Categories
Magonjwa ya viungo

Miguu kujaa maji, Chanzo, Ushauri na Tiba

miguu kujaa maji
mguu uliovimba

Nini maana ya miguu kujaa maji?

Kujaa maji kitaalamu edema, ni kitendo cha kuvimba kwa maneneo mbalimbali ya mwili. Unaweza kujaa maji kwenye miguu, enka, usoi na hata mikono. Yatokana na kukusanyika kwa majimaji yasiyohitajika eneo husika. Makala yetu itajikita zaidi kwenye miguu kujaa maji na nini kifanyike kutibu shida yako.

Miguu yako inavimba kwa sababu kubwa mbili

1.Maji kujikusanya(edema)

Hapa inatokea pale tishu au mishipa ya damu inaposhikiia maji mengi kuliko inavotakiwa. Kukaa mda mrefu wakati unafanya kazi, au ukiwa kwenye ndege, mabadiliko ya homoni wakati wa mimba hata kusimama mda mrefu yaweza kupelekea hali hii.

Mwili wako kumbuka umetengenezwa kwa maji asilimia 60. Sasa inapotokea hakuna uwiano mzuri wa amji, inapelekea kiwango fulani cha maji kuegemea eneo lingine zaidi.

2.Kututumka(inflammation)

Hii inatokea pale tishu za miguu zinapochokozwa na kitu kigeni na hivo kuvimba. Ni kawaida eneo la mwili kuvimba pale kunapotokea hitilafu. Endapo utavunjika mfupa eneo la maungio, ama kuna baridi yabisi, lazima eneo husika livimbe kukupa ishara kwamba kuna shida.

Magonjwa na changamoto zinapelekea miguu kujaa maji

1.Moyo kufeli

Hii inatokea pale moyo wako unapokuwa dhaifu katika kupump damu kwenda maeneo mbalimbali ya mwili. Dalili zingine za kufeli kwa moyo ni pamoja na

  • pumzi kukata na kushindwa kupumua vizuri
  • mwili kuchoka sana
  • kukohoa kupita kiasi

2.Matatizo kwenye mishipa ya damu

Matatizo makubwa mawili kwenye mishipa ya damu ambayo kitaalamu tunaiata Deep vein thrombosis(DVT) na thrombophlebits yanaweza kupelekea miguu kuvimba. Ukiwa na hizi changamoto maana yake kuna kipande cha damu kimegamda kwenye mshipa na hivo kuzuia usafirishaji.

Muone daktari mapema endapo utaona dalili

  • maumivu kwenye miguu na mguu kuwa laini
  • ngozi kuwa nyekundu au blue
  • ngozi yenye hali ya joto kuliko kawaida
  • maumivu baada ya kukaa au kusimama mda mrefu
  • ngozi kuwa kavu na inayobabuka na
  • malengelenge kwenye ngozi ya mguu

3.Magonjwa ya figo

Figo zinapopata hitilafu kwa mda mrefu, zinafeli kufanya kazi yake ya kuchuja maji. Na matokeo yake kiwango kikubwa cha maji kinahifadhiwa kwenye mwili badala ya kutolewa nje.

Maji yanayobaki yanaweza kujikusanya kwenye miguu na mikono. Ukiwa na tatizo kwenye figo na kisha maji yamejaa waweza pia kupata dalili zingine kama

  • mwili kuishiwa nguvu
  • kushindwa kupumua vizuri
  • kiu kupita kiasi
  • kichefuchefu
  • kuwashwa na kutoa damu

4.Mimba

Kwa wajawazito wengi, mimba inapofikia wiki 25, inakuwa ni mimba kubwa na inaleta mgandamizo kwenye mishipa yako ya damu. Mgandamizo huu unapunguza kiwango cha damu kinachosafiri na hivo kupelekea miguu na mikono kujaa maji.

Endapo una mimba na umeona dalili hizi hakikisha unaenda hospitali haraka, kwani siyo dalili njema. Dalili mbaya ni

  • kuvimba kupita kiasi hasa maeneo ya macho
  • maumivu ya kichwa kupita kiasi
  • macho kushindwa kuhimili mwanga na kushindwa kuona vizuri

Kama umepata dalili za miguu kuvimba, kukosa pumzi baada tu ya kujifungua, ongea na daktari kama unaweza kuwa na changamoto ya moyo. Atakupangia vipimo na utapata uhakika wa afya yako.

5.Baridi yabisi na magonjwa mengine ya joints

Magonjwa haya yamegawanyika: Nitayaelezea kila moja na dalili zake

Gout

Gout ni ugonjwa unaosababishwa na kuongezeka kwa uric acid kwenye damu. Acid hii inapojikusanya maeneo ya maungio huleta maumivu makali sana na kupelekea eneo hilo kuvimba. Utajiona kama una gout endapo unaamka asbhi, dole gumba la mguuni lina maumivu makali kama sindano inachoma.

Osteoarthritis

Hii ni aina ya baridi yabisi ambapo mgonjwa anapata maumivu na kuvimba kutokana na kuchoka kwa maungio. Hii inawapat zaidi wazee

Rheumatoid arthritis

Ugonjwa huu ni aina ya baridi yabisi ambapo kinga ya mwili inapambana na tishu za mwili. Ugonjwa unaweza kumtokea mtu wa umri wowote.

Majeraha

Kama mfupa umevunjika, au enka kuteguka, inaweza kupelekea eneo hilo kuvimba. hii ni namna ya kawaida kabisa ya mwili kuvimba kutokana na shambulizi. Kitendo cha kuvimba ni ishara kwamba mwili unapambana kulitibu eneo husika.

Cellulitis

Haya ni maambukizi ya bakteria kwenye eneo la ndani la ngozi. Dalili zingine za cellulitis ukiacha kuvimba ni pamoja na

  • homa
  • maumivu ya ngozi
  • eneo la ngozi kutengeneza dimple yani mbonyeo
  • ngozi kuwa laini sana kupita kiasi
  • wekundu kwenye ngozi unaoongezeka kila siku

Nini cha kufanya endapo miguu yangu imevimba?

Unaweza kujaribu huduma hizi za kwanza wakati ukijiandaa kwenda hospitali

  1. Punguza vyakula vyenye chunvi
  2. Weka ratiba ya kufanya mazoezi mepesi kila siku
  3. Usikae mda mrefu bila kusimama na kutembea
  4. Kama una uzito mkubwa na kitambi, lenga kurekebisha uzito wako kwanza

Lakini kwasbaabu kuvimba kwa miguu kunaweza kuashiria tatizo kubwa la kiafya, usipuuze dalili zake. Hakikisha unaenda hospitali mapema kupimwa kujua shida iko wapi.

Bofya kusoma kuhusu: Miguu kuwaka moto

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *