Jinsi ya kujitunza baada ya kutoa mimba
Kutunza mwili na akili vizuri baada ya kutoa mimba ni jambo la muhimu sana. Kwenye makala hii nitakwelekeza namna ya kuhudumia mwili wako baada ya kutoa mimba pamoja na njia salama za kusafisha kizazi ili uwe na uwezo wa kuzaa siku za mbele.
Kutoa mimba ni hatari kwa afya yako
Kumbuka lengo langu, siyo kukuhamasisha wala kukushauri ukatoe mimba hapana. Kutoa mimba ni hatari kwani yaweza
Lengo ni kukusaidia afya yako irudi kuwa vizuri baada ya wewe kufanya hili tukio.
Endapo daktari ameshauri ufanyiwe abortion kitaalamu, hatari ya kupata madhara kwenye kizazi ni ndogo kwasababu daktari amefuata utaalamu wote kwenye kutoa mimba. Hapa ni kama una tatizo linalolazimu kufanyiwa hizo. Na siyo kunyofolewa mimba wakati huna tatizo lolote.
Tafiti zinasema kwamba mwanamke mmoja kati ya wawili hufanya abortion katika muda wao wa kuzaa kabla ya kufikisha miaka 45.
Njia za kutoa mimba hospitali
Daktari anaweza kupendekeza njia mbali mbali za kutoa mimba kulingana na afya yako. Njia hizi ni kama
- vidonge(abortion pill)
- vacum aspration
- dilation and evacuation (kutanua mlango wa kizazi na kiumbe kutolewa)
Nini cha kutegemea baada ya kutoa mimba?
Wanawake wote hupata dalili zinazofanana haijalishi njia gani imetumika kutoa mimba. Japo kama mimba iliyotolewa ni kubwa kuanzia miezi mi3 dalili huwa mbaya sana na mwanamke anaweza kupoteza maisha.
Baaada ya kutoa mimba, ni kawaida kwa mwanamke kupata dalili hizi
- kutokwa damu kwa wiki 3 mpaka 6, japo baadhi ya wanawake hawapati bleed kabisa
- Kutokwa na mabonge ya damu iliyoganda
- Maumivu makali ya tumbo yanyofanana na yale ya hedhi
- Maumivu na kuvimba matiti
Baada ya kutoa mimba hedhi yaweza kurejea baada ya wiki 4 mpaka 8, na kutakuwa na mabadiliko kwenye mwonekano na utokaji wa hedhi yako.
Baadhi ya wanawake hupata mabadiliko ya mood na hisia sana baada yakutoa mimba. Mabadiliko ya homoni yanaweza kuchangia na pia hisia zako na mawazo kuhusu jambo ulilofanya.
Uwezekano wa kushika mimba ingine baada ya abortion
Fahamu kwamba inawezekana ukashika mimba ingine mapema kabisa hata kabla ya kuona hedhi ya kwanza. Hii ni kwasababu hedhi inatanguliwa na yai kupevuka. Hivo ni muhimu usishiriki kabisa tendo au kutumia uzazi wa mpango ili usishike mimba ingine mapema.
Vipi kama nitachelewa kushika mimba ingine nifanye nini?
Asilimia 20 ya wanaotoa mimba, wanachelewa kushika mimba zingine. Wachache sana hawashiki tena mimba maisha yote baada ya kutoa, hasa waliotoa mimba kubwa. Na ndio maana tumeleta huduma ya kusafisha kizazi ili kukuokoa usije kukwama kushika mimba miaka ijayo. Hakikisha tu unamaliza dozi zote mbili tutakazokupatia.
Jinsi ya kujitunza mwili baada ya kutoa mimba
Siku chache baada ya kutoa mimba, utapatwa na uchovu mkubwa, mwili kuishiwa nguvu na maumivu ya tumbo mara kwa mara. Muhimu uwe na mtu wa kukusaidia kukupeleka hospitali, kukufulia nguo na kukupikia katika kipindi hichi, ili upate muda mwingi wa kupumzika.
Baada ya kutoa mimba utakuwa kenye hatari kubwa ya kupata maambukizi hasa PID. Kwa sababu inachukua muda kwa mlango wa kizazi kufunga. Kupunguza hatari hiyo nakushauri haya.
- usitumie tampon mpaka hedhi ijayo, tumia pedi ya kawaida kuvyonza bleed yoyote
- usifanye tendo kwa wiki mbili wala kuingiza kitu chochote ukeni kwa wiki ya kwanza
- kama unapenda kuogelea, usitumie swimming pool kwa wiki mbili.
Fanya pia mambo haya kuendelea kutunza mwili
- Masaji tumbo lako ili kupunguza maumivu ya tumbo na kusaidia kutolewa kwa mabaki ya mimba
- Tumia kitu cha moto kukanda tumbo ili kupunguza maumivu
- Tumia dawa zote ulizoandikiwa na daktari ikiwemo antibiotics
- Waweza kutumia dawa za famasi kupunguza maumivu kama ibuprofen. Maumivu yakiwa makali sana rudi hospitali uonane na daktari
- Fatilia joto la mwili wako kama utapatwa na homa urudi hospitali na
- Endelea kwenda clinic kufanyiwa vipimo ili kupata uhakika kwamba mabaki yote ya mimba yameisha na kizazi kimepona.
Muda gani inachukua Kupona Baada ya Kutoa Mimba?
Kupona baada ya kutoa mimba kunatofautiana kwa kila mwanamke. Kama ulitoa mimba ya chini ya miezi miwili utapona mapema ndani ya siku chache. Na damu inaweza kukata mapema ndani ya wiki 6.
Kama ulitoa mimba kubwa ya miezi mitatu au minne na kuendelea itachukua muda mrefu zaidi kupona. Baadhi ya wanawake watahitaji kulazwa hospitali na kufanyiwa upasuaji. Usiwe na hosfu kubwa kwasababu wanawake wengi hupona mapema na kurudi nyumbani.
Huduma ya kitabibu baada ya kutoa mimba
Wanawake wengi waliotoa mimba watahitaji kwenda clinic na kufatiliwa afya kwa wiki kadhaa. Kama hakuna dalili za changamoto zozote, uatendelea tu kujihudumia nyumbani bila ulazima wa kwenda clinic.
Wanawake watakaopata dalili mbaya ni muhimu kuweka appointment na daktari ili kupata huduma mapema. Japo ni mara chache sana inatokea, baadhi ya wanawake wanahitaji uangalizi wa hali ya juu.
Lini unatakiwa kumwona daktari?
Unatakiwa kwenda hospitali haraka endapo unapata dalili hizi
- damu inatokwa kwa wingi sana kiasi ya kutumia zaidi ya pedi moja kwa kila lisaa
- Unatokwa na mabonge makubwa ya damu, ukubwa wa kitenesi
- Kujihisi huna nguvu
- Unapata mawazo ya kujidhuru au kujiua
- kujisikia kukosa pumzi
- unapata harufu mbaya ukeni
- Homa kali
- Una hofu kwamba mimba haijatoka yote
Nini kitatokea endapo hutasafisha kizazi baada ya kutoa mimba
Madhara haya yanaweza kukupata endapo utatoa mimba na usisafishwe kizazi
- Kushindwa kushika mimba kwa miaka ijayo
- Kuziba kwa mirija ya uzazi
- Kuugua PID na fangasi mara kwa mara
- Kushindwa kufurahia tendo
- Maumivu chini ya kitovu na
- Kutokwa na harufu mbaya ukeni
Kwanini ni hatari kusafishwa kwa vyuma na kuchokonolewa kwenye kizazi?
Kwa tiba ya hospitali kusafisha kizazi kupitia vyuma, yaani kifaaa cha MVA+Dilation &evacuation, inaweza kusababisha makovu kwenye kizazi pamoja na kulegea kwa kizazi.
Kizazi kikilegea na kuwa na makovu inapelekea ushindwe kushika mimba mapema siku zijazo au mimba zijazo kutoka mapema kabla ya wakati. Pili gharama ya kusafisha kizazi yaweza kufika sh laki 1 na 50, hii yaweza kuwa kikwazo kwa wanawake wengine kufikia lengo la kusafisha kizazi.
Vidonge Asili vya Kusafisha kizazi vya Uterus cleasing pills(UCP)
Kusafisha kizazi ni jambo la msingi sana kwako, baada ya kutoa mimba ama mimba kuharibika na hasa kama una malengo ya kushika mimba kwa siku zijazo. Kwanini nakushauri kutumie ucp? kwasababu hizi
- Vidonge vya UCP vinagharimu pesa kidogo tu sh elfu 50 ukilinganisha na gharama ya kusafisha kizazi hospitali.
- Uwezo wa vidonge hivi vya UCP wa kusafisha ni mkubwa zaidi na ni rahisi kutumia.
- Kutumia vidonge vya UCP inakuepusha na maambukizi pamoja na makovu ambayo unaweza kupata wakati wa kuingiziwa kifaa cha kukusafisha hospitali.
- Vidonge vya UCP vinakusaidia pia kuongeza uzalishaji wa ute kwenye uke, ute ambao ni muhimu kufurahia tendo la ndoa.
Matumizi ya vidonge vya Ucp
UCP ni dawa asili yenye vidonge 2 (kwa dozi moja)kama vinavyoonekana kwenye picha hapo juu. Ambayo vinatumika kwa wiki moja, kwa kuweka kidonge ukeni na kutoa kila baada ya siku tatu. Kisha unapumzika masaa 24 unaweka tena kidonge kingine.
Vimetengenezwa kitaalamu kupitia muunganiko wa mimea na kuhifadhiwa vizuri ili kutunza uasili wa dawa pasipo kuwekwa kemikali.
UCP imetengenezwa kiasili ili kutatua changamoto mbalimbali za wanawake kama kusafisha mabaki ya mimba, kuzibua mirija, uchafu ukeni na PID.
Tahadhari
Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge vyenye mfanano na hivi vya UCP, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb.
22 replies on “Kusafisha Kizazi Baada ya Kutoa mimba”
Nina Mimba Ya Mwez 1 nawiki1 je yawezekana kutoa
Sory hatuna hiyo huduma
Kama mimba imetoka na baada ya wiki mbili nasikia maumivu chini ya kitovu,ni dalili ya nini?
Ni dalili ya PID (maambukizi kwenye njia ya kizazi) muhimu upate dawa ya kusafisha mapema, ili kuzuia athari kama mirija kuziba
dawa za kutumia kwa mtu aliyetoa mimba ya wiki tatu
Je iyo dawa ya kutoa mimba inapatikana clinic yoyote iliyo karibu nawe?
Dawa za kutoa mimba hatuna, na wala hatuna huduma za kutoa mimba
MTU AKIWA MIMBA IMETOKA YENYEWE NA HAKUSAFISHWA NA IMEPITA MIAKA, JE HII DAWA INAWEZA KUMSAIDIA KUSAFISHA KIZAZI?.
Dawa itamsaidia, japo tunashauri apate dozi kubwa ya vidonge vinne
Samahani, nilitoa mimba ya miezi tatu na sikusafishwa na sahihi niko na mimba ya miezi sita.je,nitakua na madhara yeyote siku ya kujifungua?
hapana, hakuna madhara, endelea tu kuhudhuria clinic
mm ni mwnadada wa miaka 26 nina ndoa yangu ..tumebahatika mtoto mmoja 2018, ila kila nkishika mimba inatoka , wakat mwngne nakuwa na mimba nkipima utrosound wanasema hawaon kitu,npo iringa mufindi napataje dawa imetoka mimba ya week 10
Pole kwa changamoto tafadhali tuandikie kwa namba yetu 0678626254 uanze tiba
Kama anatokwa na damu yenye halufu atakuwa salama na anaweza tumia dawa gani za antibiotic
Kama mimba imetoka yenyewe dawa yake ni nin?
Endapo bint katoa mimba na amefululiza kutokwa damu mpaka wik 8 je, tatzo ni nin na nin tiba yakuzuia uhatar wakuendlea kupoteza damu
huyu apelekwe hospitali ili apewe dawa ya kukata damu. Pia kunaweza kuwa na ulazima wa kusafishwa
Mm mke wangu aripata mimba yakwanza akakaa nayo mpaka miez 7 mimba ikatoka sasa mpaka saiz mwaka wa pir hapati mimba tatizo itakua nini
pengine mirija ya uzazi imeziba, ama pengine kuna tatizo lingine, cha muhimu ni kwenda nae hospital akapimwe kujua tatizo nini
Je, mke wangu alikuwa na mimba ya miezi miwili na ikatoka nini kilichosababisha?
Nlitoa mimba y miezi 3 na nusu alfu nkapelekwa hospitalini kuoshwa tumbo je inaweza niathiri baadaye?
Samahan nlitokwa mimba na staki kubebe nyingne nimetoka kwenye siku zangu zimepita siku9 naweza kufanya mapenzi au nitapata ujauzito