Bawasili Kwa Mjamzito

bawasili kwa mjamzito
bawasili

Bawasili ni nyama zinazotokea eneo la mkundu(haja kubwa) kutokana na kuvimba kwa mishipa midogo ya damu. Nyama hizi zaweza kuwa ndogo sana kama punje ya haragwe au zikawa kubwa zaidi kama tonge ugali na mtu mzima. Bawasili kwa mjamzito haina tofauti na ile ya kawaida.

Aina za Bawasili

Bawasili ya ndani: hizi vimbe zinazojitokeza eneo la ndani la mkundu na hazionekani kwa macho lakini zinasababisha maumivu makali sana kwa mgonjwa husika.

Bawasili ya nje: hizi ni vimbe zinaota kwa nje ya mkundu kwa pembeni, ama zinaweza kuota ndani ya mkundu na zikatoka nje.

Je bawasili kwa Mjamzito ni Tofauti?

Ukweli ni kwamba hakuna mtu anapenda kuongelea kuhusu bawasili na ndio maana unaitwa ugonjwa wa aibu. Bawasili ni kuvimba tu kwa mishipa midogo ya damu kwenye eneo lako la mkundu. Baada ya kuzaa mishipa hii inaweza kuachia na bawasili ikaisha kabisa.

Kwanini wajazito ndio huugua zaidi bawasili?

Japo kila mtu anaweza kuugua bawasili lakini inawapata zaidi wenye mimba hasa katika miezi mitatu ya mwisho(third trimester) yani week 28.
Kuongezeka kwa msukumo wa damu kwenye eneo la nyonga na mgandamizo unaletwa na kiumbe cha tumboni husababisha mishipa midogo ya damu kwenye mkundu kuanza kuvimba.

Bawasili pia inaweza kusababishwa na mjamzito kukosa choo ama kupata cho kigumu sana. Choo kinapokuwa kigumu kinakufanya utumie nguvu kubwa kujikamua ili kukitoa. Wajawazito wanapata sana shida ya choo kutokana na kupanda kwa homoni ya progesterone wakati huu wa mimba.

Mabadiliko ya homoni huchangia bawasili kwa mjamzito

Homoni ya progesterone hufanya misuli ya mwili ikiwemo ya kwenye utumbo kulegea na kusukuma chakula taratibu sana, kiasi ya chakula kutosagwa haraka na hivo kukuletea dalili za kukosa choo au cho kigumu na kiungulia.
Kama uliwahi kuugua bawasili kabla hujashika mimba, waweza kupata tena bawasili ukishapata mimba.

Dalili za bawasili kwa Mjamzito

Dalili za bawasili hutegemea na aina ya bawasili inayokusumbua.Utajisikia hali hizi

 • kutokwa damu wakati wa kutoa haja kubwa
 • maumivu makali wakati wa kutoa haja kubwa
 • uvimbe kwenye eneo la haja kubwa, utagundua pale unaponawa baada ya kujisaidia
 • muwasho mkunduni na
 • kujisikia kuungua katika eneo la mkundu

Je bawasili inaisha yenyewe baada ya kujifungua?

kwa wanawake wengi bawasili huisha yenyenyewe baada ya kujifungua bila kutumia dawa.

Unawezaje kujikinga usipate bawasili wakati wa ujauzito

Hatua zifuatazo zitakusaidia kupunguza hatari ya kuugua bawasili wakati wa ujauzito.

 1. Pendelea kula vyakula vyenye kambakamba kwa wingi kama maparachichi, matunda , maharage na mboga za majani katika kila mlo
 2. Usijizuie kwenda chooni pale unapobanwa na haja kubwa
 3. Usitumie vyoo vya kukaa vinakufaya ujikamue sana kutoa haja
 4. Kunywa maji ya kutosha kila mara
 5. Usitumie muda mwingi kukaa ama kusimama
 6. Fanya mazoezi mepesi haya ya kutembea muda wa asubuhi na jioni
 7. Wakati wa kusoma au kupumzika lala kwa upande kwa kuweka mto chini ya tumbo na kichwani

Tiba ya bawasili ukiwa nyumbani kwako

Kuna njia nyingi unaweza kufanya kupunguza makali ya bawasili ukiwa nyumbani pasipo kumeza dawa. Njia hizi ni

 • Kupakaa mafuta ya black seed kwenye eneo la mkundu mara tatu kwa siku
 • Sitz bath-weka maji ya uvuguvugu kwenye beseni kubwa, weka maji na chumvi kisha vua nguo na ukalie maji haya kwa nusu saa
 • Tumia kipande cha barafu kwa kufunga kwenye kitambaa na uweke eneo la mkundu kwa dakika chache kupooza maumivu
 • Fanya zoezi la kegel ili kutanua mishipa ya damu na kurhusu damu kutemebea vizuri: namna ya kufanya, ukienda kukojoa bana mkojo wa sekunde 10 kisha uachie , fanya hivo mara tatu kila unapoenda kukojoa.
 • Chukua maji ya aloevera pakaa kwenye eneo a mkundu mara tatu kwa siku

Tiba ya hospitali kwa mjamzito mwenye bawasili

Kama tatizo ni kubwa sana, utahitaji kumwona daktari ili kupatiwa tiba ya bawasiri yako. Hospitali utapewa tiba stahiki kwa kulingana na aina ya tatizo lako.

Wakati wa ujauzito usimeze dawa zozote bila kumshirikisha daktari kwani unaweza kupelekea mimba kuharibika. Hata dawa za kupaka kwenye ngozi zinaweza zisiwe salama kwa upande wako.

Daktari anaweza kupendekeza kukupa tiba ya kupakaa eneo la mkundu au vidonge vya kuingiza mkunduni kutibu bawasili yako.

Njia zingine Kutibu Bawasili kwa mjamzito-hospitali

Rubber band litigation-tiba hii inafaa hasa kwa bawasili ya nje ambayo ni kubwa. Uvimbe unafungwa kwa raba ndogo ili kuzuia damu kuwenda kwenye uvimbe, na baada ya hapo uvimbe utakatika wenyewe. Tiba inachukua siku 10 mpaka 12 kupona. Baada ya kinyama kuanguka litabaki kovu ambalo litazuia kuvimbe tena eneo lilelile.

Sclerotherapy- Tiba hii inafanyika kwa kemikali ya dawa kuchomwa na kuingizwa kwenye uvimbe wa bawasili ili kufanya uvimbe kupungua na kubaki kovu. Baada ya tiba hii kuna uwezekano wa uvimbe kurudi tena .

Hemorrhoidectomy-Ni upasuaji unaofanyika ili kuondoa uvimbe wa bawasili. Tiba hii inaweza kupelekea hatari ya kuvuja dmau sana, hatari ya kuathiriwa kwa misuli ya karibu ya mkundu na kuleta maumivu makali. Pia upasuaji huchukua muda mrefu zaidi kupona. Ndiomaana tiba hii hufanyika kwa bawasili iliyofikia hatua mbaya pekee

Hitimisho

Kuugua bawasili wakati wa ujauzito ni jambo la kawaida na linawatokea wanawake wengi. Nenda hospitali mapema endapo utaona shida ni kubwa na imegoma kupona kwa tiba mbadala za nyumbani. Baada ya kujifungua kuwa na uhakika kwamba bawasili itaisha yenyewe na utapona kabisa.

Tumia mafuta tiba ya black seed

tiba ya bawasili
mafuta tiba ya bawasili kwa mjamzito

Mafuta tiba haya hutengenezwa kupitia mbegu za black seed. Yanazalishwa zaidi nchini Pakistan kwa ajili ya kutibu bawasili na miwasho mkunduni. Huhitaji kuagiza nje ya nchi maana tayari tumekuletea tiba asili na salama.

Matumizi: Kutibu bawasili yako, osha eneo la haja kubwa kwa maji kidogo yenye chunvi, kisha pakaa mafuta tiba haya mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni. Tumia hivyo kwa wiki mbili utapona.

Tembelea ofisi zetu hapa magomeni, ama ulipie tukutumie kwa mkoani.

Gharama za mafuta tiba haya ni Tsh 40,000/= Tuandikie whatsap no- 0678626254

Bofya kusoma kuhusu: Kuvimba miguu na mikono kwa mjamzito

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *