Dawa ya Amoxicillin, Matumizi na madhara

amoxicillin
amoxicillin

Amoxicillin inatumika kutibu magonjwa mengi yanayosababishwa na maambukizi ya bakteria. Dawa hii kufupi ipo kwenye kundi la antibitiocs. Inafanya kazi kwa kuzuia bakteria kusambaa. Yafaa kutibu maambukizi ya bakteria pekee. Haifanyi kazi kwa maambukizi ya fangasi wala virusi.

Kutumia antibiotics kiholela inaweza kupeleka usugu wa dawa na ni hatari kwa afya yako. Amoxicillin pia inatumika pamoja na dawa zingine kutibu vidonda vya tumbo vinavyosababishwa na bakteria wa H.pylori na kuzuia usipate tena bakteria hawa.

Matumizi ya amoxicillin

Meza dawa kwa maji aidha ukiwa umekula au kabla ya kula kama ulivyoelekezwa na daktari, hasa kila baada ya masaa 8 au 12. Dozi utakayopewa hospitali itategema na hali yako ya kiafya na ugonjwa unaokusumbua.

Hakikisha unakunywa maji ya kutosha wakati unatumia amoxicillin mpaka pale daktari atakapokwambia vingine. Kupata matokeo mazuri meza dawa muda ule ule kila siku.

Endelea kumeza dawa mpaka umalize dozi yote uliyoandikiwa hospitali, hata kama dalili mbaya zitapungua mapema. Kuacha dawa mapema kunafanya bakteria kurudi na kukua tena na hivo maambukizi kurudi upya.

Matokeo/madhara ya amoxicillin (side effects)

Kichefuchefu. kutapika na kuharisha inaweza kutokea wakati wa dozi ya amoxicillin. Mjulishe daktari au mfamasia aliyekuhudumia mapema.

Kumbuka kwamba daktari amependekeza upate dawa hii kwasababu ameona kwamba faida utakazopata ni kubwa kuliko madhara ya dawa. Hata hivo wagonjwa wengi wanaotumia amoxicillin hawapati dalili zozote mbaya.

Kutumia amoxicillin kila mara yaweza kupelekea fangasi mdomoni au ukeni . Muone daktari mapema endapo utaona kuna utando usio wa kawaida mdomoni ama uchafu mzito mweupe ukeni.

Lini unatakiwa kumwona Daktari

Endapo utaona dalili za mkojo mchafu, kichefuchefu na kutapika, macho kuwa ya njano, maumivu makali ya tumbo na kutokwa damu , muone daktari mapema.

Aleji ya amoxicillin inatokea mara chache sana. Japo ni muhimu sana kurudi hospitali endapo utagundua viashiria vya aleji kama muwasho na kuvimba hasa kwenye ulimi, uso na koo, kushindwa kupumua na vipele.

Yawezekana pia ukapata dalili zingine mbaya ambazo hatujaziandika hapa. Ni muhimu kuripoti hospitali ili upate huduma.

Tahadhari kabla ya kutumia amoxicillin

Kabla ya kuanza tiba, mjulishe daktari au mfamasia anayekuhudumua endapo una aleji ya aina yoyote. Kama una aleji dawa hii yaweza kuleta mpambano na kukuathiri.

Kabla ya kutumia amoxicillin, mjulishe daktari historia ya afya yako. Mjulishe kama kuna dawa zozote unatumia, au kama unaugua magonjwa kama ya figo na magonjwa ya virusi.

Amoxicillin inaweza kupeleka baadhi ya chanjo kutofanya kazi, mfano chanjo ya typhod. Wakati wa dozi usipate chanjo yoyote mpaka umalize.

Pia kabla ua upasuaji, mjulishe daktari kama kuna dawa zozote unatumia , ikiwemo dawa za famasi na tiba asili.

Wakati wa ujauzito amoxicillin itumike tu pale inapohitajika. Usinunue na kumeza dawa yoyote famasi wakati una mimba bila kumshirikisha daktari.

Mwingiliano wa dawa ya amoxicillin na tiba zingine

Amoxicillin inaweza kuingia ufanisi wa dawa zingine. Ndio maana kuna umuhimu wa kumwambia daktari dawa zote, ikiwemo virutibishi na tiba za mimeza unazotumia. Hii itamsaidia daktari kufanya maammuzi sahihi kuhusu dawa za kukupatia.

Amoxicillin inaweza kusababisha majibu tofauti kwa mgonjwa ya kisukari kupitia kipimo cha mkojo. Dawa hii pia yaweza kuathiri baadhi ya vipimo vya maabara.

Bofya kusoma kuhusu Vidonge vya Misoprostol