Tendo la Ndoa Baada ya Kujifungua

tendo la ndoa baada ya kujifungua

Nini cha kutarajia unapoanza tendo la ndoa baada ya kujifungua?

Muda gani usubiri kuanza tendo la ndoa baada ya kujifungua? Ujauzito na kujifungua ni matukio yanayobadilisha sana mwonekano wako na hata namna utakavoshiriki tendo la ndoa.

Mabadiliko ya homoni baada ya kuzaa yanabadilisha tishu za kwenye uke na kuwa nyembamba na za kusisimka zaidi. Kunyonyesha pia kunapunguza sana hamu ya tendo. Kwa kifupi mwili wako utahitaji muda zaidi wa kupunzika bila kufanya tendo baada ya kujifungua.

Usubiri muda gani kuanza tendo la ndoa baada ya kujifungua?

Hakuna muda maalumu wa mwili wa kusubiri ndipo uanze tendo baada ya kuzaa. Inatofautiana kwa kila mwanamke. Japo madaktari wanashauri usubiuri walau wiki 4 mpaka wiki 6 kama ulijifungua kawaida.

Utahitaji kusubiri zaidi ya miezi miwili endapo ulijifungua kwa kuongezewa njia ya uke. Ama ulijifungua kwa upasuaji ili kuhakishika majeraha yanapona vizuri.

Je kujifungua inaathiri vipi tendo la ndoa?

Tendo la ndoa baada ya kujifungua ni tofauti sana. Tafiti zinasema asilimia 80 ya wanawake wanapata changamoto ya tendo kwenye miezi mi3 ya mwanzo baada ya kujifungua. Changamoto nyingi wanazopata wanawake ni pamoja na

  • uke kuwa mkavu
  • mashavu ya uke kusinyaa
  • uke kutovutika
  • kutokwa na damu
  • maumivu kwenye tendo
  • misuli ya uke kulegea
  • kuvimba uke
  • kukosa hamu ya tendo na
  • kuchoka sana baada ya tendo

Usijilaumu ni Mabadiliko ya Homoni

Fahamu tu kwamba siyo kosa lako kupatwa na hii hali, na wala usijilaumu kabisa. Ni mabadiliko tu ya homoni, na homoni hizo hizo zitakusaidia kurejea katika hali nzuri ya kufurahia tendo.

Siku chache baada ya kujifungua, kiwango cha homoni ya estrogen hupungua sana. Estrogen ndio huchochea uzalishaji wa uteute ukeni. Kwahivo kiwango chake kikipungua, uke unaanza kuwa mkavu.

Nyama za uke zinapokauka, zinafanya upate majeraha kirahisi. Majeraha yanongeza hatari ya kupata maambukizi.

Misuli ya uke Kulegea

Kitendo cha kujifungua pia kinafanya misuli ya uke kutanuka zaidi kwa muda. Lakini usiogope, kwani misuli hii itarejesha kuwa imara baada tu ya week kadhaa.

Jipe muda upone kidonda

Kama uliongezewa njia wakati wa kujifungua, itakuchukua muda mrefu kupona. Ukijaribu kufanya tendo mapema utachelewa kupona kidonda na kuhitaji kushonwa tena. Pia inaongeza chansi ya kupata maambukizi kama utaanza tendo haraka.

Kujifungua kwa upasuaji kunaweza pia kuathiri uke. Utahitaji kupona kwanza kidonda, hivo siyo sawa kuanza tendo mapema. Shugulikia kwanza kidonda kipone

Je naweza kushika mimba ingine mapema bila tatizo?

Jibu ni ndio, unaweza kushika mimba ingine haraka sana baada ya kujifungua. Kwa wanawake ambao hawajanyonyesha vizuri kwenye week 6 za mwanzo yai linaweza kupevuka. Na yai linapevuka kabla ya hedhi kutoka. Kumbe waweza kushika mimba mapema tu hata kabla hujaona hedhi yako ya kwanza.

Kama unanyonyesha vizuri, homoni za maziwa zinakuwa juu na hivo kukukinga dhidi ya mimba. Kumbuka njia hii inaleta matokeo mazuri sana endapo:-

  • mwanamke hajaanza kupata hedhi
  • ananonyesha mara kwa mara biula kupitisha masaa manne
  • mzazi yupo chini ya miezi sita baada ya kujifungua na
  • mtoto bado hajaanzishiwa chakula zaidi ya maziwa ya mama

Kumbuka: Kipengele kimoja tu kikikosekana hapo juu basi hi njia inakuwa haifai tena kupanga uzazi.

Fikiria Kutumia Njia za Kisasa Kupanga Uzazi

Kama hutaki kushika mimba ingine haraka, basi tumia njia zingine za uhakika kujizuia na mimba.

Ikiwa bado hujafanya maamuzi ya njia ya kutumia na unahitaji tendo, anza kwa kutumia condom. Ongea na daktari akwelekeze njia sahihi kwa upande wako.

Je ni salama kushika mimba ndani ya mwaka mmoja baada ya kuzaa?

Kushika mimba mapema sana kunakuweka kwenye hatari ya kujifungua mtoto njiti ama mtoto mwenye matatizo ya kimaumbile.

Wataalamu wa afya wanashauri mama ajiwekee muda wa kupumzika walau mwaka mmoja baada ya kumaliza kunyonyesha. Ama ukishindwa sana walau mwaka mmoja baada ya kujifungua.

Je kutokwa damu katikati na baada ya tendo ni kawaida?

Wiki chache baada ya kujifungua, utapata hali ya kutokwa na matone ya damu kwasababu kizazi kinajitibu. Tendo linaweza kuongeza kiwango cha kuvuja damu.

Pia uke wako utakuwa mkavu na unaosisimka zaidi. Kitendo hichi kitafanya misuli ya uke kusinyaa na hivo kupelekea majeraha na michubuko. Uke wako waweza pia kuvimba.

Kama damu itaendelea kutoka hata zaidi ya week sita za mwanzo, hakikisha unamwona daktari haraka. Utahitaji kutibiwa kwanza majeraha kabla hujarudia kufanya tena tendo.

Hamu ya Tendo la ndoa baada ya kujifungua

Homoni mbili za estrogen na progesterone zinaleta mchango mkubwa sana kwenye ukuaji wa mtoto wakati una mimba. Pia ndizo zinakufanya upate hamu ya tendo la ndoa.

Kiwango cha homoni hizi huwa juu sana nyakati za ujauzito. Baada tu ya kujifungua, homoni zinashuka kwa kasi.

Hii ina maana gani? ina maana kwamba utakosa hamu ya kushiriki tendo kwa week za mwanzo. Lakini mwili utarejea kawaida baada ya wiki sita.

Kunyonyesha na hamu ya tendo la ndoa baada ya kujifungua

Kama unanyonyesha kwa njia ya titi unaweza kuchukua mda mrefu zaidi kwa hamu ya tendo kurejea. Nasema kunyonyesha kwa matiti sababu kuna wengine wanapendelea kukamua kwa mashine.

Lakini pia jambo lenyewe la kulea mtoto linachosha akili na mwili kwa wazazi wote. Hivo itakufanya ukose muda na hamu ya tendo, kwasababu nguvu kubwa umeitumia kwa mtoto.

Jambo zuri ni kwamba baada tu ya kumaliza kunyonyesha, homoni zitakuwa juu tena na hamu ya tendo itarudi kama zamani.

Nini ufanye na mpenzi wako ili muweze kuenjoy tendo wakati mnalea mtoto?

1.Usikamie(take it slow). Jipe muda kwanza wa kupumzika baada ya kuzaa. Jipe hata miezi miwili au mitatu. Fanya tendo taratibu hata bao moja tu kwa siku.

2.Romance iwe ya kutosha kabla ya tendo: Hakikisha uke wako unalowa ipasavyo. Ongeza muda wa maandalizi kama hujaanza tendo husika

3.Tumia vilainishi: Unaweza kuhitaji vilainishi ili kupunguza msuguano na michubuko. Ongea na daktari wako kushauri zaidi.

4.Anza kufanya mazoezi ya kegel: Mazoezi haya yanasaidia kuimarisha misuli ya uke na zoezi linakusaidia usiponyokwe na mkojo. Unapoenda kukojoa usitoe mkojo wote, bana kwa sekunde 5 kisha achia, rudia tena seti 4 au 5. fanya hivo kila unapoenda kukojoa

5.Tenga mda wa tendo la ndoa: kwasababu kuna mwanafamilia mpya ndani ya nyumba, wewe na mpenzi wako mzungumze na muweke ratiba ya tendo la ndoa. hakikisheni mnakubaliana juu ya ratiba hii.

6.Ongea na mpenzi wako: Tendo la ndoa baada ya kujifungu ni tofauti, na siyo kwako tu ni kwa kila mtu. Hakikisheni mnazungumza kwa uwazi kuhusu mabadiliko haya na namna ya kukabiliana nayo. Hii itawafanya mfurahie tendo na kutolaumiana.

Soma Makala inayofuata kuhusu: Kujamba Sana Baada ya Kujifungua