Tumbo kujaa wakati wa hedhi

Tumbo kujaa wakati wa hedhi na maeneo mengine ya mwili kitaalamu(bloating) ni dalili inayowapata wanawake wengi sana. Unapatwa na hali fulani kama vile umeongezeka uzito na tumbo kuvimba.

Kujaa tumbo huku hutokea hasa siku chache kabla ya kuanza hedhi na kuisha baada ya hedhi kuisha. Japo ni ngumu kuzuia kabisa hali hii kujitokeza lakini kuna mambo unaweza kufanya kapunguza ukubwa wa tatizo.

Hatua tano za Kupunguza Tumbo kujaa wakati wa hedhi

Hizi hapa chini ni hatua tano za kufuata ili kupunguza tumbo na mwili kujaa wakati wa hedhi

 1. Kula chakula sahihi wakati wa hedhi
  Unatakiwa kupunguza kula vyakula vyenye chumvi kwa wingi. Vyakula vilivyosindikwa vina chumvi nyingi sana kuliko kawaida na pia vina viambata na kemikali zisizo salama kwa afya yako, punguza kutumia vyakula hivyo.
  Pendelea zaidi kutumia mboga za majani kwenye kila mlo, vakula vya nafaka isiyokobolewa, karanga, mbegu za maboga na samakai.
 2. Kunywa maji ya kutosha: Hakikisha unakunywa maji ya kutosha unapoanza kukaribia hedhi. Kama ni mvivu wa kunywa maji, unaweza kubeba chupa ndogo ila mahali unapoenda unakunywa kidogo kidogo. Hakuka kiwnago fulani unachotakiw akunywa, ila tu hakikisha unakunyw akutokana na kiu yako na aina ya mazingia uliyopo na usinywe chini ya glass 8 kwa siku.
 3. Usitumie pombe na caffeine
  Madaktari wengi wanaamini kwamba pombe na vyakula na vinywaji vyenye caffeine kwa wingi kama kahawa, energy drink na chai ya rangi vinaongeza ukubwa wa tatizo la tumbo kujaa wakati wa hedhi. Jaribu kabadili kwa kunywa maziwa ya asili.
 4. Fanya mazoezi mara kwa mara: Mazoezi ya viungo ni muhimu katika kupunguza dalili mbaya za hedhi. Tenga muda walau nusu saa kila siku kwa mazoezi madogo ya kutembea na kukimbia pia.
 5. Tumia dawa endapo tatizo litazidi: Endapo umejaribu baadhi ya njia hapo juu na hazijakusaidia, unaweza kutumia dawa kupunguza ukubwa wa tatizo. Hakikisha unaongea na dakari kabla ya kuamua kutumia dawa zozote.

Nini kinasababisha tumbo kujaa wakati wa hedhi?

Jibu la haraka ni mabadiliko ya homoni. Kabla ya hedhi mwili huzalisha zaidi homoni za estrogen na progesterone ambazo zinafanya ukuta wa kizazi kujengeka. Ukuta huu unaongezeka kwa maandalizi ya kubeba mimba itakayoingia.

Pamoja na mabadiliko ya homoni vitu vingine vinavyochangia tumbo kujaa ni pamoja na

 • aina ya dawa na virutubishi unavyotumia
 • vinasaba vyako
 • lishe yako hasa kama watumia zaidi vyakula vya chumvi na
 • aina ya vinywaji unavyotumia kama vina caffeine na pombe.

Muda gani watakiwa kumwona daktari?

Unatakiwa kumwona daktari endapo kama tatizo halijaisha baada ya hedhi kuisha na kama tatizo ni kubwa kiasi cha kukuzia kufanya kazi zako za kila siku. Kujaa sana kwa tumbo na mwili wakati mwingine yaweza kuwa kiashiria cha tatizo kubwa la kiafya litakalohitaji matibabu. Mfano wa changamoto ni uvimbe au tatizo la ini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *