Shahawa Nyepesi

shahawa nyepesi
mbegu za kiume

Mwisho wa makala hii, tayari utakuwa umejua kwanini unapata shahawa nyepesi, kiwango cha mbegu kinachotakiwa kumpa mwanamke mimba, nini cha kufanya ili shahawa zako ziwe nzito na mbegu ziwe nyingi zaidi.

Nini maana ya shahawa

Shahawa ni majimaji yanayozalishwa wakati na kutolewa wakati mwanaume anapomwaga mbegu kwenye tendo la ndoa. Shahawa zinabeba mbegu na majimaji mengine kutoka kwenye tezi dume.

Kikawaida shahawa zinakuwa nzito na nyeupe kwa rangi. Japo kuna baadhi ya sababu zinaweza kupelekea mabadiliko ya rangi ya shahawa. Shahawa nyepesi inaweza kuwa ni kiashiria cha mbegu chache na hivo kukufanya ushindwe kumpa mwanamke mimba.

Sababu kubwa nne kwanini unatoa shahawa nyepesi.

1.Upungufu wa mbegu

Sababu kubwa ya shahawa zako kuwa nyepesi ni upungufu wa mbegu(low sperm count). Kitaalamu hujulikana kama oligospermia. Kama una mbegu chache maana yake zipo kidogo kuliko kiwango cha chini kinachohitajika kumpa mwanamke mimba. Mbegu chini ya milioni 15 kwa milliliter ndizo chache sana.

Baadhi ya sababu zinazopelekea uwe na mbegu chache ni pamoja na

 • kuvimba kwa mishipa midogo ya damu kwenye korodani mpaka kupelekea kushuka uzalishaji wa mbegu
 • maambukizi hasa magonjwa ya zinaa na kisonono
 • vimbe kwenye korodani mpaka kuathiri uzalishaji wa mbegu
 • homoni kuvurugika: upungufu wa homoni ya kiume ya testosterone unafanya uzalishaji wa mbegu kupungua
 • majeraha kwenye via vya uzazi
 • tatizo la mbegu kutotoka nje na badala yake kurudi ndani(retrograde ejaculation)
 • matatizo ya kinga ya mwili kushambulia mbegu

2.Kumwaga mbegu mara kwa mara inapelekea shahawa nyepesi

Kumwaga sana mbegu kila mara, ni sababu ya mbegu zako kukosa ubora na hivo kutoa mbegu nyepesi. Kupiga punyeto ni sababu mojawapo inayokufanya umwage mbegu sana.

3.Upungufu wa madini ya zinc

Tafiti zinasema kwamba wanaume wenye madini ya kutosha ya zinc mwilini au wanaotumia virutubishi vya zinc, wanakuwa na mbegu nyingi ukilinganisha na wale wenye upungufu wa zinc.

4.Majimaji ya kusafisha njia ya kutoka mbegu.

Kama unaona umetokwa na majimaji kabla hata hujaanza tendo au katikati ya tendo , unaweza kudhani ndio mbegu kumbe ni kemikali tu inatolewa ili kusafisha mazingira mbegu zije kupita pasipo kudhurika.

Je ni Sahihi Kupata Shahawa Zenye rangi?

Endapo utagundua shahawa zako siyo nyeupe, zina rangi ya njano ama pink basi ujue kuna shida mahali. Shahawa zenye rangi nyekundu ama pink inamanisha tezi dume yako imevimba ama pia mirisha ya kusafirisha mbegu inavuja damu.

Shahawa za njano zinaweza kuashiria uwepo wa mkojo. Na shahawa za njano na kijani zinaashiria kwamba kuna maambukizi kwenye tezi dume.

Lini unatakiwa Kumwona Daktari?

Kama umefatilia na kuona mbegu zako ni nyepesi kwa muda mrefu, onana na daktari bingwa wa magonjwa ya wa uzazi kwa wanaume mapema(urologist).

Utakaopenda hospitali kipimo cha kwanza utakachofanyiwa ni semen analysis ili kujua una mbegu kiasi gani. Lakini pia kipimo kitagundua ubora wa mbegu zako.

Daktari pia anaweza kukuuliza historia ya changamoto yako. Aatakuuliza pia mwenendo wa maisha yako kiujumla ikiwemo vyakula unavyokula na kunywa.

Matibabu ya Shahawa Nyepesi

Uwezekano wa kumpa mwanamke mimba unapungua sana ukinganisha na yule mwenye shahawa nzito.
Matibabu ya changamoto yako yatazingatia na chanzo cha tatizo. Mfano kama shida ni maambukizi utapatiwa antibiotics utapona.

Nini Ufanye ili Kuimarisha Shahawa Zako

Kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya mtindo wako wa maisha yatakusaidia kuimarisha uzalishaji wa mbegu. Zingatia mambo haya 6

 1. Acha kuvuta sigara
 2. Punguza matumizi ya pombe
 3. Rekebisha uzito mkubwa na kitambi kama unalo tatizo hilo
 4. Punguza matumizi ya vyakula vyenye sukari
 5. Jitahidi kudhibiti msngo wa mawazo unaweza kusoma hapa njia salama za kupunguza stress
 6. Weka ratiba ya kufanya mazoezi walau mara 4 kwa week

Daktari pia anaweza kukushauri upumzike kwa muda kidogo kufanya tendo la ndoa ili kupunguza kasi ya kumwaga mbegu mara kwa mara.

Tumia tiba hii ya mimea kupitia vidonge vya zinc na confido kuongeza shahawa na mbegu.

zinc na confido

Ni tiba asili zilizotengenezwa wa mimea, zikawekwa kwenye mfumo wa vidonge na kuthibitishwa na mamlaka ili kutibu changamoto za kiume. Changamoto kama upungufu wa mbegu, shahawa nyepesi, kuwahi kufika kileleni na uume kutosimama vizuri kwenye tendo.

Huhitaji kujaribu dawa zisizo na uhakika, tayari tumeshafanya utafiti wa kina na kujiridhisha kwamba dawa hizi mbili, zikitumika kwa pamoja zinaleta matokeo ndani ya mwezi mmoja.

Baada ya kutumia Confido na zinc tegemea haya

 • Shahawa kuwa nzito, na mbegu kuongezeka na kufikia kiwango cha zaidi ya milioni 40 kwa mililita
 • Uwezo wa kufanya tendo kuongezeka na utaweza kurudia mpaka mara tatu bila kuchoka
 • Hamu ya tendo kuimarika na kukufanya ufurahie tendo la ndoa
 • Misuli ya uume kuimarika na kukufanya uwe imara wakati wote wa tendo

Gharama ni Tsh 150,000/= dozi ya mwezi mmoja.

Tunapatikana mwembechai Dar, Chati na daktari kwa whatsapp namba 0678626254 kuanza tiba

Bofya hapa kusoma kwanini unawahi kufika kileleni na kushindwa kurudia tendo na

Namna ya kumkuna mwanamke akatoa maji wakati wa tendo

11 replies on “Shahawa Nyepesi”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *