Kujamba Sana Baada ya Kujifungua

kujamba sana baada ya kujifungua
kujamba

Mwili wako unapitia mabadiliko makubwa saa baada ya kujifungua, na hiyo ni kawaida kwa kila mwanamke. Mabadiliko mengi hayaishi baada ya mtoto kuzaliwa. Ukiacha kutokwa na damu, matiti kujaa, kutokwa jasho usiku, pia waweza kuanza kujamba sana baada ya kujifungua.

Hapa chini ni maelezo kwanini hali ya kutokwa na gesi chafu inaongezeka zaidi baada ya kuzaa, na vitu vya kufanya ili kupunguza hali hiyo.

Je kujamba sana baada ya kujifungua ni kawaida?

Kama unapata hali ya kutokwa na gesi kupita kiasi baada ya kuzaa, haupo peke yako. Japo hujui hili, pengine hukuambiwa na manesi hositali, ila tambu ani jambo la kawaida baada ya kujifugua.

Nini kinapelekea kujamba sana baada ya kujifungua?

Kuna sababu nyingi zinazopelekea upate gesi nyingi, sababu hizi ni pamoja na kuteguka kwa misuli ya mkundu na nyonga. Misuli ya nyonga inahimili uzito mkubwa sana wakati wa ujauzito.

Wakati wa kujifungua, pale unavopush mtoto atoke, unaweza kujeruhi misuli ya kwenye mkundu. Majeraha haya yanaweza kupelekea ushindwe kubana hewa chafu.

Tafiti zinaonesha karibu nusu ya wanawake wote wanaojifungua wanapata majeraha kweye misuli ya mkundu.

Madhara yanayotokana na misuli kulegea

Baada ya kujeruhi misuli hii, inaweza kuleta madhara kama

  • kuhisi haja kila baada ya dakika chache
  • kutokwa na choo bila hiyari
  • kushindwa kujizuia kujamba
  • kutokwa na damu mkunduni

Dalili hizi, hasa hasa kujamba sana, zinatokea zaidi kwenye miezi ya mwanzo baada ya kujifungua.

Kukosa choo na kupata choo kigumu

Ni kawaida kutopata choo kwa wakati kwenye siku za mwanzoni baada ya kuzaa. Kama unahisi tumbo kujaa gani na linauma, inawezekana kuna shida ya mfumo wa chakula tumboni. Tatizo litaalamu huitwa constipation. Hii inawapata wote waliojifungua kwa kisu au kwa njia ya uke, na inaweza kuchukua mda kuisha.

Dalili za Constipation ni Pamoja na

  • kupata choo kidogo kama cha mbuzi mara kwa mara
  • kupata choo kigumu sana
  • tumbo kujaa gesi
  • tumbo kufurukuta
  • maumivu wakati wa kutoa haja
  • kwenda choo unakunya lakini bado unajisi kama choo hakijaisha

Dawa Zinachangia Upate Choo Kigumu

Daktari anaweza kupendekeza utumie virutubishi vyenye madini chuma kwa wingi endapo ulizaa kwa kisu. Madini chuma yanachangia kwa kiasi kikubwa kupata choo kigumu.

Kama tatizo litaendelea kwa zaidi ya siku 4 jitahidi urudi hospital haraka. Tambua pia baadhi ya dawa za maumivu unazotumia baada ya kuzaa, zinaweza kupelelekea ukose choo na choo kigumu.

Lishe na mtindo wa maisha Vinachangia kujamba sana baada ya kujifungua

Baada ya kujifungua mama anaanza kula sana. Hata vile vyakula alivyokinai wakati wa mimba sasa anakula vizuri bila kujizuia. Mahitaji ya maziwa yanaongezeka kwa mtoto, hivo inamlazimu mama nae kula kwa kasi

Vyakula vyenye kambakamba(fibers) kwa wingi vinapeleke gesi na kujamba. Sasa unapotaka kutibu tatizo hebu cheki na aina ya vyakula. Tazama list hapa chini urekebishe

  • maharagwe
  • maziwa
  • nafaka
  • mboga jamii ya kabeji
  • matunda kama apple na peasi
  • bublish na pipi
  • vyakula vilivyosindikwa kama maziwa, soda nk

Je kujamba ni jambo baya?

La hasha, kujamba i jambo la kiafya kabisa. Mtu mzima ajamba mara 18 kwa siku, tena nyakati zingine unajamba hata bila kujitambua. Lakini kujamba kupita kiasi na bila kujiuzia hapo kuna shida. Kwanza unakosa kujiamini mbele za watu na mbele ya mpenzi wako nyakati za tendo.

Endapo umejifungua hivi karibuni na umeanza kupata maumivu ya tumbo, hakikisha unafika hospital haraka. Sometime maumivu ya tumbo siyo tumbo la chakula, bali ni kiashiria cha tatizo lingine.

Ni zipi dalili mbaya kuhusu tumbo langu?

Dalili mbaya ni pale maumivu ya tumbo yanapoambatana na dalili kama

  • kutokwa na damu nyingi
  • homa kali zaidi ya nyuzijoto 38
  • maumivu makali ya tumbo la chini ya kitovu na
  • kutapika

Kama una dalili za kushindwa kujizuia choo, ni jambo jema kama utajieleza kwa daktari akufanyie vipimo tena.

Dawa na Tiba kwa Choo Kigumu

Endapo shida ya kutoa gesi chafu mara kwa mara itaendelea kwa zaidi ya miezi kadhaa, unatakuwa kuonana na daktari kupata vipimo na tiba. Tiba atakayokupa daktari itategemeana na chanzo cha gesi.

Daktari anaweza kupendekeza ubadili lishe yako au kutumia dawa za kulainisha choo.

Kwa tatizo la kushindwa kujizuia haja kubwa, unaweza kujaribu mazoezi ya nyonga, kwa kufata mwogozo utakaopewa na daktari wako

Huduma ya kwanza ukiwa nyumbani

Kujamba kutokana na tumbo kujaa gesi na kukosa choo ni jambo la la aibu ukiwa na watu. Jambo zuri ni kwamba kuna hatua waweza chukua kupunguza tatizo.

Fanya haya

  1. Kunywa maji ya kutosha walau glass 10 kwa siku
  2. Tumia vunywaji vya moto kama green tea kila asubuhi
  3. Pata muda mwingi wa kupumzika hasa pale mtoto anapolala
  4. Kula zaidi mbogamboga za kijani: licha ya kuwa na kambakamba nyingi kwenye mboga za kijan, pia kuna madini mengi ya magnesium ambayo husaidia katika ufanyaji kazi mzuri wa misuli na hivo kupunguza tatizo la constipation.
  5. Jaribu kutumia dawa za kulainisha choo ndapo tatizo litaendelea

Endapo unakosa choo baada ya kujifungua kwa kisu fanya haya

  • usianze kutumia dawa za madini chuma mpaka upate choo cha kwanza baada ya kujifungua
  • jaribu kutembea kidogo walau dakika kumi, usilal tu mda wote
  • tumia kitu cha uvuguuvugu eneo la tumbo nb usiweke nguo maana yaweza kulowanisha kidonda. unaweza kuwea chupa yenye maji moto

Mazoezi ya kukaza misuli ya nyonga na mkundu

Unaweza kuanza mazoezi madogo ya kukaza misuli ya nyonga baada ya kujifungua. Chukua hatua hizi

Ongea na nesi au daktari akwelekeze namna ya kufanya mazoezi ya kegel au fuata hatua hizi.

  1. Ukiwa umekaa au umechutama
  2. Jifanye kama unazuia haja kubwa ama unajisuia mkojo, fanya hili zoezi hata kama hujiskii kwenda haja
  3. Fanya zoezi mara tatu kwa siku au zaizi. na kila zoezi fanya seti 8 mpaka 12, kwa kubana misuli na kuachia baada ya swkunde 6-8
  4. Jitahidi kufanya zoezi mara 3 mpaka 4 kwa wiki
  5. Kumbuka huwezi kuona matokeo haraka, inachukua mda mpaka miezi kadhaa.

Hili zoezi la kufaya kama unabana haja, unaweza kulifanya popote hata ukiwa ofsini bila mtu yeyote kujua. Unaweza kufanya pia ukiwa ndai ya gari kila unapokutana na taa nyekundu unabana mpaka taa zikiruusu unaachia.

Soma makala inayofuata kuhusu: Siri za kufurahia tendo la ndoa baada ya kujifungua