Dawa ya Doxycycline Kutibu Gono na Kaswende

dawa ya doxycycline
dawa ya doxy

Dawa ya doxycycline kwa kifupi doxy, ni dawa maarufu sana kwa rika la vijana. Kati ya vijana 10 watano waliwahi kutimia dawa ya doxy kutibu magonjwa ya zinaa.

Dawa hii inatumika kutibu magonjwa mengi yanayosababishwa na bakteria. Doxy pia hutumika kutibu malaria. Dawa inafanya kazi kwa kuzuia kusambaa kwa vimelea wa bakteria. Kumbuka dawa ni kwa kutibu magonjwa ya bakteria tu na siyo magonjwa ya virusi labda daktari akwelekeze vingine.

Namna ya kutumia dawa ya doxycycline

Kabla ya kuanza kutumia dawa, ni vizuri kusoma karatasi ya maelezo inayopatikana kwa mfamasia. Dawa ya doxy ni vizuri ikamezwa walau masaa mawili baada au kabla ya kula. Meza dawa kwa kutumia maji ya kutosha walau glass moja ya maji.

Dawa haitafanya kazi vizuri endapo utameza muda mchache baada ya kula, ama baada ya kunywa maziwa au chakula chochote chenye madini ya calcium. Ongea na daktari au mfamasia masharti ya kutumia dawa. Baada ya kumeza dawa usilale kwa muda wa dakika 10.

Endapo unatumia doxycycline kujikinga na malaria, dawa hutumika mara moja kwa siku. Kama unasafiri kwenda kwenye nchi zenye kiwango kikubwa cha wagonjwa wa malaria, meza siku mbili kabla.

Kipimo cha dawa

Kama unatumia doxy ya maji, hakikisha unatingisha chupa vizuri kabla ya kutumia. Pima kiwango cha dawa kwa umakini kwa kutumia kijiko au kizibo kilichokuja na dawa. Usitumie kijiko cha nyumbani kwasababu utapata kipimo tofauti.

Kwa watoto dozi inategea pia uzito wa mgonjwa.

Ili kupata matokeo mazuri ya dawa, meza dawa katika muda ule ule kila siku. Endelea kumeza dawa mpaka umalize dozi kama ulivyoelekezwa na daktari. Kukatisha dawa kunapelekea bakteria kuwa sugu  na kushambulia mwili zaidi.

Matokeo/madhara ya kutumia doxycycline

Dalili kama tumbo kuvurugika, kuharisha, kichefuchefu na na kutapika vinaweza kutokea baada ya kuanza dozi ya doxy. Kama dalili zitaendelea kuwa mbaya zaidi mjulishe daktari.

Pia mjulishe daktari endapo una dalli zingine mbaya kama maumivu wakati wa kumeza chakula, dalili za shida kwenye figo kama mkojo mweusi.

Changamoto kwenye fuvu la kichwa

Doxcylicine yaweza kuleta tatizo kubwa la mgandamizo ndani ya fuvu la kichwa(intracranial hypertention). Wanawake walio kwenye umri wa kuzaa na wenye uzito mkubwa wapo kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo hili..

Dalili mbaya mara nyingi huisha baada ya kumaliza dozi. Nenda hospitali mapema endapo utapata dalili za kichwa kuuma sana na kupungua uwezo wa kuona.

Matumizi ya doxycycline kwa muda mrefu yanaweza kupeleka fangasi mdomoni na ukeni. Mjulishe daktari mapema kama utaanza kuona utando usio wa kwaida mdomoni, au kutokwa na uteute mweupe mwingie ukeni.

Tahadhari kabla ya kutumia doxycycline

Usitumie doxy kama hujapimwa hospital na kuandikiwa na daktari aluyekupima. Pia kabla ya kuanza kutumia dawa ya doxycycline, mjulishe daktari kama una aleji na dawa; ama aleji ya antibitiocs zozote. Dawa hii ina kiambata hai cha sulfites ambaho hueta aleji kwa baadhi ya wagonjwa.

Kabla ya kumeza dawa, mjulishe daktari historia ya magonjwa yako, hasa kama una tatizo la kumeza chakula, hernia ya kifuani na kiungulia.

Dawa ya doxycycline inaweza kukufanya kusisimka zaidi na mwanga wa jua. Punguza muda wa kuwa juani. Vaa nguo za kufunika mwili vizuri ukiwa juani.

Mjulishe daktari kama una ujauzito au unapanga kushika mimba hivi karibuni. Hutakiwi kushika mimba mapema wakati upo kwenye dozi ya doxycycline. Dawa inaweza kumuathiri mtoto aliye tumboni. Mjulishe pia daktari endapo unanyonyesha.

Mwingialiano wa doxy na dawa zingine

Mwingialiano wa dawa unaweza kupunguza ufanisi wa dawa ingine na kuongeza hatari ya madhara. Andiko hili halitoi maelezo yote kuhusu mwingiliano wa doxy na dawa zingine. Kuna umuhimu wa kumsikiliza daktari vizuri kabla ya kuanza tiba.

Baadhi ya dawa za kifafa kama phenobarbital, dawa za kuchochea mzunguko mzuri wa damu (blood thiners) hupunguza ufanisi wa doxy.

Kama unatumia chakula au kinywaji chenye madini ya calcium, aluminium, chuma, magnesium, zinc,  meza doxy masa matatu baada ya kutumia chakula/kinywaji chako. Baadhi ya vitu vyenye madini haya ni kama dawa za kupunguza asidi, maziwa, multivitamins na juisi zenye calcium.

Muhimu kuzingatia

Usichangie dozi ya doxycycline na mtu mwingine. Kama dawa unatumia kuzuia kupata malaria, muhimu ujue bado upo kwenye hatari ya kupata malaria.

Dawa hii umepatiwa kwa tatizo lako la sasa. Usitunze na kutumia kwa wakati ujao. Endapo utasahau kumeza dozi, meza mapema pale unapokumbuka. Meza dawa muda ule ule kila siku. Na kama unapata dalili mbaya zaidi muone daktari mapema

Uhifadhi wa dawa

Tunza dawa kwenye joto la wastani mbali na mwanga mkali na pasiwe na unyevunyevu. Usitunze dawa chooni. Dawa isiyotumia itupe. Hifadhi dawa mbali na watoto. Tupa dawa kama imepita muda wake wa matumizi (expire date)

Bofya kusoma kuhusu: Matumizi sahihi ya P2, maswali na majibu

11 replies on “Dawa ya Doxycycline Kutibu Gono na Kaswende”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *