Folic Acid Kwa Mjamzito

folic acid
Folic Acid

Folic acid naweza kusema ni moja ya kitu cha muhimu zaidi kwa mjamzito ambacho kitakuvusha kuelekea kujifungua mtoto mwenye afya njema zaidi. Inashauriwa kutumia kiwango cha microgramu 400 za folic acid kabla na baada ya ujauzito.

Inasaidia kujifungua mtoto mweye afya njema ya ubongo na uti wa mgongo pia. Hakikisha unatumia kila siku kama ulivyoelekezwa hospitali.

Folic Acid ni Kitu Gani?

Folic acid ni vitamin B ambayo inapatikana zaidi kwenye mboga za kijani na matunda yenye uchachu kama limau na chungwa. Lakini pia inaweza kutengenezwa maabara. Jina lingine la folic acid huitwa folate. Kazi kubwa za folic acid ikiwa ni kuimarisha uzalishaji wa seli hai nyekundu za damu na pia ukuaji wa ubongo na uti wa mgongo kwa kiumbe cha tumboni.

Lini Natakiwa akuanza Kumeza Vidonge vya Folic Acid?

Changamoto za kimaumbile hasa hutokea mimba ikiwa na week 3 mpaka 4. Kwahivo ni muhimu sana kuwa na kiwango kikubwa cha folate katika umri huu wa mimba. Ndio maana kuna umuhimu sana wa kupanga kushika mimba, ili kabla mimba haijaingia tayari uanze kumeza folic acid.

Kituo cha udhibiti wa magonjwa cha nchini marekeni(CDC) kinapendekeza kumeza folic acid mwezi mmoja kabla ya kushika mimba, na kuendelea kumeza kila siku mpaka utakapojifungua.

Kiasi Gani Cha Folic Acid Natakiwa Kumeza Kila Siku?

Kiwango kinachopendekezwa na shirika la afya duniani kwa mwanamke alieyepo kwenye umri wa kuzaa ni 400 mcg kila siku. Kama unameza multivitamin basi hakikisha unajua kuna kiwango gani cha folic acid ndani yake kujua kama kinakidhi kiwango kinachotakiwa.

Hapa chini ni mwongo kwa makundi yote ya wanawake juu ya kiwango cha folic acid kinachotakiwa kutumika.

  • kama ndo wajiandaa kushika ujauzito: 400 mcg
  • miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito: 400 mcg
  • miezi minne mpaka tisa ya ujauzito: 600 mcg
  • wakati wa kunyonyesha :500 mcg

Faida za Kumeza Folic Acid ni zipi hasa?

Kama tulivosema awali, bila kiwango cha kutosha cha folic acid kiumbe kilichopo tumbo hakiwezi kukua vizuri inavotakiwa. Kiumbe kinaweza kupata changamoto za ukuaji wa ubongo na uti wa mgongo. Matatizo haya kitaalamu huitwa
Spina bilfida: yaani kutokamilika ukuaji wa uti wa mgongo na
Anencephaly: Kutokamilika kwa ukuaji wa sehemu muhimu za ubongo.

Habari njema ni kwamba unaweza kuepuka madhara haya kwa mtoto anayezaliwa kwa kutumia kiwango sahihi cha folic acid. Kama tayari uliwahi kujifungua mtoto mwenye matatizo ya uti wa mgongo na ubongo basi hakikisha unaongeza kiwango cha folic acid unachotumia mpaka mcg 4000 sawa na gramu 4 kila siku. Zungumza pia na daktari kwa kina kabla ya kuanza kumeza.

Kumeza Folic Acid kabla na baada ya ujauzito kutamlinda mtoto dhidi ya

Lakini pia kwa mjamzito folic acid inapunguza hatari ya kupata matatizo kama

Chanzo cha Folic Acid kutoka kwenye Vyakula

Vyakula vitakavyokupa folic acid kwa kiwango kikubwa ni pamoja na

  • Maini: ujazo wa kiganja -215 mcg
  • Parachichi moja: 59 mcg
  • Broccoli: ujazo nusu kikombe-52 mcg
  • Juisi ya machungwa: ujazo kikombe kimoja- 35 mcg
  • yai moja- 22 mcg
  • Maziwa fresh: kikombe kimoja: 12 mcg

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *