Faida na Hasara za Uzazi wa Mpango

faida na hasara za uzazi wa mpango
uzazi wa mpango

Njia za uzazi wa mpango zinazotumiwa aidha na wanawake au wanaume ni zile zinazosababisha kuchelewa kutoa muda au kuzuia mimba. Japo baadhi ya dini hawakubaliani navyo ila kwa dharura(nami naunga mkono) zinafaa.

Zifuatazo njia za uzazi wa mpango.

1.Kumwaga mbegu nje (withdrawal)

Hapa mwanaume anautoa uume wake kutoka kwenye uke kabla ya kumwaga shahawa au kukojoa. Yani pale mwanaume anapohisi anakaribia kufika kileleni, basi anatoa uume haraka na kumwaga kwa pembeni.

Faida za njia hii ya kumwaga nje ni pamoja na

  • njia hii haina madhara yoyote,
  • haina gharama na ni ya haraka.

Hasara za njia hii ni pamoja na

  • ugumu kutambua mara zote muda wa kukojoa au kumwaga shahawa kwasababu unaweza kunogewa na utamu wa tendo la ndoa.
  • mwanamke anahitajika kumtegemea sana mwanaume kuzuia mimba.

2.Njia ya kalenda

Kwenye kufuata kalenda, wenza wanaamua kujamiiana kutegemea kupevuka kwa yai la mwanamke kwa kutofanya mapenzi siku za hatari.

Jinsi ya Kutambua siku za Hatari

Njia zifuatazo zitakusaidia kujua siku ya ovulation/siku za hatari ili uepuke kushika mimba kabla hujapangilia.

  1. Kwa miezi 8 mpaka 12 rekodi siku ambayo unaanza hedhi na uhesabau siku zote za kila mzunguko. Siku ya kwanza ni ile unayoanza hedhi katika mwezi husika na hesabu mpaka siku unayoanza hedhi katika mwezi mwingine hapo mzunguko mmoja utakuwa umekamilika.
  2. Rekodi mzunguko mfupi na mzunguko mrefu zaidi katika ufuatiliaji wako
  3. Kupata siku yako ya kwanza ya hatari chukua nama ya mzunguko mfupi zaidi toa 18, mfano mzunguko wako mfupi ni siku 27-18 inabaki 9.
  4. Kupata siku yako ya mwisho ya hatari kwenye mzunguko, chukua siku za mzunguko wako mrefu toa 11. Mfano mzunguko wako mrefu ilikuwa siku 30-11 inabaki 19.

Katika mahesabu hapo juu ni kwamba siku kati ya mzunguko mfupi na mrefu ndizo siku zako za hatari. Kwamaana ya kwanza siku kati ya 9 na 19 ndizo siku zako za hatari. Kama unataka usishike mimba basi usifanye ngono siku ya 9 ya hedhi mpaka siku ya 19.

Faida hasara za uzazi wa mpango wa kalenda

Faida za kutumia kalenda ni pamoja na

  • mwanamke anautambua mwili wake na mzunguko wa hedhi yake
  • ni njia salama isiyobadili homoni za mwili

Hasara za kalenda ni pamoja na

  • inahitaji ufatiliaji wa karibu zaidi
  • inataka umakini mkubwa
  • kujituma na kutafiti kwa makini
  • mwanamke awe na uhakika lini yai linapevuka
  • kujamiiana kunatakiwa kuepukwa kipindi cha siku za hatari.
  • uwezekano wa kushindwa ni mkubwa endapo hedhi inavurugika au mzunguko ni mrefu zaidi ya siku 32.

3.Uzazi wa mpango wa kondomu

Kondomu ni mpira uliotengenezwa nyenzo maalumu kwa ajili ya kuvaa mwanamke au mwanaume kipindi cha tendo la ndoa ili kuzuia shahawa kuingia kwenye uke wa mwanamke.

Faida za kutumia kondomu ni pamoja na : Kondomu ni njia pekee ambayo mbali na kuzuia mimba pia inazuia maambukizi ya magonjwa ya ngono pamoja na ukimwi. Kondomu ni rahisi kupatikana na bei ni nafuu sana.

Hasara za kondomu:

  • kondom mpya lazima itumike kwa kila tendo la ngono baada ya kukojoa au kumwaga shahawa.
  • inapunguza msisimko na ladha ya tendo la ndoa.
  • kondomu zaweza kuleta muwasho na aleji kwa baadhi ya watu.
  • kondomu yaweza kupasuka katikati ya tendo la ndoa, kutokana na msuguano mkali.

4.Vidonge vya uzazi wa mpango na sindano

Vidonge na sindano huwa na dawa ambazo zina vichocheo vinavyozuia mayai kupevuka na kutolewa. Pia kemikali hizi hufanya ute ute wa ukeni kuwa mzito sana kiasi ya kuzuia mbegu kuogelea.

Faida za vidonge na sindano

  • ni rahisi kutumia, ukichachoma mara moja mpaka miezi mitatu.
  • ni nafuu sana na huduma inapatikana hospitali zote

Hasara za vidonge na sindano za uzazi wa mpango

  • kuvurugika kwa hedhi ama kukosa kabisa hedhi
  • hamu ya tendo la ndoa yaweza kupungua
  • uzito waweza kuongezeka zaidi au kupungua sana
  • kuchelewa kushika mimba ingine baada ya kuacha kutumia
  • kumeza vidonge mara kwa mara na kuchoma sindano kila baada ya miezi mitatu, husababisha kichefuchefu, kuongezeka kwa hamu ya chakula na kuumwa kichwa.

5.Vipandikizi au vijiti

Vipandikizi ni vijiti vyembamba vidogo vinavyowekwa kwenye sehemu ya juu ya mkono wa mwanamke kwa njia ya upasuaji mdogo. Vijiti vina kichocheo kinachozuia kupevuka kwa mayai.

Faida za njiti kupanga uzazi:

  • Ni njia ya uzazi wa mpango inayofanya kazi kwa muda mrefu(inazuia ujauzito mpaka miaka mitano tangu kupandikizwa).
  • Vinaweza kutolewa wakati wowote na mwanamke akarudia hali yake ya kuzaa kama kawaida
  • Upatikanaji wake ni nafuu

Hasara na vijiti.

  • Vijiti vinavuruga homoni za mwili
  • inaweza kupelekea ukose hedhi ama hedhi kuvurugika
  • inahitaji upasuaji mdogo wakati wa kupandikiza na kutoa kipandikizi.
  • huleta hasira, huzuni, kunyonyoka nywele, majimaji ukeni na kuongezeka uzito.

6.Kitanzi au loop

Ni kifaa kidogo kiliyoundwa na aina maalumu ya plastiki ambacho huwekwa kwa utaalamu ndani ya mfuko wa uzazi. Hufanya kazi hadi miaka 10.

Faida za kutumia kitanzi:

  • ukiweka mara moja unakaa muda mrefu zaidi bila kuweka tena
  • haileti mabadiliko ya homoni kam njiti na sindano

Hasara za kitanzi:

  • lazima kiwekwe na mtaalamu wa huduma ya afya.
  • mtumiaji hupata damu nyingi ya hedhi kuliko kawaida
  • mtumiaji hupata maumivu makali kabla na wakati wa hedhi
  • uke huwa mlaini muda mwingi na
  • mwanamke hukosa hamu ya tendo.

Unahitaji maoni ama ushauri? Tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254 utajibiwa, Usipige simu namba ni ya whatsapp tu.

Bofya kusoma makala inayofuata kuhusu uzazi wa mpango wa asili kwa kufuata kalenda