Mazoezi ya kupumua kwa mgonjwa wa corona

kukosa uwezo wa kunusa ni dalili ya corona
virusi vya corona vinavyosababisha Covid-19

Ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona, hushambulia mapafu na mfumo wa hewa na kusababisha majeraha. Covid-19 kwa kiasi kikubwa inapelekea mtu apate nimonia na kushindwa kupumua vizuri. Kupona mapafu yako baada ya kuugua corona inaweza kuchukua muda na yahitaji tiba na kufanya mazoezi ya kupumua pia.

Hospitali ya chuo kikuu cha Tiba cha John Hopkins cha nchini Marekani kimependekeza mlolongo wa mazoezi ambayo mgonjwa wa corona anatakiwa kufanya ili apone mapema.

Faida za mazoezi ya kupumua kwa mgonjwa wa corona

Kuvuta pumzi ndefu husaidia kuimarisha uwezo wa mapafu. Kumbuka lengo ni kujenga uwezo wa kuvuta pumzi ndefu muda wowote ukiwa kwenye shughuli zako na siyo tu ukiwa umepumzika.

Pia zoezi la kuvuta pumzi ndefu linasaidia kupunguza msongo wa mawazo na wasiwasi, vitu ambavyo vinampata sana mgonjwa wa corona. Pia mazoezi yatakusaidia upate usingizi mzuri.

Mazoezi haya yanamfaa mgonjwa yeyote mwenye nimonia na siyo tu kwa covid-19. Japo mkazo zaidi tunaweza kwenye ugonjwa wa corona kwasababu virusi vyake zinaweza kusababisha madhara makubwa ya mapafu ndani ya muda mfupi. Mazoezi haya ya upmuaji unaweza kuanza kwa kuyafanya ukiwa peke yako umetulia, na baadae ukishazoea utafanya popote kwenye shughuli zako.

Tadhari kabla ya kuanza mazoezi haya

Usifanye mazoezi ya kuvuta pumzi, na pia nenda hospitali kwanza endapo

  • una homa kali
  • unashindwa kupumua vizuri ukiwa umelala
  • una maumivu ya kifua ama mabadiliko ya mapigo ya moyo
  • una uvimbe kwenye mapafu yako

Ukishaanza mazoezi na ukapatwa na dalili zifuatazo inatakiwa usitishe mara moja kufanya mazoezi. Dalili hizi ni pamoja na

  • kizunguzungu
  • kubanwa pumzi kusiko kawaida
  • maumivu ya kifua
  • kukosa nguvu
  • mabadiliko ya mapigo ya moyo
  • dalili yoyote ingine mbaya

Jinsi ya kufanya Mazoezi ya Kuvuta pumzi ndefu (deep breath)

Mazoezi ya kuvuta pumzi ndefu yatakusaidia kurudisha uwezo wa mapafu kwa kutumia ukuta unaotenganisha mapafu na tumbo yani diaphragm. Mazoezi yanajumuisha kushugulisha ukuta huu unaoshikilia mapafu.

Unapoanza mazoezi haya ili kurejesha hali nzuri ya upumuaji kutokana na maambukizi ya corona yatakiwa uende taratibu. Mazoezi yamegawanywa katika hatua 4. Hakikisha unamaliza zoezi moja na kulirudia ndipo uende kwenye zoezi la pili.

Hatua ya kwanza: Pumzi ndefu ukiwa umelala kwa mgongo.

mazoezi ya kupumua
  1. Lala kwa mgongo na ukunje magoti kama inavyoonekana kwenye picha
  2. Weka mikono yako juu ya tumbo
  3. Funga mdomo wako na weka ulimi kwenye ukuta wa juu wa mdomo
  4. Vuta pumzi ndefu kwa kutumia pua zako. Jaribu kusambaza vidole vya mikono tumbo kadiri hewa inavyoingia
  5. Taratibu toa pumzi nje kwa kutumia pua yako.
  6. Rudia zoezi kwa muda wa dakika moja

Hatua ya pili: Pumzi ndefu ukiwa umelalia tumbo

mazoezi ya kupumua kwa mgonjwa wa corona
  1. Lala kwa tumbo na unyooshe mikono yako mbele
  2. Fumba mdomo wako na weka ulimi eneo la juu la uvungu wa mdomo
  3. Vuta pumzi ndefu kwa kutumia pua yako. Kadiri unavovuta pumzi akili yako iweke kwenye tumb namna linavyosukuma godoro lako.taratibu vuta toa hewa nje kwa kupitia pua
  4. Rudia zoezi hili ka dakika moja

Hatua ya tatu: Pumzi ndefu ukiwa umekaa

  • Kaa kwa kubyooka kwenye kiti au kitanda
  • Weka mkono mmoja kwenye tumbo na mwingine kwenye kifua
  • Funga mdomo na weka ulimi kwenye ukuta wa juu wa mdomo
  • Vuta pumzi ndefu taratibu kupitia pua. Jaribu kusambaza vidole kadiri hewa inavyoingia
  • Taratibu toa hewa nje kupitia pua
  • Rudia zoezi kwa dakika moja

Hatua ya 4: Zoezi la Pumzi ndefu ukiwa umesimama

  • Simama wima na uweke mikono yako kwenye tumbo
  • Funga mdomo wako na uweke ulimi eneo la juu la mdomo
  • Vuta pumzi ndefu taratibu kupitia pua. Jaribu kusambaza mikono yako wakati hewa inaingia
  • Taratibu toa hewa nje kupitia pua
  • Rudia zoezi kwa dakika moja

Soma zaidi Dalili za Ugonjwa wa Covid-19 na namna ya kujikinga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *