Categories
Afya ya mwanamke na uzazi

Kupona Mapema Baada Ya Kujifungua Kwa Upasuaji

Kujifungua mtoto ni jambo la furaha sana kwa kila mwanmke aliyekuwa mjamzito. Maana mwisho wa siku unapata kiumbe chako baada ya kukibeba tumboni kwa shida miezi tisa yote. Kujifungua kwa uke kuna tofauti na kujifungua kwa upasuaji.

Pamoja na furaha yote lakini kumbuka kwamba kujifungua kunakuja na mzigo mwingine hasa mabadiliko ya mwili wako. Shepu itabadilika sana na utahitaji kuzoea tabia mpya. Kama umejifungua kwa upasuaji utahitaji mda nwingi zaidi wa kupumzika. Hapa chini ni

Hatua za tano za kukusaidia kupona mapema baada ya kujifungua kwa upasuaji

1.Pata Muda Zaidi Wa Kupumzika

Kama ilivyo kwa upasuaji mwingine, upasuaji wa kujifungua unataka upumzike zaidi ili kupona mapema. Baada ya kujifungua unaweza kukaa hospitali kwa siku 3 mpaka 5, na baada ya hapo itachukua mpaka week 6 kupona kabisa.

Hakikisha unalala kila wakati mtoto anapopata usingizi, maana akiamka atahitaji uwepo wako. Pata usaidizi kutoka kwa ndugu ama uwe na mfanyakazi(beki tatu) kwa ajili ya kumbeba mtoto na kubadilisha nguo, itakusaidia kupumzika zaidi

2.Usifanye Kazi Ngumu

Unapojifungua kwa upasuaji mwili unalegea na wahitaji matunzo kama ya mtoto mdogo. Usipandishe ngazi wala kuinua vitu vizito sana. Hakikisha kila kitu inachohitaji kwa haraka kama nepi, pampasi na chakula kipokaribu yako.

Usibebe kitu chochote kizito zaidi ya mtoto wako. Waambie ndugu wa karibu wakusaidie kubeba maji kupeleka bafuni na vitu vingine vizito. Unapotaka kukohoa au kupiga chanya basi hakikisha unashikilia tumbo lako ili kuulinda mshono.

Ongea na daktari akujulishe ni baada ya muda gani utaruusiwa kuanza kazi zako na pia mazoezi ili kutengeneza tena shepu yako.

3.Usianze mazoezi magumu haraka

Fanya mazoezi mepesi, kama kutembea kila siku kadiri utakavoweza. Pia usianze kufanya tendo mapema, subiri mpaka pale daktari atakapokuruhusu.

Usisahau pia kuwa makini na afya ya akili kama vile unavotunza mwili wako, tunza na hisia zako pia. Kuwa na mtoto mchanga itakupa hisia mbalimbali ikiwemo hasira za hapa na pale, uchovu na zingine. Zungumza na rafiki yako wa karibu namna unavojisikia au mshauri wa afya ya akili.

4.Tumia dawa za Maumivu inapobidi

Ongea na daktari kabla ya kumeza dawa pale maumivu yanapokuwa makali sana. Kumeza dawa kiholela kwa kipidi hii unaponyonyesha ni hatari.

Pata Lishe Ya Kutosha

Mlo kamili ni muhimu sana kwa kipindi hiki unaponyonyesha na unapouguza kidonda chako. Kumbuka kwamba mtoto wako anategemea sana chakula unachokula.

Hakikisha unakula aina nyingi za vyakula katika siku husika. Tafiti zinasema kwamba kutumia mboga za majani kwa wingi wakati wa kunyonyesha zinafanya ladha ya maziwa kwa mtoto kuwa nzuri na mtoto ufurahia zaidi anaponyonya. Pia muhimu kunywa maji ya kutosha ili usipate choo kigumu ama kukosa choo.

Lini Watakiwa Kumwona Daktari?

Wakati unajiuguza unaweza kupata hali ya kidonda kupata malengelenge na damu kutoa kidogo hiyo ni kawaida. Lakini ukiona dalili hizi hapa chini hakikisha unaenda hospitali haraka.

Dalili mbaya ni pamoja na

  • kidonda kuwa chekundu, kuvimba na kutoa usaha
  • maumivu makali sana eneo la kidonda
  • homa kali ya zaidi ya nyuzijoto 38
  • kutokwa na uchafu wenye harufu kali ukeni
  • kutokwa na damu nyingi ukeni
  • miguu kuvimba
  • kushindwa kupumua vizuri
  • maumivu ya kifua
  • maumivu kwenye eneo la matiti

Kama kuna ndugu au rafiki yako aliwahi kujifungua kwa upasuaji usijilinganishe nae katoka kupona kwako. Kila mwanamke ana mwili wa tofauti, wekeza nguvu na hisia zako katika afya yako itakusaidia kupona mapema.

Unahitaji maoni na Ushauri? Tuandikie kwa Whatsapp namba 0678626254. Usipige simu namba ni ya whatsapp tu

Bofya kusoma makala inayofuata kuhusu: Maandalizi ya kujifungua kwa upasuaji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *