madhara ya chemotherapy ni pamoja na

  • Kutapika na kichefuchefu
  • Nywele kunyonyoka
  • Uchovu kupita kiasi
  • Vidonda mdomoni
  • Kuharisha
  • Kupata maambukizi ya bakteria au fangasi
  • Kupungukiwa damu
  • Maumivu na ganzi kwenye miguu na mikono
  • Kuishiwa nguvu

Ni muhimu kufahamu kwamba aina tofauti za chemotherapy zinaleta aina tofauti pia za madhara. Na pia uwezo wa kuhimili chemotherapy unatofautiana kwa kila mgonjwa. Siyo kila mgonjwa atapata dalili zote mbaya.

Namna Tiba ya mionzi inavyofanya kazi

Tiba ya mionzi inajumuisha mionzi mikali kuelekezwa kwenye uvimbe wa saratani. Mionzi hii inabadili mpangilio wa vinasaba wa uvimbe, na kufanya seli za saratani kufa baala ya kuganwanyika na kuongezeka.

Tiba ya mionzi inaweza kutumika pamoja na tiba ingine katika

  • Kupunguza ukubwa wa uvimbe kabla ya kufanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe huo wa saratani
  • Kuua seli za saratani zilizosalia baada ya upasuaji
  • Kutumika pamoja na chemotherapy
  • Endapo una changamoto ya kiafya inayokuzuia kupata chemotherapy, mionzi pekee unaweza kutumika.

Namna tiba ya mionzi inavyotolewa

Kuna aina kuu tatu na tiba ya mionzi kutibu kansa

External beam radiation: Mionzi inaelekezwa moja kwa moja kutokwa kwenye mashine ya mionnzi kupitia juu ya ngozi mpaka kwenye eneo lenye saratani.

Internal radiation: Madini yenye mionzi huwekwa ndani ya mwili kwenye eneo lenye saratani, madini haya yanaweza kuwa kimiminika au metali ngumu.

Sytemic radiation: Njia hii inajumuisha matumizi ya mionzi katika mfumo wa kidonge au kimiminika ambacho unatumia kwa kumeza mdomoni au kwa sindano kwenye damu.

Aina husika ya moinzi utakayopatiwa inategemea na aina ya saratani uliyonayo na pia namna daktari anavyofikiri kwamba itakusaidia zaidi.

Madhara ya tiba ya mionzi

Kwasababu tiba ya mionzi inalenga eneo moja tu lenye saratani, madhara yake ni madogo ukilinganisha na chemotherapy. Japo seli zingine ambazo siyo saratani zinaweza kuathiriwa pia. Madhara ya mionzi ni kama

  • Changamoto ya mfumo wa chakula kama kichefuchefu, kutapika na kuharisha
  • Mabadiliko ya ngozi
  • Kupoteza nywele
  • Uchovu na
  • Kushindwa kufanya tendo la ndoa

Je chemo na mionzi hutumika kwa pamoja?

Chemo na mionzi kwa kiasi kikubwa hutumika kwa pamoja katika kutibu aina fulani za saratani. Tiba huitwa concurrent therapy. Tiba hii huependekezwa endapo aina yako ya saratani

  • Haiwezi kuondolewa kupitia upasuaji
  • Inaweza kusambaa maeneo ya karibu
  • Haiponi kupitia aina moja ya tiba

Namna ya kuishi na madhara ya Chemo na mionzi

Kwa tiba zote mbili ya mionzi na chemo, tumeona kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kupata adhara mbalimbali. Hiyo haimaanishi kwamba huwezi kufanya chochote kupunguza madhara haya

Hapa chini ni ushauri wa kufatilia ili kuishi na madhara haya ya tiba

  • Ongea na daktari kuhusu dawa unazoweza kutumia kupunguza kichefuchefu na kutapika
  • Jaribu kunywa chai ya tangawizi kuondoa kichefuchefu
  • Gawanya milo yako, kisha ule kidogo kidogo. Kula zaidi vyakula vyenye virutubishi vingi
  • Nawa mikono yako mara kwa mara kupunguza hatari ya kupata maambukizi
  • Muda wote hakikisha unawasiliana na daktari juu ya madhara unayopata

Soma zaidi kuhusu lishe ya mgonjwa wa saratani